TANESCO: bili za mwezi huu kiboko jamaa wamefanya maisha kuwa magumu zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO: bili za mwezi huu kiboko jamaa wamefanya maisha kuwa magumu zaidi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by dosama, May 8, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jamani mimi Mtanganyika kazi yenyewe hii ya uwalimu bili imekuja toka 23,000 hadi 39,879/= si tunakoelekea jamani ni kukaa gizani kwa sie tusio kuwa nacho?

  Na naona wanashindana na wa maji maana nayo imetoka 8,467.43 hadi 31,546.32


  Y jamani ????? Kwa nini???? Na matumizi ni yale yale niko bachelor je nikiwa na familia??
   
 2. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Afadhali ya kwako wenzio wametoka 20,000 mpaka laki na ushee!! MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  MKUU JIPANGE
  DAWA YA HAWA WEZI NI kutafuta alternative
  Kuna solar za laki nane ukizifunga hizo
  mbona tanesco utawasahau
  ndio njia pekee
  ya kufanya mkubwa
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Mawazo yangu ndugu yangu kajiendeleze kielimu zaidi kwani maisha yako ya ualimu yatazidi kuwa magumu na mimi sioni sababu ya kulalamika. Hao viongozi hawajali mtu kama wewe hivyo jiangalie mwenyewe na kajiendeleze kielimu utaona maisha yanabadilika. Usijichukulie kama mtu uliyeshidwa!
   
 5. S

  Smarty JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  si upige nyoka tu...
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  haaaa....mimi nilidhani niko peke yangu.......bili yangu imeongezeka elfu 40 na zaidi......
  mbona twafa.......
   
 7. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  kwani walimu ndo wenye maisha magumu tu!!!ajiendeleze kielimu aongeza ujuzi au mshahara!?hata walimu wapo wenye maisha mazuri usishushe taaluma kiasi hicho mkuu!
   
 8. mean girl

  mean girl Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kaka unachanganya kati ya elimu na mfumuko wa bei nchini,kuwa na elimu au kutokuwa nayo haipi serikali chhance ya kupandisha huduma bila ya kuzingatia maisha ya jumla ya wananchi wake wote,nani alisema ukiwa na elimu kubwa ndo maisha yatakuwa mazuri? Ajira zenyewe ukiomba ukiwa na elimu kubwa unaambiwa YOU ARE OVERQULIFIED.
   
 9. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu unatumia LUKU au zile mita za kukadiria? Kama ni zile za kukadiria wakati mwingine huwa wanakosea. Kuna dada mmoja waliwahi kumpelekea bili ya laki tatu ndani ya mwezi mmoja utafikiri ana kiwanda nyumbani kwake. Maji nayo je? Una mita? Au nazo ni zile wanakukadiria tu mwisho wa mwezi?. Kama una mita ni rahisi kufahamu tatizo liko kwako au wamekubambika. Mimi watu wa maji wamewahi kuniletea bili ya laki tatu na 30 elfu kwa mwezi mmoja kisa aliyesoma mita alipeleka data za uongo ofisini kwao. Nimehangaishana nao mpaka kwa wakubwa wao wameirekebisha sasa. Kwa kifupi umeme na maji wamepandisha sana gharama zao.
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Gesi nayo imepanda toka elfu 52 hadi elfu 60
   
 11. B

  Baby shangazi Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sio peke yako, yaan sisi wameleta 35,900 kutoka 15,000 wakati matumizi ni yale yale, ipo siku tutawafundisha adabu.
   
 12. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi nilipopanga LUKU imekua ishu mpaka tunahisi kuna mtu anatumia jiko la umeme kumba mambo yenyewe ndio imekua kila mahali jamani twafwa
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  bora malipo hayo yangekuwa yakiendana na huduma nzuri,lakini wapi umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni na bado unaletea bill ya 20,000/= sasa hebu fikilia je umeme ungekuwa unawaka kuanzia asubuhi ungelipa kiasi gani?
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kuhusu umeme karibuni ktk chama changu cha watumiaji wa SOLAR


   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  achaneni na mita za zamani, wataishia kuwaba,bikia bill, tumieni luku
   
Loading...