Tanesco, Dowans wavutana

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
0
mhando%20tanesco.jpg
Leon Bahati
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema linakusudia kukata rufaa kupinga hukumu inayowataka kuilipa kampuni ya Dowans fidia ya mabilioni ya fedha, lakini likatahadharisha kuwa kuna siri nyingi zilizo kwenye kesi hiyo ambazo ikibidi watalazimika kuziweka hadharani.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja juzi aliitaka Tanesco kutoa maelezo ya kina kuhusu hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Dowans kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), ikitaka ilipwe fidia na shirika hilo baada ya kukatisha mkataba wa kuzalisha umeme mwaka 2008.

Mahakama hiyo iliitia hatiani Tanesco na kuitaka ilipe fidia ya zaidi ya Sh185 bilioni kwa Dowans.
Jana Tanesco ilitangaza nia hiyo ya kukata rufaa huku ikijigamba kuwa iliibuka kidedea kwenye kesi kampuni ya Richmond Development LLC na sasa italipwa dola za Marekani 1.2 milioni sawa na Sh 2.9 bilioni.
Taarifa maalumu iliyotolewa na Tanesco jana iliweka wazi kwamba inasubiri ICC isajili hukumu hiyo kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, ili shirika hilo liweze kutathmini na kuamua hatua nyingine za kuchukua.

“Tanesco imeomba ICC kuandikisha uamuzi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania kama inavyotakiwa kisheria ili kuruhusu Tanesco iweze kuchukua hatua nyingine yoyote katika suala hili, kama ikibidi,” inaeleza taarifa hiyo.
Katika taarifa yake, Tanesco imeeleza kwamba imeamua kuweka hadharani maelezo ya hukumu hiyo licha ya sheria za ICC kutaka iwe siri, baada ya kuona gazeti hili limeripoti kuhusu uamuzi huo katika matoleo yake ya juzi na jana.

“Pamoja na sheria za usuluhishi zinazotaka maelezo ya uamuzi kuwa siri, Tanesco imebidi kutoa hadharani maelezo ya uamuzi kutokana na taarifa ambazo zimetolewa katika vyombo vya habari (Mwananchi pamoja na gazeti dada la The Citizen),” inaeleza sehemu ya taarifa ya Tanesco.
Tanesco inaeleza kuwa baada ya taarifa hizo kumekuwepo na mijadala ambayo inaashiria kupotosha, hivyo ikaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo na huenda baadaye ikazidi kuweka wazi siri nyingine.
“TANESCO ina haki ya kutoa maelezo ya maamuzi kutokana na ulazima wa kulinda maslahi yake. TANESCO bado inapitia uamuzi wa ICC kwa kina na baadaye ikibidi itatoa taarifa zaidi kuhusu suala la maamuzi haya ili kusiwe na upotoshwaji,” inaeleza Tanesco katika taarifa yake.

Tanesco imeeleza kwamba hukumu iliyotolewa Novemba 15 ilihusu mashauri mawili ya kampuni za Richmond Development Company/Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited dhidi ya Tanesco.
Ilifafanua kwamba Richmond walipeleka ombi la usuluhishi ICC Septemba, 2008 na madai yao yalikuwa ni fidia ya dola 169 milioni za Kimarekani, ikiwa ni madai ya kukashifiwa na kusitishwa kwa mkataba wao.
“Shauri hili lilisikilizwa Aprili 2010 huko Dubai. Dowans kwa upande wao waliwasilisha ombi la usuluhishi ICC mwezi Novemba, 2008 wakidai ukiukwaji wa mkataba na kutolipwa gharama zote za uwekezaji wa mitambo. Jumla ya madai ilifikia dola milioni 149. Shauri hilo lilisikilizwa mwezi Juni, 2010 jijini Dar es salaam,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pamoja na kutolewa hukumu hiyo na kutaja fidia ambazo Tanesco inapaswa kuilipa Dowans na hata Richmond kulilipa shirika hilo, bado kiwango halisi hakijafahamika hadi hapo Mahakama Kuu itakapopitia na kutoa tafsiri halisi, inaeleza taarifa hiyo.
Lakini kulingana na maelezo ya hukumu hiyo, Tanesco itailipa Dowans dola 24.2 milioni za Kimarekani (takriban Sh36.3 bilioni) pamoja na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka kulingana na limbikizo la dola milioni 20 milioni, (Sh 30 bilioni) kuanzia Juni 15, 2010.

Pia Tanesco italipa dola 40 milioni (Sh 60 bilioni) za Kimarekani pamoja na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka kulingana na limbikizo la jumla ya dola 36.7 (takriban Sh 55 bilioni) kuanzia Juni 15, 2010.
Gharama nyingine ambazo Tanesco itawajibika kulipa, zinaelezwa kuwa ni za kesi ambazo ni dola 1.7 milioni sawana na Sh 2.6 bilioni.
“Kiasi halisi kitakacholipwa kwa Dowans bado hakijakokotolewa kwa kuzingatia hukumu na pia uamuzi huo bado haujaandikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria,” inaeleza taarifa ya Tanesco.

Pamoja na Dowans kuibana Tanesco kwenye mashauri hayo, shirika hilo la nishati nchini lilifanikiwa kuibwaga Richmond katika dai lake la kutaka lilipwe dola 169 milioni za Kimarekani, ikiwa ni asilimia 50 ya gharama za kisheria na gharama nyinginezo.
Kwa sababu hiyo Richmond imeamriwa na ICC iilipe Tanesco dola 1.2 milioni za Kimarekani (karibu Sh 1.8 bilioni).
Lakini Richmond pia ilifanikiwa kuishinda Tanesco katika dai kwamba iliikashifu, hivyo kutozwa dola za Marekani
50,000 (Sh 75 milioni)

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,528
2,000
Serikali/tanesco wasibadilisha maswala ya kisheria kuwa ya kisiasa. Wanataka ku-apeal kwa watz kwa kumwaga hadhari muenendo wa kesi hii wakati ni uvunjaji wa sheria. Wataitia matatani nchi hii kwani kama walivyoomuliwa kuilipa richmond kwa kuidhalilisha kadhalika watazalisha kesi nyingine na watalipa faini zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom