Tanesco-EWURA kuna nini?

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
319
68
Kwanza Tanesco wamepandisha gharama za kuunganishia umeme wateja kwa zaidi ya 200%
EWURA wamekataa ongezeko hilo
Tanesco kasitisha huduma uunganishaji wa umeme kwa wateja akidai gharama anatotumia ni kubwa kuliko anayopata

Wananchi wanalalamika ongeeko ni kubwa mno

EWURA ni shirika la Serikali au?
Tanesco ni Shirika la Serikali au?

Kama ni ya serikali si yanapata ruzuku ambazo ni kodi za wananchi

Leo hii mwanachi anaambiwa akanunue vifaa vyake mwenyewe ambavyo hata hivyo madukani havipatikani, urasimu Tanesco ni mkubwa sana hapa kuna watu wanaitwa vishoka ktk kila offisi ya Tanesco kuna watu huwa pale nje wako maalumu kwa kazi za rushwa za wakubwa ndani ya ofisi. Hawa si wafanyakazi wa tanesco bali ni wasaidizi wa maofisa wa Tanesco katika rushwa. Mteja akiingia ndani atakutana na tangazo hakuna huduma za uunganishaji umeme akitoka tu anakutana na hao vishoka

Haya malumbano ni dili kwa vishoka ambao ni vibaraka wa maofisa wa tanesco;

Maisha bora ni ndoto kwa hali hii
 
Tanesco yapingwa

2007-11-16 09:00:12
Na Joseph Mwendapole

Baadhi ya wananchi wamepinga mapendekezo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kutaka kupandisha gharama za kuunganisha umeme kwa zaidi ya asilimia 200.

Endapo mapendekezo hayo yatakubaliwa, gharama hizo zitafikia Sh. 563,271, wakati awali ilikuwa Sh. 200,000.

Wakizungumza na Nipashe jana, wananchi hao walisema endapo shirika hilo litapandisha gharama hizo, wengi watashindwa kuzimudu.

Bw. Bakari Kiembe, mkazi wa Mwananyamala alisema kama mapendekezo hayo yatakubalika, nishati hiyo itakuwa kama anasa.

Alisema watu wa kipato cha chini hawatamudu gharama za kuunganishiwa umeme kwa kiasi kilichopendekezwa na shirika hilo.

Alisema uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukipigwa vita na serikali utaibuka kwa kasi kwa kuwa wananchi hawatakuwa na nishati mbadala.

`Mtu anajibana anajenga kajumba kake miaka kumi ndipo anamaliza na akitaka umeme unamwambia atoe Sh. 500,000 atazitoa wapi,` alihoji.

Mkazi mwingine wa Sinza, Bw. Ayubu Mtemi, alisema kupanda kwa gharama hizo ni matokeo ya shirika hilo kutokuwa na mshindani.

Alipendekeza litafutwe shirika lingine litakalokuwa likitoa huduma kama ya Tanesco ili kuondoa ukiritimba.
Bw. Mtemi alisema shirika hilo ni la umma na linapaswa kutoa huduma ambayo haiwaumizi wananchi wake lakini halifanyi hivyo.

Alisema lazima serikali iingilie kati na kutupilia mbali mapendekezo hayo kwa kuwa huduma ya umeme ni ya lazima tofauti na zingine.

`Angalau huduma ya simu unaweza kupandisha gharama kwa kuwa kupiga simu mtu anaweza kujibana, lakini suala la umeme ni lalazima,` alisema.

Aliongeza kuwa endapo mapendekezo hayo yatakubaliwa, mpango wa serikali kuwapatia nishati hiyo watanzania wengi ifikapo mwaka 2010 utakuwa ni ndoto.

Bw. Juma Mulla, wa Manzese alisema ni wakati muafaka kwa serikali kufikiria kuliuza shirika hilo kama ilivyofanya kwa mengine.

Hata hivyo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imekataa mapendekezo ya Tanesco mpaka itakapofanya mijadala na wananchi watoe maoni yao.

Kutokana na kukataliwa kwa ongezeko hilo, Tanesco imeamua kusitisha shughuli za kuwaunganishia umeme wateja wapya, mpaka mazungumzo yake na EWURA yatakapokamilika.

Katika ofisi mbalimbali za shirika hilo jijini Dar es Salaam, matangazo yamebandikwa yakielezea kuwa, huduma hizo zitaanza kutolewa itakapoamuliwa baadaye.

`Malipo mapya na yale ya zamani, yamesitishwa mpaka itakapotangazwa upya baadaye,` lilisema sehemu ya tangazo moja katika ofisi za Mkoa wa Ilala.

Tangazo hilo pia lilisema kuwa, hata fomu za maombi ya mwanzo, hazitatolewa kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limesema wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme watatakiwa kununua vifaa wao wenyewe.

Meneja Uhusiano wa shirika hilo, Bw. Daniel Mshana, alinukuliwa akisema juzi kuwa wakati wakiendelea kujadiliana na EWURA, wateja watakaotaka kuunganishiwa umeme watalazimika kununua vifaa wao wenyewe.

source Nipashe
 
..umeme ushakuwa anasa!

..kwa mtindo huu maendeleo yatakuwa magumu sana kupatikana!

..ina maana hata bei ingepanda mara dufu,basi tu,labda ewura wamekataa!
 
watanzania tunapelekwa kushoto kulia ilimradi siku inapita hakuna penye nafuu,imekuwa ukiwa na shida ya mguu wenzako wana kupasua kichwa.
Hebu tuangalie ni vitu gani ambavyo tanesco huwa wanavitoa wakati wa kukuunganishia umeme kwa mteja wa kwanza na kama kuna mtu anajua gharama zake basi aziweke hapa.
1,bracket au bomba lenye urefu wa kama mita mbili
2,waya mm 18 kutoka kwenye nguzo kuu ya umeme mpaka kwenye nyumba,ni mita si zaidi ya mita hamsini yaani 25 each one
3,bodi au kibao cha kuwekea mita
4,vikombe kwa ajili ya kufungia waya vinne
Kama nimesahau mnaweza kuongezea,hivi ni vitu ambavyo vitatumika kwa miaka zaidi ya hamsini baada ya kufungwa.
Tatizolipo kwa tanesco wakati wanapotoa tenda kwa ajili ya kuagiza hivi vifaa huwa wanacheza mchezo hapa kati wa maofisa wa tanesco na mtu wa tenda kwa kuweka bei ya juu kuliko gharama halisi ya vifaa vyenyewe na ili ndio tatizo lilipo na si mahali pengine.
Naomba hao EWAUR watupe gharama halisi na wafanye utafiti wa kina ilikujua tatizo.
 
Hapa ndipo unyonyaji mkuu ulipo.
Tenda za ununuzi wa vifaa vya Tanesco huenda kweli zina mushkeli. Haiwezekani gharama zipande kwa % zote hizo kwa wazalishaji wote wa vifaa vya uunganishaji umeme duniani, hata mtoto wa shule ya msingi anajua hili haliwezekani kamwe. Inawezekana hawa jamaa wana 'single supplier' ambaye ana uhusiano nao usio wa kawaida, hivyo wanapanga bei. Huu ni wizi wa mchana kweupe.
 
Huwezi kukuza uchumi wa Taifa lako wakati sekta muhimu kama ya nishati unaikimbiza toka kwa wananchi wajasiriamali........

Wewe Tanesco unafikiri hivi viwanda vidogo vidogo vitaendeshwa vipi ikiwa unavipa ugumu wa kupata nishati hii.

Tanesco mnatakiwa kuawapa uwezo wananchi wa kipato cha chini ili waweze kuzalisha na wapate uwezo wa kulipa hizo Bills na connection charges.

