TANAPA, je wanaozima moto Mlima Kilimanjaro mnawajali au mnawapuuza?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
TANAPA ni shirika kubwa sana linakusanya pesa nyingi kupitia Mlima Kilimanjaro ila cha ajabu ni kwamba, waliokwenda kuzima moto mlimani ni waliambiwa wawe watu wa kujitolea ambao walikusanywa Mgambo wa Kilimanjaro na Arusha hawa ni miongoni mwa waliokwenda kusaidiana na wengine kuuzima moto, sasa watu hawa wanaingia kwa shift kutoka chini kupanda mlima ambapo moto ulipo wanatumia masaa 3 na zaidi.

Mfano kuna group linaingia shift ya saa 12 jioni wanatoka saa 3 asubuhi cha ajabu kila mtu anafungiwa mikate mikubwa 3 au 4, soda ndogo ya portable 1 ya sh 500 na glucose ya kulamba basi hakuna chakula kingine. Hivi kweli hawa viongozi wanawaonaje hawa watu wa kujitolea wa kuzima moto hicho ni chakula? Chakula hicho na baridi uliyopo kule juu unaweza ukakaa nacho hadi saa 3 asubuhi?

Moto wanazima kwa majani unakata majani unapigapiga ndio uzime kweli are we serious TANAPA wameshindwa kukodi ndege za zimamoto ukizingatia ule moto ni mkubwa na unasambaa kwa kasi sana, mmeshindwa hata kuwapa mama ntilie tenda wawapikie ugali nyama kweli? Hakuna cha posho au incentive yoyote baada ya hapo utaambuliwa tena usafiri urudishwe walipo kuchukua, hapa ni kupimana uzalendo au.

Jana kuna mmasai mgambo walipomaliza tu wakarudi, ilipofika saa 1 jioni wakapigiwa simu kuwa moto umeanza tena warudi, kwani walikubali kurudi? Huenda wachache walirudi ila walio wengi wamekataa. Mabilioni inaliwa na wengine na wengine ndio wakufanya kazi za kujitolea.

EH MUNGU TUSAIDIE
 
Yaani hao TANAPA wanabahati nihuu uchaguzi watu wametingwa namambo yao. Wangekua washatumbuka kuanzia waziri,katibu mpaka mkurugenzi. Moto ule wameshindwa kutafuta hata ndege za kuzima moto eti kampuni binafsi imejitolea ndege ikafanye tathmini ya uharibifu.

Yaani ninarudia kusema,hao washukuru huu uchaguzi ingawaje lolote linaweza kuwapata pia. Tuendelee kuelekeza macho na masikio yetu kwa Gerson Msigwa
 
Moto unazimwa kwa mateke,vijiti,majani na rungu!

Hii ndiyo athari ya mtu mmoja kutawala kila kitengo na kila wizara.Vitengo na wizara hazina uhuru wa kuamua mambo yao wenyewe,ni mpaka wasubirie command kutoka kwa mtu mmoja.Mengi yanakuja ambayo yataumbua hii serekali ya kifisadi.
432890.jpg
 
Katika ule mkataba wa ununuzi wa vifaa vya jeshi la zimamoto ambao ulisitishwa/unachunguzwa, Mojawapo ya vifaa vilivyoorodheshwa ni Drones maalum za uzimaji moto.

Nadhani hapa ndipo palipohitajika hizo drones kufanya tathmini ya uharibifu na kufanya zoezi la uzimaji kuwa rahisi zaidi. Pia drones/ndege za uzimaji moto ni muhimu sana hasa kwny maeneo magumu kufikika...
 
Back
Top Bottom