TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Wengi tukisikia solar energy tunajawa na hisia kwamba ni jambo la maana sana! Ni umeme mzuri kwa mwanakijiji anayetaka mwanga wa kufukuza wanyama watembeao gizani tu! Kwani nchi zetu hizi maskini hatuhitaji miradi mikubwa kiasi hicho kinacholengwa na Tanesco.

Ni uharibifu wa pesa kwa kujidai kuingia kwenye renewable energy. Ni biashara ya makampuni ya kigeni kujipenyeza ndani ya TANESCO, nao wanaandika eti by 2050 Tanzania itatumia renewable energy, wakimaanisha wind na solar. Huu naweza kuita ni upuuzi.

Solar na wind bado ni luxurious energy sources ambazo tunawaachia nchi zilizoendelea kufanya majaribio. Ni aibu kwa shirika kama Tanesco kujiingiza kwenye miradi ya gharama kubwa kiasi hicho. Maneno kama renewable energy na alternative energy ni kujiridhisha tu na kuwazubaisha wanasiasa na kunufaisha makampuni ya nje ambayo yanatuuzia hizo pannels.

Katika East Africa walianza Uganda. Kwa mikogo wakatangaza kuwa na solar farm, ukweli ni kwamba hilo ni shimo la fedha. Wangeweza kupata umeme mwingi kutoka Nile kuliko hizo pannels. Sasa wameingia Tanesco nao kwa mikogo wanatangaza tender ya kufunga mitambo ya solar. Spain Andalusia inajigamba kuwa na solar farm ya kisasa kabisa na technolojia za kisasa lakini bado ni umwamba tu, wana umeme mwingi kwa njia za nuklia na mafuta.

Je, kwa nini Tanesco inajiingiza kwenye solar? Jibu ni rahisi: Kwanza hawaijui kiuhakika kiasi hicho zaidi ya kusimuliwa na makampuni yanayouza pannel na kutoa mifano ya nchi jirani na ulaya ambako hakuna nchi hata moja ilnayotegemea solar. Mfano mzuri ni ujerumani ambako Angela Merkel aliahidi kuondoa mitambo yote ya nuklia ili kuweka renewable kama hizi wanazokimbilia Tanesco. Tangu 2005 hadi leo hajafika kokote! Kumbuka huyu ni mfizikia, syansi anaijua sana. UK wao waliongeza nuklia na ikajengwa na kampuni ya China. Hivi karuibuni Afrika kusini imejenga nyuklia mpya na ni mitambo itakayokuwa mikubwa kuliko yote duniani.

Pili Tanesco kuna tamaa ya kupewa kitu kidogo na makampuni ya nje ili kubeba techolojia ya aina hii ambayo kwa tender kama hiyo, lazima itajengwa na makampuni ya nje.

Bila kujali 2050 nani atakuwa hai, Munachokifanya ni wizi mtupu na hasara kwa kizazi kijacho. Kama mna ubavu jengeni mitambo ya nyuklia.
 
Hii ndo nimesema dk chache zilizopita! Lini nchi isiyo na umeme, third world ikategemea solar na wind? Wahuni tu hawa. Hili ni kama la watu wa fire na drones za kuzimia moto!

Wakati wa Muhongo tulielezwa mipango ya nyuklia, wameiacha sasa wako Solar?

Mradi wa Mwakyembe na wind za Singida uko wapi vile!

Tanesco acheni usanii!
 
Tanzania hatuwezi kamwe kuwekeza kwenye renewable energy kwa ajili ya power supply. Hizo zibaki kwenye gesi tu na si zaidi ya hapo. Nani ataweza kugharamia kununua mitambo ya umeme wa upepo na gharama zake kubwa sana za kuiendesha. Nani atagharamia umeme wa solar.

Wasitake kujitutumua na kuiga wasiyoweza. Vyanzo tulivyonavyo viendelezwe wala hakuna haja ya kubeba majukumu mazito ambayo hata hivo hawawezi kwa vichwa walivyonavyo.
 