Sikatai gharama za uendeshaji zaweza kuwa kubwa kwenu Tanesco.............BUT how do one solve this problem.............sidhani kw akupandisha bei ndio mtakuwa mmesolve tatizo NO WAY...............Tanesco inabidi muwe na wateja wengi wa kulipa umeme ili muweze kujiendesha....................and only if kama utapunguza bei ya connection ndio utawapata wateja wengi.
Yes unaweza kusema gharama za kuunganisha say ni $300........fine......lakini mwambie mwananchi toa say $150 tutakuunganishia umeme and within say 6months/1Year uwe umemaliza deni lako la $150...................mkipenda mwaweza (Tanesco) kuweka hata %ge interest depending na time ya ulipaji hapo unakuwa umemuwezesha mwananchi at the same time pato la Tanesco linaongezeka.

anayewashauri muongeze gharama kama mnavyotaka huyo ANALIUA SHIRIKA.....kwa mtakuw ana wateja wachache wakubwa
 
Ewura, Tanesco wavutana vikali

2007-11-20 10:10:56
Na Mwandishi Wetu

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), wameanza kukutana kujadili kupandisha viwango vya gharama vya kulipia umeme kwa wateja wake.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na malalamiko makubwa kutoka kwa wateja ambao wanapinga ongezeko la mara kwa mara la bei ya umeme nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, vikao hivyo vilianza jana mkoani Mbeya na kikao cha mwisho kitafanyika mkoani Dar es Salaam Ijumaa wiki hii.

Vikao vingine vitafanyika leo na kesho katika miji ya Mwanza, Arusha na Dodoma.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, alisema kiwango kilichopendekezwa ni asilimia 40 kwa wateja wa majumbani na viwandani.

Kiwango cha umeme kwa wateja kinatozwa Sh. 38 kwa uniti O -50.

Alisema kiwango hicho kimependekezwa kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

``Hata hivyo, TANESCO inajua kwamba ongezeko hilo litaathiri wateja lakini hakuna jinsi ni lazima shirika lijiendeshe kibiashara ili kukidhi mahitaji na malengo yetu,`` alisema.

Alisema TANESCO imewasilisha kwa EWURA ombi la kupandisha viwango hivyo katika kipindi cha mpito kuanzia 2008-2009.

Alionyesha wasiwasi kuwa hata kiwango kipya kilichopendekezwa hakitaikomboa TANESCO na changamoto za uendeshaji na kwamba itandelea kubadilisha viwango mara kwa mara kuendana na hali ya soko.

Dk. Rashid alisema ``Ongezeko hilo litaifanya TANESCO kuweka kiwango madhubuti cha gharama kulingana na gharama za uendeshaji, uboreshaji na utoaji huduma endelevu kwa wateja.``

Aliongeza kuwa viwango vipya vitaliwezesha shirika hilo kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme, kuweka miundombinu na kusambaza umeme pamoja na kutimiza lengo la kukuza na kuongeza uwezo wake.

Akitoa takwimu za viwango, uwezo wa shirika na uwezekano wa kuinua mapato ya TANESCO, Dk. Rashid alisema ripoti ya taarifa za fedha za mwaka jana zilizokaguliwa, zinaonyesha kuwa shirika lilikuwa linaendeshwa kwa hasara ya Sh. bilioni 677.

Alisema mwaka 2006 wastani wa viwango vya kulipia umeme ulikuwa Sh. 84 kwa uniti kwa kilowati kwa saa wakati wastani wa gharama ya uzalishaji ilikuwa Sh. 183 kwa kilowati kwa saa ambao ni hasara ya Sh. 99 kwa shirika lake na hivyo kufanya hasara kubwa iliyofikia Sh. bilioni 183 kunakoletwa na kuzalisha umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa gharama ndogo.

Alifafanua kuwa hadi mwaka jana hasara hiyo iliendelea kuongezeka na kufikia Sh. bilioni 677 kutokana na kuzalisha umeme wa mafuta kulikosababishwa na ukame uliokausha mabwawa makubwa ya maji.

Aliwaambia waandishi kuwa katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu shirika limepata hasara ya Sh. bilioni 58 .

Alisema changamoto za uendeshaji zimesababisha kushindwa, kukopa kwenye mabenki, kuchelewesha kuwalipa wazabuni na kukosekana ruzuku kutoka serikalini.

Aliongeza kuwa ukusanyaji mapato umeendelea kuwa mdogo na kulifanya shirika lishindwe kujiendesha kwa ufanisi na kuwa chini ya viwango vinavyotakiwa kwenye uzalishaji viwandani.

Aliwataka wateja kulipa gharama halisi ili shirika liweze kuboresha huduma zake.

Alisema matatizo yanayolikabili shirika ni utegemezi wa mafuta kuzalisha umeme wa mafuta ambao ni ghali kupindukia, kushindwa kuunganisha wateja wapya, kutoa huduma za chini ya viwango, kutumia miundo mbinu michakavu, uharibifu wa miundo mbinu.

Mapema mwezi huu, TANESCO ilipandisha gharama ya kuunganisha umeme kwa wateja kwa asilimia 200 na kufikia zaidi ya Sh. 500,000.

Aidha ilisitisha kwa muda usiojulikana kuunganisha umeme kwa madai kuwa mteja anayehitaji ni lazima ajinunulie vifaa kama vile mita, vikombe, nyaya, nguzo na kulipia gharama ya ufundi.
 
Kweli mbuzi atakula usawa wa kamba yake!. Walalahoi tulie tu! Tusubiri kupumzika kwa raha kaburini hamna haja ya mwanga wala nini!
 
Tusubiri kupumzika kwa raha kaburini hamna haja ya mwanga wala nini!

Have a quick look on tha attached file below
 
Attachments

  • tanesco-ewura.jpg
    tanesco-ewura.jpg
    19.9 KB · Views: 99
Hivi kwa nini wananchi wabebeshwe mzigo wa uzembe wa wengine.
IPTL, RIchmond, etc etc.
Kwa sababu huo mzigo walio kuwa nao TANESCO ni kutokana na mikataba mobovu na Vile vile Kwenye Kodi zingine, tuna changia changia starehe za wengine.
 
Tanesco yapingwa

2007-11-16 09:00:12
Na Joseph Mwendapole

Baadhi ya wananchi wamepinga mapendekezo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kutaka kupandisha gharama za kuunganisha umeme kwa zaidi ya asilimia 200.

Endapo mapendekezo hayo yatakubaliwa, gharama hizo zitafikia Sh. 563,271, wakati awali ilikuwa Sh. 200,000.

Wakizungumza na Nipashe jana, wananchi hao walisema endapo shirika hilo litapandisha gharama hizo, wengi watashindwa kuzimudu.

Bw. Bakari Kiembe, mkazi wa Mwananyamala alisema kama mapendekezo hayo yatakubalika, nishati hiyo itakuwa kama anasa.

Alisema watu wa kipato cha chini hawatamudu gharama za kuunganishiwa umeme kwa kiasi kilichopendekezwa na shirika hilo.

Alisema uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukipigwa vita na serikali utaibuka kwa kasi kwa kuwa wananchi hawatakuwa na nishati mbadala.

`Mtu anajibana anajenga kajumba kake miaka kumi ndipo anamaliza na akitaka umeme unamwambia atoe Sh. 500,000 atazitoa wapi,` alihoji.

Mkazi mwingine wa Sinza, Bw. Ayubu Mtemi, alisema kupanda kwa gharama hizo ni matokeo ya shirika hilo kutokuwa na mshindani.

Alipendekeza litafutwe shirika lingine litakalokuwa likitoa huduma kama ya Tanesco ili kuondoa ukiritimba.
Bw. Mtemi alisema shirika hilo ni la umma na linapaswa kutoa huduma ambayo haiwaumizi wananchi wake lakini halifanyi hivyo.

Alisema lazima serikali iingilie kati na kutupilia mbali mapendekezo hayo kwa kuwa huduma ya umeme ni ya lazima tofauti na zingine.

`Angalau huduma ya simu unaweza kupandisha gharama kwa kuwa kupiga simu mtu anaweza kujibana, lakini suala la umeme ni lalazima,` alisema.

Aliongeza kuwa endapo mapendekezo hayo yatakubaliwa, mpango wa serikali kuwapatia nishati hiyo watanzania wengi ifikapo mwaka 2010 utakuwa ni ndoto.

Bw. Juma Mulla, wa Manzese alisema ni wakati muafaka kwa serikali kufikiria kuliuza shirika hilo kama ilivyofanya kwa mengine.

Hata hivyo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imekataa mapendekezo ya Tanesco mpaka itakapofanya mijadala na wananchi watoe maoni yao.

Kutokana na kukataliwa kwa ongezeko hilo, Tanesco imeamua kusitisha shughuli za kuwaunganishia umeme wateja wapya, mpaka mazungumzo yake na EWURA yatakapokamilika.

Katika ofisi mbalimbali za shirika hilo jijini Dar es Salaam, matangazo yamebandikwa yakielezea kuwa, huduma hizo zitaanza kutolewa itakapoamuliwa baadaye.

`Malipo mapya na yale ya zamani, yamesitishwa mpaka itakapotangazwa upya baadaye,` lilisema sehemu ya tangazo moja katika ofisi za Mkoa wa Ilala.

Tangazo hilo pia lilisema kuwa, hata fomu za maombi ya mwanzo, hazitatolewa kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limesema wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme watatakiwa kununua vifaa wao wenyewe.

Meneja Uhusiano wa shirika hilo, Bw. Daniel Mshana, alinukuliwa akisema juzi kuwa wakati wakiendelea kujadiliana na EWURA, wateja watakaotaka kuunganishiwa umeme watalazimika kununua vifaa wao wenyewe.

source Nipashe

Yaani hapa hakuna ujanja, gharama za umeme lazima zipand tu kama wanavyotaka TANESCO mengineyo ni siasa. NAdhani wakati umefika Wananchi tukaelezwa chanzo cha TANESCO kutaka kupandisha gharama za umeme; EWURA wanafanya siasa tu hapa na Wanachi tunapiga kelele bure lakini kwa hili hatutafanikiwa vinginevyo serikali irudishe ruzuku kwa TANESCO. TANESCO hivi karibuni imekopa kutoka mabenk shilingi bilioni 300 ili kujiimarisha na waweze kutoa huduma bora sasa wasipopandisha mwisho wake itakuwa nini.

Ni serikali hii hii ndiyo imeifikisha TANESCO hapo ilipo na haiwezi kukwepa hilo- Serikali imeruhusu NET Group Confusions kuihujumu TANESCO kwa miaka 4 kwa manufaa ya vigogo wachache na mafisadi wanaotutawala.

1. Ni Serikali hii hii iliingia mkataba uliopigiwa kelele hata na Benki ya Dunia na IPTL na leo IPTL wazalishe wasizalishe TANESCO inalazimika kulipa mabiloni ya shilingi.

2. Ni serikali hii hii inayokumbatia Mafisadi iliyoingia Mkataba wa mabilioni na Richmond ambayo TANESCO inatakiwa kulipa.

3. Ni serikali hihi inayokumbatia ufisadi wa kiwango cha kufuru ambayo imeilazimisha TANESCO kuingia mkataba na Kampuni ya Mkapa Kiwira Coal Mine kwa manufaa na TANESCO italipa. Not mention Agreko and other deals!

TANESCO wamekuja na wazo la akili sana kuwa anayetaka kuunganishiwa umeme itabidi anunue vifaa mwenyewe nao watatoza gharama za kuunganisha tu EWURA bado wanakataa, sasa TANESCO ita-survive vipi? Vinginevyo tukubali TANESCO ife!

Mimi ninalipa umeme kila mwezi na najua kuwa itaniumiza sana lakini penye ukweli lazima tukubali. NO way TANESCO lazima wapandishe bili tu, tupende tusipende maana si tumekubali kuwakumbatia Mafisadi ambao wameila TANESCO bila kunawa?
 
Back
Top Bottom