TANAPA yatangaza Utalii katika Mji wa Seattles | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANAPA yatangaza Utalii katika Mji wa Seattles

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambugani, Jul 21, 2012.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), limeanza mkakati wa kupanua wigo wa kutangaza utalii katika hifadhi zake, ambapo limezindua kampeni maalum ya kutangaza vivutio hivyo katika mji wa Seattle, nchini Marekani.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Tanapa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameshiriki katika kampeni hiyo yenye lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini katika kipindi kifupi kijacho.

  Kampeni hiyo ilizinduliwa jana katika mji wa Seattle kwa matangazo yanayotangaza vivutio vya utalii nchini katika mechi ya Mabingwa wa Ulaya, Chelsea na Seattle FC.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Balozi Kahasheki alieleza kuwa Tanzania imekuwa ikitumia mpira wa miguu kwa ajili ya kutangaza vivutio vyake katika maeneo mbalimbali, lakini safari hii imegeukia soko la mji wa Seattle ambao una wapenzi wengi wa soka ambao kutokana na matangazo hayo ya utalii wanaweza kuvutiwa na kutembelea vivutio vya utalii
  nchini.

  Alisema inatarajiwa matangazo hayo ya utalii yatawafikia watazamaji milioni 800 kwa mwaka kupitia vituo mbalimbali vya televisheni vinavyorusha matangazo hayo pamoja na wale wanaofika uwanjani kwa ajili ya kuangalia mechi mbalimbali katika uwanja wa Seattle Sounders.

  CHANZO: NIPASHE
  Mara tunaambiwa Serikali imejitoa katika biashara!

  Waziri anatangaza utalii kweli ama ndiyo kwenda kuku Marekani? Kama Serikali inatangaza, je, Makampuni ya utalii yanafanya kazi gani?
   
 2. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ni habar zenye kutia faraja kwa sisi wa tz
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ninavyoona kazi ya TANAPA na Serikali kwa ujumla ni kutunza mbuga za Taifa na kuhifadhi wanyamapori na sio ya kutangaza utalii.
   
Loading...