Elections 2010 Tandika kwazizima kwa vurugu!!!

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
482
176
Nasikiliza redio one hapa ofisini wanarusha vurugu zinazotokea hopo temeke

aliye karibu atuhabarishe
 
Alisema Kikwete................Ushindi lazima. Na kwamba damu itamwagika. Alikuwa anajua fika kwamba watachakachua na wapinzania/wanamageuzi hawatakubali upuuzi wao.

What a shame, wataweka wapi nyuso zao?
 
Check ITV police jamani kuweni na huruma ya nini kupiga watoto wadogo? IGP Mwema hii ndio police ya jamii? very disappointed
 
Tandika haikaliki,vijana wanachoma matairi,mitaa imefungwa hali ni tete... Watu wamechoka

WITO WANGU:Matokeo yatangazwe mapema jamani...
SOURCE:ITV
 
Slaa alisema fujo zitaanzishwa na CCM. Sasa tunaona jinsi CCM wanavyochelewesha matokeo ili kuwakasilisha wananchi. Matokeo mengi yaliochakachuliwa yatatangazwa usiku wakati watu wengi wakiwa majumbani halafu kesho polisi watakuwa kila kona!!
 
Kazi ipo, matumaini tuliyokuwa nayo yanaanza kufifia, CCM wanajeuza matokeo
 
Hivi hawa jamaa, haya mambo mpaka lini?

Yaani hata wawakilishi bungeni wanataka kutuchagulia!!! Huu ndo utawala wa haki, kweli JK!!:doh:
 
Wananchi na wafuasi wavyama vya upinzani wamefunga mitaa na wameanza vurugu matairi yanachomwa vurugu zimezidi kuwakubwa na polisi nasikia wanajipanga!
 
tudai haki lakini si kwa vita. style hiyo haijawahi kusaidia popote duniani, kama ilitokea ni kwa kiasi kidogo sana:yield:
 
Monday, 01 November 2010 15:47

Dar es Salaam. JIJINI Dar es Salaam polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya wananchi waliokuwa wakifanya maandamano ya kupinga matokeo ya udiwani kata ya Tandika.

Vurugu za aina hiyo pia ziliripotiwa mkoani Kigoma ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika ofisi za halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge.


Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea wawili ambao ni Ally Mleh wa Chadema na Peter Selukamba wa CCM.


Vurugu za Tandika zilitokea majira ya alasiri, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya wagombea wa nafasi za Udiwani wa kata ya Tandika ambapo kwa taarifa za awali kutoka kwa msaidizi wa kituo mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Zena Mgaya ameibuka mshindi dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Bakari Mbegu ambaye ndiye waliokuwa wakichuana vikali.
 
rafiki zako CCM wanachakachua

Kings kura ni siri ya mtu mimi sina chama na siwezi kusema nilimpigia nani ila jua napenda mageuzi na huwa sipendi kebehi esp za kidini ambazo wengi wetu humu ndani wanazo. Namshukuru Mungu nina akili najua lipi zuri kwangu na lipi baya sijambeza mtu hata siku moja ila nasimamia ukweli. hakuna asiejua kuwa ni vigumu sana kushinda kwa mazingira tuliyonayo haina maana kusema hivyo wewe ni ccm huo ni ukweli kama huamini nenda zanzibar watakufumbua macho.
 
Mother kanipigia nae amepigwa hayo mabomu wakati anaenda kwa ofisi pride Tandika
 
Back
Top Bottom