Tanesco bado ni jipu

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,288
1,500
Tatizo la umeme bado ni nchini, mfano Dar es salaaam ukatwaji wa umeme ni mkubwa kwamba shughuli za uzalishaji mali zinasimama.

Sasa ni zaidi ya miezi miwilu ukataji umeme asubuhi, mchana na jioni imekuwa kawaida. Tanesco hawasemi ili watu wafikiri kuwa tatizo la umeme nchini hamna.

Prof. Muhongo nae kakaa kimya.

Hivi kweli Tanzania ya viwanda bila umeme itawezekana wapi? Kwani hii sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na wananchi haipewi kipaumbele. Kelele za kupeleka umeme vijijini hazima maana kama watumiaji wakubwa na muhimu wa umeme hawaupati na wahusika wanafanya mambo kisiasa.

Nilitegemea Menejimenti yote ya Tanesco ingevunjwa na kusukwa upya na watu nje ya Tanesco ambao wangekuwa na mawazo mapya na mtazamo mpya. Maana kuwapa ukurugenzi na Mkurugenzi mkuu wale waliokaa Tanesco miaka mingi ndiyo hao hao kina mramba, mhando etc.

I am very disappointed with Tanesco
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom