TANESCO Arusha na mgao wa visasi vya Kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO Arusha na mgao wa visasi vya Kisiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVUMBUZI, May 2, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kuna habari za kuaminika kutoka ndani ya TANESCO Arusha kuwa mgao ulioanza tangu tarehe 1/11/2010 hadi leo maeneo ya Kimandolu ni visasi vya kisiasa vya kuwakomoa wananchi wa maeneo hayo kwa kumpa kura chache JK ktk uchaguzi uliopita. Maeneo ya Kimandolu ndiko alikotoka diwani wa CHADEMA Mh. Estomihi Malla aliyetakiwa awe Meya wa Arusha na badala yake kudhulumiwa na Gaudence Lyimo wa CCM.
  Kitendo hiki kichafu cha TANESCO Arusha cha kuwaadhibu wakazi wa Kimandolu na vitongoji vyake kimedhihirika baada ya utafiti uliofanywa na kugundua kwamba wakati hakuna mgao wa umeme maeneo mengine ya Arusha, Kimandolu imekuwa kwenye mgao mkali wa siku 5 kwa wilki mfululizo tangu baada ya matokeo ya uchaguzi ya ubunge na madiwani kutangazwa hadi leo isipokuwa wiki ya pasaka tu.

  Leo tena TANESCO Arusha wameanza tena mgao wao wa chuki kwa wananchi wa Kimandolu wakati maeneo mengine ya hapa Arusha mjini yakiwa na umeme kama kawaida .

  Wananchi wa kimandolu wameanza kuitisha vikao ili wajipange waingie kwa maandamano makubwa TANESCO Arusha kumtaka meneja atoe maelezo kwa nini anawatesa watu wa Kimandolu.

  Wananchi wa kimandolu mgao wao ni mkali kuliko mgao wowote ule wa umeme uliowahi tokea nchini kwani huanzia jumatatu kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 usiku na jumanne saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni , Jtano saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, Alhamis saa 2 asubuhi hadi 12 jioni, ijmaa saa 12 jioni hadi saa 4 usiku. Vivyo hivyo na jumamosi isipokuwa baadhi ya siku za jumapili ndo hamna mgao.

  Watu wanashawishika kwamba habari hizi ni za kweli kwa sababu wanaamini mabwawa mengi yamejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mikoa ya Morogoro- Kilombero na Iringa pamoja na Tanga. Mikoa hii ndiko kuliko mabwawa makubwa yanayozalisha umeme mwingi unaotumiwa katika mikoa yetu. Kama tunapata umeme nyumba ya mungu mbona kilimanjaro na vitongi vyake hakuna mgao. Wahusika tunawataka watoe majibu haraka kwani wananchi wa Kimandolu wamechoka na wanataka kutumia uhuru wao kupata maelezo uso kwa uso kutoka meneja wa TANESCO Arusha.
   
 2. N

  Ndingonyi New Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanesco Arusha wizi wa pesa za wannchi macha juwa kali linawaka hata aibu hawan kuzungusha wannchi kutewa nzima, kuwalipisha zaidi ya viwango vyao, kukata umeme kwa chuki na kuwalipicha mamilioni, muulizeni mhasibu wenu Tanesco Arusha amekusanya mamilioni mangapi kuanzia mwaka jana mpka mwaka huu, hakuna umeme lakini unakwenda kukata mita za watu na kuwalipisha bila sababu. Aibu kwani hata mahesabu yanu hayendani na baruwa zenu kwa wananchi. Mtakata umeme lakini maendeleo ya Arusha ni maendelea ya taifa, kwa hivyo mnaangamiza Taifa lenu wenyewe. Hilo ni shirika la umma na siyo la mtu binafsi. Mkome kabisa kuibia wananchi wezi na mafisadi wanaoiba mchana. Huko Tanesco kuna viongozi wamejipanga na tai zao utafikiria wanchapa kazi kumbe wantafuta jinis gani ya kula pesa za walal hoi. Fanyeni kazi nyie mafisadi wa Tanesco hamkuja huko kuvaa tai na kuendeleza vitambi, amkeni huko makao makuu mkasikilize hoja za wananchi huko Arusha.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Hawa wasipojirekebisha siku si nyingi Meneja ataanza kuona ofisi kama kituo cha Polisi. madhara ya kuchanganya professional na siasa na hatimaye kuanza kutumia huduma za jamii kama fimbo ya kuwachapa mnaotofautiana kisiasa
   
Loading...