Solar ni umeme Bora na rahisi sana kuliko unavyopotosha! Nimetumia solar hapa Gezaulole Kigamboni Dar es salaam miaka 6 sikuona Wala kupata shida ya aina yeyote. Tofauti yake uwekezaji wake unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika
 
Wakati mwingine ni uungwana kukubali kuwa wewe ni mjinga na pengine mpumbavu inapotokea kitu unachofahamu kuhusu jambo fulani ni matokeo ya ujinga ulio nao.

Suala la nishati kwa maisha ya binadamu wa leo ni nyeti sana, hasa kwa vile aina nyingi za nishati zina madhara ya kimazingira kupelekea kuathiri uhai wa viumbe hai akiwemo binadamu na hivyo nishati yoyote ambayo inaleta madhara iwe ni ya muda mfupi au mrefu ni vyema kutathimini vizuri namna ya kuitumia.

Mengine yanayohusiana na vyanzo vya nishati ni pamoja na kujua kama nishati hiyo ni endelevu, gharama zake nk. Ukiorodhesha aina zote za vyanzovya nishati vilivyopo..jua, upepo, maji, mafuta, madini (gesi , uranium,coal nk), joto ardhi na vingine jibu unalopata kuhusu nishati gani inakidhi changamoto za kimazingira na uendelevu jibu ni jua, upepo pengine na joto ardhi..gharama haiwezi kuwa kigezo cha kudrive maamuzi unapochagua aina ya nishati.


Baada ya kufahamu hayo kinachotokea kwenye maisha yetu tunapochagua aina ya nishati tulizo nazo ni kuwa na mchanganyiko wa kutumia nishati zote...ili hata kama nchi yetu inayo nishati fulani kwa wingi, let say maji..ni muhimu pia kutumia nishati ya jua na upepo japo kwa asilimia kidogo ili kuwa na mbadala wa nishati inayotokana na maji ili kuchangia kupunguza athari za kimazingira na kuwa na uendelevu, kama nishati moja ikipata changamoto, maji yana matumizi mengi, lakini maji yanategemea mvua, mvua zinaweza kupungua na hivyo maji kupungua pia, kama huna chanzo kingine utaathirika sana.

Ni muhimu na lazima kuwa na MIX ya vyanzo vyote...na hicho ndicho wanafanya TANESCO!
Kwanza wamechelewa sana, ilitakiwa tuwe na megawat zaidi ya 300 zinazotokana na jua na upepo kwenye gridi yetu, hizi sio luxurious energy..ni reliable energy!
 
Tanzania hatuwezi kamwe kuwekeza kwenye renewable energy kwa ajili ya power supply. Hizo zibaki kwenye gesi tu na si zaidi ya hapo. Nani ataweza kugharamia kununua mitambo ya umeme wa upepo na gharama zake kubwa sana za kuiendesha. Nani atagharamia umeme wa solar.

Wasitake kujitutumua na kuiga wasiyoweza. Vyanzo tulivyonavyo viendelezwe wala hakuna haja ya kubeba majukumu mazito ambayo hata hivo hawawezi kwa vichwa walivyonavyo.
Unaposema renewable energy ina gharama kuendesha unamaanisha nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco ndio pori kubwa la ufisadi hapa nchini. Miradi mingi inayoanzishwa huwa haina lengo la kusaidia kuimarisha shirika bali ni kichaka kinachotumiwa na vigogo kujipigia pesa.

Kwa mtazamo wangu njia rahisi ya kumaliza tatizo la umeme hapa nchini ni kuruhusu makampuni mengine yaje kuleta ushindani kwa tanesco, kama vile Tigo, Vodacom, Airtel walivyokuja kuleta ushindani kwa Ttcl na kusaidia kuondoa kama sio kumaliza kabisa tatizo la mawasiliano ya simu hapa nchini.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom