TANESCO Arusha tangazeni kama kuna mgao wa umeme

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,352
9,810
Karibia miezi 6 sasa Tanesco Arusha wamekuwa wakikata umeme kila siku. Imefikia mahali sasa suala la kukatika umeme limekuwa la kawaida, yan wanaturudisha nyuma kipindi kile cha Lowassa ambapo kila kona ilikuwa giza.

Mi ninachoomba kama kuna mgao tangazeni rasmi, kuliko kutukatia umeme kila siku. Magufuli alipoingia madarakani alijitapa kuwa mgao wa umeme sasa itakuwa historia, lakini kinachoendelea inaonyesha hamna kitu. Ni maneno ya wanasiasa tu, giza linatamalaki kila siku!!
 
hata,huku umeme hakuna ni UKWELI KUNA MGAO jamaa yangu wa,TANESCO kaniambia ila inavyoonesha AWAMU HII KUKILI MATATIZO NI MWIKO leo nimeona CLIP ya PHILIP MPANGO akikohoa kwenye media akiprove yeye yupo GADO na CORONA hamna nimesikitika sana.Sijui na nyie mmeiona?
 
Arusha pande zipi mkuu?

Mi niko sinoni ukikata Mara chache Sana ndaa ya dakika chache unarudi
 
Karibia miezi 6 sasa Tanesco Arusha wamekuwa wakikata umeme kila siku. Imefikia mahali sasa suala la kukatika umeme limekuwa la kawaida, yan wanaturudisha nyuma kipindi kile cha Lowassa ambapo kila kona ilikuwa giza.

Mi ninachoomba kama kuna mgao tangazeni rasmi, kuliko kutukatia umeme kila siku. Magufuli alipoingia madarakani alijitapa kuwa mgao wa umeme sasa itakuwa historia, lakini kinachoendelea inaonyesha hamna kitu. Ni maneno ya wanasiasa tu, giza linatamalaki kila siku!!
Tafadhali onyesha eneo na namba ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi
 
Tuma hata inbox tafadhali
Ya nini? Kwani simu yangu ndo inatumia umeme ama? Jambo la msingi tumechoka kukatiwa umeme ovyo. Na ajabu ni kwamba vyanzo vya umeme vinatumia maji kuzalisha umeme, na mvua zinanyesha kila mahali..
 
Aisee na hapa Dumila, Dakawa, hadi maghubike hali ni hivyo hivyo, mnakata sana umeme na unakaa siku 2 umeme haujarudi, sijui shida nini kila siku mnakata umeme, yaani utafikiri mtu amekaa kwenyw switch yeye ni kuzima na kuwasha, watu hawafanyi kazi bila umeme siku mkija huku mnaweza kupigwa mawe na wanaomiliki mashine za mpunga
Tafadhali onyesha eneo na namba ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi
 
Back
Top Bottom