Tandale si mchezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tandale si mchezo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee wa Kale, Mar 19, 2010.

 1. M

  Mzee wa Kale Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima kwenu,

  Nilifika Tandale Sokoni majira ya saa 11, jioni nikiwa na ndugu zangu niliotoka nao Zanzibar, ambapo kesho yake alfajiri walitakiwa kuondoka kwenda nje ya nchi, sasa tulikwenda huko kwa ajili ya kununua angalau vijizawadi kidogo, tulifika pale tukiwa na Tax driver ambaye tulimchukua kutoka maeneyo ya Kwa Mtogole, baada ya kukamilisha kununua nafaka na kupakia kwenye Tax, na kuanza safari ya kurudi hotelini mambo yakaanza, alikuja jamaa mmoja akavamila gari kwa ghafla akadai gari yetu imemkanyagia embe zake, hatukuona embe zilizokanyangwa, akamvamia driver wetu akampora simu, baada ya muda kidogo kundi kubwa la vijana likaja kuzunguka gari ambapo sisi tukiwa ndani wakitaka tutoke ili kumsaidia driver wetu, mimi nikawauliza kama ni msaada kwa nini nyinyi ambao ndio mko wengi msimsaidie, nikawaambia ndugu zangu fungeni vioo wekeni lock inawezekana sisi ndio wametulenga huyo driver ni mchezo tu a kuigiza, kwa kweli hapo tukapona na tukaondoka salama.

  Natafakari sipati jibu maisha ya vijana wetu utu kwao haupo, wakimwona mtu na vijisenti wako tayari kumtoa roho ili mradi siku ipite, Wana JF tunawezaje kuwasaidia vijana hawa ili kupunguza tatizo linaloikabili nchi yetu kwa wakati wa sasa na ujao?
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,311
  Trophy Points: 280
  Shhhhhhh! Umetuongopea wewe Nchi yenye amani na utulivu mambo kama haya si rahisi kutokea.....:) (Mkuu hiyo ni joke...... pole kwa sekeseke lililokukumba... unajua watawala wetu siku zote wanafikiria mwisho wa pua yao.... mpaka sasa hawajabaini Tz inakoelekea...)
   
 3. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njia pekee ya kuokoa vijana wetu ni kuongeza ajira tanzania. JK yuko busy kuwaentertain mafisadi so hii ya kuongeza ajiri ni ndoto kwa sasa... ndio tz yetu etiiii
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa kuamua kuwa taifa la wachuuzi, things willget even worse mzee. Kungekuwa na system nzuri ya kuwaweka watu kwenye shughuli za uzalishaji, matatizo mengi sana yangeepukika.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tusubiri kilimo kwanza
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  halafu ukitaka kuuza nje bidha zako mpaka uombe kibali, lakini wewe ukilalamika ukali wa bei zao iwe shule, kodi, nk utaambia mguvu ya soko, ebo mleta mafuta unataka apate hasara? lakini wewe ukipata hasara ulijitakia au ulipenda au ujinga wako.
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Pole sana mkuu, hiyo ndo tandale ambayo haina utawala. hatuna serikali kwa kweli ndo maana hata walinzi wa raia yaani polisi washagundua mapema kwamba ukijidai unakomaa na haki mwisho wa siku hakuna anayeku appreciate na unakufa maskini so na wao wizi km huo ni mtaji kwao, ukitoa taarifa kwao watataka kujua umeibiwa nini au km ni pesa shs ngapi? wakishajua jioni wanawafwata wale wezi wanaenda kusanya mgao wao, polisi wanawajua vibaka na wezi wote, hiyo ndo bongo zaidi ya uijuavyo ndugu yangu
   
Loading...