TANCIS ifanyiwe marekebisho ikusanye kodi za ndani

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,062
2,288
Kwa Kamishna Mkuu TRA,


Ili kutekeleza azma ya Rais kuhusu ukusanyaji wa mapato, naomba kutoa mchango wangu na mapendekezo kama ifuatavyo:-


1. Ukusanyanji wa kodi za ndani ni wa kizamani mno, kila ukienda kwenye meza ya ofisa wa TRA kodi za ndani utakuta rundo la mafaili ya wateja. Baadhi ya wateja wenye makampuni yenye zaidi ya miaka kumi, mafaili yao hayabebeki. Bado idara ya kodi za ndani inatumia mfumo wa kizamani wa kujaza fomu kwa mkono na kuziwasilisha kwa maofisa wanaohusika ili wafanye makadirio. Hii inasababisah wananchi kurundikana kwenye maofisi ya kodi za ndani kusubiri kukadiriwa kodi. Mfano ni ofisi za Kinondoni na Shauri Moyo.


2. Hali hii inaweza kubadilika ikiwa itafanyia marekebisho mfumo wa TANCIS ili utumike kukadiria na kukusanya kodi za ndani kama unavyotumika kukadiria na kukusanya kodi za Forodha. Kwa kodi za ndani mnaweza kuupa jina lingine.


3. TANCIS ikirekebishwa ili ilingane na mfumo wa ukusanyaji wa kodi za ndani ulivyo itakuwa na fomu zote zinazotumika kukadiria kodi za ndani, itakuwa pamoja na mambo mengine kama faini kwa kuchelewesha kupeleka makadirio, interests kwa kuchelewa kulipa na kadhalika.


4. Wasajiliwe tax consultants, wahasibu, wanasheria na watu wengine watakaokidhi viwango ambao watakuwa na uwezo wa kuingia kwenye TANCIS ya kodi za ndani. Hii ina maana kuwa sio kila mfanyabishara anayetaka kulipa kodi atakuwa na mamlaka ya kuingia kwenye TANCIS. Baada ya usajili watapewa password ambayo watakuwa wanaingilia. Kwa maana hiyo badala ya walipakodi kwenda ofisi za TRA kukadiriwa kodi wataenda kwa waliopewa password za kuingia kwenye TANCIS. Hii itasaidia kufanya walipa kodi wasipate usumbufu wa kusafiri kutafuta ofisi ya TRA ili kulipa kodi za ndani.


a. Kwa mfano fomu ya makadirio ya mwaka ikijazwa na mtu aliyeidhinishwa kwenye mfumo huu, mlipa kodi palepale ataenda kulipa kodi yake aliyojikadiria, chini yake zitaambatanishwa hati mbalimbambali zinazotakiwa kulingana na mahitaji ya kodi inayotakiwa kulipwa. Kwa mtandao ataiwasilisha TRA. Ofisa wa kodi za ndani atakachokifanya ofisini kwake ni kuipitia na kufanya makadirio kulingana na taratibu (kama inavyotakiwa kisheria) kama makadirio yakuwa zaidi ya yale yaliyofanywa na mlipa kodi basi atalipa kodi ya ziada kulinganana mfumo ulivyoelekeza. Objections zitashughulikiwa kulingana na sharia ndani ya mfumo huo huo bila mlipa kodi kulazimika kufika TRA labda aitwe kwa mahojiano.

Kama mtu yuko Chanika, Dar es Salaam halazimiki kwenda ofisi za Shaurimoyo au kwa sasa TAZARA. Mhasibu anaweza kuwa kulekule Chanika akaingiza taarifa ya makadirio ya kodi anayotaka kulipa, yakipitishwa atalipa na kupata hati ka kulipa kodi (Tax Clearence itolewe kama Relase Order invyotolewa kwenye mfumo wa Forodha)


b. TANCIS ikitumika itaongeza ajira, hivyo kutimiza lengo la serikali la kuongeza ajira.



5. Internal management ya TANCIS hii itakuwa kama ilivyo kwa TANCIS ya idara ya Forodha ila hapa assessment zielekezwe kwenye ofisi za eneo linalohusika badala ya kuelekezwa Dar es Salaam kama ilivyo kwa Forodha. Hii ni kutokana na maeneo mbalimbali kuwa na tofauti ya vipato, hivyo maofisa waliopo ofisi za maeneo hayo wanakuwa wana nafasi ya kujua uhalisia wa ukadiriaji wa kodi.


6. Faida ya mfumo huu ninaoupendekeza itakuwa ni

a. kutorundika mafaili mengi ofisisni (mtaweka utaratibu wa kuleta hard copies).

b. Maofisa wa TRA kodi za ndani watakuwa wakaguzi zaidi.

c. Mawasiliano kati ya maofisa wa TRA na walipakodi yatapungua hivyo kupunguza mianya ya rushwa na kukwepa kodi.
 
Back
Top Bottom