Tancut Almasi - Mama

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Nimekutana na huu wimbo umenikumbusha mbali sana, wote wenye mapenzi na mama zao sikilizeni huu wimbo. sauti nzuri za Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga wa Tancut Almasi wimbo Mama, pata burudani.....kwa hisani ya wanamuziki wa Tanzania, hongera Mzee Kitine.
 
tancut bwana wana nyimbo yao inasema...
Nakwenda safari
Safari yenyewe Safari ngumu sana
Najuwaaaa kama utabaki yatasemwa mengi ndio wabaya wetu mamaaa watafurahi...
 
tancut bwana wana nyimbo yao inasema...
Nakwenda safari
Safari yenyewe Safari ngumu sana
Najuwaaaa kama utabaki yatasemwa mengi ndio wabaya wetu mamaaa watafurahi...

Tatizo maandishi hayatoi sauti, vijana watauchukulia juu juu wimbo huu, aah, acha nirudie tena.....

"Najuwaaaa kama utabaki yatasemwa mengi ndio wabaya wetu mamaaa watafurahi.................................."

Thanks GC.
 
Wimbo mwingine kwa akina mama ni wa JUWATA "Mwana mkiwa"........... Sauti ya TX Moshi na Gurumo

"Ni asubuhi kumekucha maama, mama njaa inaniumaeee............, wakati wa uhai wa baba yako we mwana maisha yalikuwa ni mazuri sana........... iiiiiiiiiiiiii nyamazaeeee, iiiiiiiiii nyamazaeeeeeeeeeeee........... zidisha juhudi kwenye masomo na mafanikio utayaona baadaye................"
 
3D,

Hiyo kitu ilikuwa imetulia sana, "mama hajanza kusema ananza kulia ihiiii...."

Hahahaha sijawai kuja upande huu hata siku mmoja, lakini sitojilaumu kutembelea pande hizi. Good staff buddies.
 
Tancut wana nyingine inasema:
Ilisemwa hapa Duniani
Urafiki wajenga undugu
Lakini urafiki wakoo
Waonekana wakati wa raha
Wakati wa shida huonekani
Kwa hiyo wewe, sio rafiki, ila ni adui yangu...

Hawa jamaa nao walikuwa watamu aisee
 
Mkuu,

Huu wimbo nilishaomba siku kibao kama kuna mwenyewe. Asante sana tena sana sana sana.

Asanteni wenye Blog kwa kuuweka na mbarikiwe.

Nikifanikiwa kununua CD au Cassete yao, bomba sana sana.
Nimekutana na huu wimbo umenikumbusha mbali sana, wote wenye mapenzi na mama zao sikilizeni huu wimbo. sauti nzuri za Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga wa Tancut Almasi wimbo Mama, pata burudani.....kwa hisani ya wanamuziki wa Tanzania, hongera Mzee Kitine.
 
Mkuu,

Huu wimbo nilishaomba siku kibao kama kuna mwenyewe. Asante sana tena sana sana sana.

Asanteni wenye Blog kwa kuuweka na mbarikiwe.

Nikifanikiwa kununua CD au Cassete yao, bomba sana sana.

Sikonge, nimekutumia kwenye mail yako mp3 ya huo wimbo umeupata?
 
Samahani Mkuu. Nilifikiri nimekujibu kwenye email. Labda ilikuwa ni furaha?

Nimeusikiliza na NASHUKURU SANA KWA WIMBO.

Ila huo siyo ule ORIGINAL maana kuna kitofauti kidogo sana.

Ukiipata Original ni poa zaidi maana huko kuna zile nyingine za NAKULILIA AFRICA na "...... usinisogelee, wewe ni mke wa mtu....." Nashindwa kuelewa kama ukienda RTD unaweza kununua. Itabidi nikiingizana Dar basi niende mwenyewe pale RTD. Tatizo ni kuwa huku shamba nikiwaomba watu wa Dar wanitafutie, wao wanasema "hizo Old school sisi hatusikilize tena...."
Sikonge, nimekutumia kwenye mail yako mp3 ya huo wimbo umeupata?
 
Thanks umenikumbusha mbali sana kwa mara ya kwanza na ya mwisho hawa mapacha wa tancut niliwaona dodoma mwaka 1989 sijui wapo wapi sasa
 
Thanks umenikumbusha mbali sana kwa mara ya kwanza na ya mwisho hawa mapacha wa tancut niliwaona dodoma mwaka 1989 sijui wapo wapi sasa

Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, mmoja alifariki na mwingine bado ni mwanamuziki, miaka ya karibuni alikuwa Kalunde Band.
 
Mkuu nakupa 5!!

Tancut Almas, inanikumbusha mwaka 1990 wakati ule ndo namaliza SIX pale TOSA, basi tulialikwa na IRINGA GIRLS kwenda kwenye Muziki wa TANCUT ALMAS waliokuwa wakipiga pale IRINGA GIRLS nasi ilikuwa kali ya mwaka tuliserebuka ile mbaya.

Nakumbuka walikuwa wana raise funds kwaajili ya kujenga madarasa ya FIVE na SIX pale shuleni kwao. Basi ilikuwa ni balaa kwani KASALOO KIANGA na nduguye KIANGA SONGA walikuwa ni kivutio bab-kubwa.

Kwakweli umenikumbusha mbaalii kweli kweli (iRINGA GIRL'S vs TOSA).
 
Mtindo wao maarufu wakati ule ulikuwa ni " Kinye Kinye Kisonzo......tisa kumi Mangalaaaa!!!!"
 
Kinye kinye kisonzo tisa kumi Mangala nilikuwa mpenzi sana wa hii bendi mpaka kaka yangu akawa ananiita kisonzo
 
.. Utawaona kweli mtu na mke wake wakitembea kama baba na mwana. baadhi ya maneno kwenye wimbo wao mmoja hivi wakiponda ma sugar D
 
tancut bwana wana nyimbo yao inasema...
Nakwenda safari
Safari yenyewe Safari ngumu sana
Najuwaaaa kama utabaki yatasemwa mengi ndio wabaya wetu mamaaa watafurahi...
.. nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetuuuu, chunga watoto mama nitarudi, nitarejea kwa mapenzi ya Mungu....
.. nikirudi mama nitakuletea zawadi ooo, iyelee eee mama iyelee ooh..
good memories those days
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom