TANAPA yaanza Mchakato wa kuanzisha Cable Car Mlima Kilimanjaro

Cable car inatakiwa ianzie mbali na route za miguu.
Wapanda mlima kwa kutembea watumie njia na gate zilizopo ila kianzishwe kituo na gate jipya eneo tofauti kwa ajili ya watakaotumia cable car.
 
Wakiweka hayo makitu ndio mwisho wa kumuona JB wa Bongo movie na Diamond platnumz wakiishia kwenye mita 200 za mwanzo!
 
Mawazo yako ni kama mtu ujenge nyumba ya ghorofa nne na uweke lifti na ngazi, halafu useme wasiotaka lifti watapanda ngazi. Obvious wengi watatumia lifti hata wale wenye uwezo wa kupanda ngazi. Hivyo hivyo ukiweka cable car watu wengi watazitumia, hata wale wenye afya njema na uwezo wa kupanda mlima kwa miguu yao.

Vivutio ni vivutio kwa sababu ya uniqueness na sio kwa sababu ya wingi wa watalii. Utalii wa watu wengi mara nyingi sana ni haribifu. Watu wanaenda kwa ajili ya kupiga selfie tu na hivyo hawajali kuhusu hali ya mazingira waliyoyakuta. Wanatupa taka ovyo, wanajichukulia "souvenirs " bila kujali athari zake. Watadai watengenezewe vyoo n.k. Hata joto la pumzi za watalii zinaweza kuleta athari.

Nchi za wenzetu zenye watalii kuliko sisi sasa hivi wanafanya kila jinsi kuwapunguza. Sehemu kama Venice wana mipango ya kupunguza cruise ships zinazopeleka watalii n.k.
Mtu anaesema kuwa angependa kupanda mlima Kilimanjaro lakini hana muda sio mpandaji tunayemtaka.

Tusisahau kuwa eco system ya Kilimanjaro ni unique na sisi watanzania ndio tuna wajibu wa kuilinda kwa wivu mkubwa ili dunia na vizazi vyetu waweze kuifaidi.

Mimi ningependa sana kwenda North Pole lakini najijua baridi ya kule sitaiweza. Kwa mtazamo wenu basi itakuwa busara kama tukiyayusha barafu yote kule na kujaza heaters ili watu kama mimi tuweze kwenda.

Amandla...

Labda hujaelewa kidogo , wanaotumia Cable car ni watazama mlima, yaani wanaenda kwa ajili ya kitazama na kurudi, na wale wanaenda kwa njia ya kawaida ni wakwea mlima. Sasa nyinyi mnaosema wasio na mda sio wapandaji mnaowataka hiyo ni shida yenu, mtuke au mstake sisi tunasubiri cable car tupande zetu mlima.
 
As long as its constructive argument.Ndio maana dunia sio meza.
I dont see as constructive rather than conservative. Ukiachana na faida ya kuongeza mapato, Cable cars zitaleta ufanisi zaidi kwenye suala la usalama hasa kwenye ajali au dharula

Unakumbuka ile ajali ya moto? Ni wazi kwamba wakina Kigwangala walichelewa kufika eneo la tukio pia walishindwa kwenda za vifaa muhimu kwa wakati kwa sababu miundo mbinu hafifu.
 
Curiosity killed the cat, na ndio majaribio yatakayozika utalii wa nje wa kupanda mlima. Usitegemee mzungu atoke Ulaya kuja kusafiri kwenye cable car. Its completely nonsense. Hizi akili za kichina zitafuta umuhimu wa mlima Kilimanjaro

Sio hilo tu uchafuzi wa mazingira kwa kuruhusu utatili wa wapanda mlima dezo utatugharimu

Nina imani huyo kibosile aliyependekeza mpangi huo anatakiwa afukuzwe mapema iwezekanazo, ni hatari sana kuliko yule aliyeshindwa kula kiapo
Wewe ni hatari kwa taifa.
 
Ndugu yangu unasema kitu usichokijua kabisa. Jaribu kwenda kupanda Mlima Kilimanjaro huenda utaelewa kwanini hiyo Cable car haifai.

Ngoja nikupe elimu nyepesi kidogo.

-Suala la uokoaji wa dharula linaweza kufanyika kwa njia nyingi sana. Kuanzia kwa kubebwa na porter, Machela, Toroli hadi Helcopter. Na njia zote hizo mimi binafsi nimefika na kuzishuhudia zikifanya kazi vizuri sana. Na huwezi kuamini, njia salama zaidi kiafya ilikuwa ni kubebwa na watu(porters) au machela! Why? Mhanga atateremshwa taratibu step kwa step ili kukwepa janga la kufa ghafla kwa sababu ya high attitute crisis sickness(nadhani wataalamu wa Afya wanaweza kuwa wanajua zaidi kuhusu kitu inaitwa Acclimatization, sio kitu cha kukizembea).

-Kuhusu hadithi za kina Kigwangwa na moto, hizo achana nazo. Hakuna mtu aliyechelewa kufika, mahali palipozuka moto panafikika kirahisi na mtu yoyote, na wahusika wa TANAPA walifika kwa wakati tu, tatizo hawanaga vifaa vya kisasa vya kuzimia moto na manpower ilikuwa ndogo(hakukuwa na pesa za kuwalipa wanavijiji ili wachape kazi faster faster, waliambiwa wajitolee!).
Kifupi ule moto uliwaka zaidi ya siku tano, na Karibu siku zote hizo Kigwangwalla alikuwa huko (although tunaambiwa alikuwa akijinjali kwenye hoteli maaneo fulani ya hifadhi akila bata zake, kwenye moto alikuwa anafika kupiga selfie zake na kusepa)
 
Hahahahhahaaha huyu hapa mwingine ni mhanga anayeenda kupoteza ajira au huenda ni ndugu zako watapoteza ajira//tafuta kazi nyingine mkuu maana ni ngumu kushindana na technology
Curiosity killed the cat, na ndio majaribio yatakayozika utalii wa nje wa kupanda mlima. Usitegemee mzungu atoke Ulaya kuja kusafiri kwenye cable car. Its completely nonsense. Hizi akili za kichina zitafuta umuhimu wa mlima Kilimanjaro

Sio hilo tu uchafuzi wa mazingira kwa kuruhusu utatili wa wapanda mlima dezo utatugharimu

Nina imani huyo kibosile aliyependekeza mpangi huo anatakiwa afukuzwe mapema iwezekanazo, ni hatari sana kuliko yule aliyeshindwa kula kiapo
 
Labda hujaelewa kidogo , wanaotumia Cable car ni watazama mlima, yaani wanaenda kwa ajili ya kitazama na kurudi, na wale wanaenda kwa njia ya kawaida ni wakwea mlima. Sasa nyinyi mnaosema wasio na mda sio wapandaji mnaowataka hiyo ni shida yenu, mtuke au mstake sisi tunasubiri cable car tupande zetu mlima.
Unajichanganya. Kwanza umesema wanaotumia cable car ni watazama mlima halafu mwisho unasema mnasubiri cable car ili mpande mlima. Lipi ni lipi?

Amandla...
 
Sasa hivi gharama ya kupanda Kilimanjaro ni tarinan US $ 4000 kwa mtu. Mnadhani kuna mtu atakubali kulipa kiasi hiki ili aupande kwa lifti? Gharama ya kupanda mlima Everest ni US $ 40000. Mnadhani watu hawawezi kukodi helicopter kwa chini ya kiasi hiki ikawqshusha kwenye kilele cha mlima?
Wanaodhani ninapinga huu mradi ili tu nilinde vibarua vya porters mnakosea sana. Vibarua ni muhimu lakini sio kama kutunza mandhari ya mlima ambayo ni unique, sensitive na fragile. Tukijazana kule juu tutauharibu mlima beyond repair.

Majuzi tu Mahakama moja Ujerumani wamezuia ujenzi wa kiwanda cha Tesla kwa kuhofia kitaharibu makazi ya nyoka na mijusi. Wanachojua wenzetu ni kuwa tukiharibu mazingira na kuharibu eco system iliyopo ni next to impossible kukarabati. Mlima Kilimanjaro ni kazi ya Mungu na tukiuharibu hatatutengenezewa mpya.

Hatuna tofauti na jangali anaemuua kifaru ili apate dola 500 kwa ajili ya mlo wake wa waleo bila kufikiria kuhusu kipato cha muda mrefu cha dola hamsini hamsini atakazopata kutokana na watalii watakaokuja kuangalia kifaru huyo kama angekuwa hai. Tuache kuwa myopic.

Amandla...
 
Back
Top Bottom