Tanesco haikutoza kodi ya Sh Bil 17 kwa posho zilizo lipwa kwa watumishi wake CAG-2020/2021

Kawegere

Member
Aug 4, 2011
20
0
Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332 (kama ilivyorekebishwa Mwaka 2019) kinasema kuwa, mapato ya mtu binafsi kutokana na ajira kwa mwaka wa mapato yatakuwa faida aipatayo mtu huyo kutokana na ajira ya mtu huyo kwa mwaka wa mapato.
Aidha, Kifungu cha 7 (3) (k) cha Sheria hiyo kinaeleza kuwa katika kukokotoa faida aipatayo mtu binafsi kutokana na ajira, posho ambazo hazijumuishwi (posho zisizo za kodi) ni posho ya nyumba, posho ya usafiri, posho ya uwajibikaji, posho ya kazi ya ziada, posho ya muda wa ziada, posho ya mazingira magumu, na honoraria kwa mtumishi wa Serikali au taasisi ambazo zinalipwa kutokana na bajeti ya vyanzo vingine vya mapato, yaani bajeti isiyotokana na ruzuku kutoka Serikalini.
Hata hivyo nilipopitia makato ya kodi ya mishahara kwa watumishi wa kudumu, watumishi wa mkataba, na watumishi wa muda kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021, nilibaini posho za wafanyakazi zenye jumla ya shilingi bilioni 61.64 hazikukatwa kodi (shilingi bilioni 53.57 kwa wafanyakazi wa kudumu na shilingi bilioni 8.07 kwa watumishi wa muda) ambazo ni faida kwa wafanyakazi.
Hali hii ni kinyume na Sheria ya Kodi ya Mapato kama ilivyoelezwa hapo juu hivyo kusababisha kutopelekwa kodi ya shilingi bilioni 17.40 katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (shilingi bilioni 15.50 kwa wafanyakazi wa kudumu na shilingi bilioni 1.90 kwa wafanyakazi wa muda).
Hali hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa gharama kwa Shirika na faini inayoweza kutolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kutowasilisha makato ya kodi kwenye posho za wafanyaka-CAG report 2020/2021
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom