TANAPA yafanikiwa kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema kuwa ukaguzi wa anga uliofanywa leo asubuhi katika Mlima Kilimanjaro umebaini kuwa moto wote umedhibitiwa lakini vikosi vya askari vimetawanywa kwa ajili ya tahadhari.
1602910877152.png

Moto huo uliozuka Oktoba 11 mwaka huu umeathiri eneo la kilomita za mraba 95.5 ambazo ni sawa na 5% ya eneo lote la hifadhi lenye kilomita za mraba 1,700.

TANAPA imesema kuwa udhibiti wa moto huo umetokana na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na askari, wananchi na Jeshi la Zimamoto.

Licha ya moto huo, shughuli za utalii katika Mlima Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida.
 
View attachment 1602801

Mwenyezi Mungu ashukuriwe kwa kuleta mvua
 
Haya ushazima, TANAPA wafanye jitihada ya kupandisha miti mengine au ndio ntolee hio?
 
Huu uzi utakosa wachangiaji..ungesema moto unaendelea saa hizi ungekuwa ukurasa wa 20.
Hongereni wote mliofanikisha kuuzima moto.
Kumbe Tanzania peoples power niwengi kuliko cha kijañi
 
Heading ingekua "Wananchi wafanikiwa kuzima moto Mlima Kilimanjaro." Taasisi na watu wengi sana walijitolea kwa kazi hii na wote wanastahili kutambuliwa na si TANAPA pekee
 
Back
Top Bottom