Tanangozi, Iringa: Ajali mbaya ya daladala na lori, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,761
Habari nilizozipata ni kwamba kuna ajali mbaya imetokea eneo la Tanangozi, Iringa. Hiace iliyokuwa inatoka Iringa mjini kwenda Ifunda imegongwa na lori lilokuwa limefeli break. Kuna taarifa za vifo vya watu zaidi ya nane.
ajali1.jpg

Daladala baada ya kupata ajali.

ajali2.jpg

Lori la mizigo lililosababisha ajali baada ya kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki

Kwa taarifa zaidi naomba mliopo eneo hilo mtupatie.

Update
"Watu zaidi ya 20 waliokuwa wakisafiri na Hiace ya Iringa mjini Kwenda Ulete Iringa vijijini mkoani Iringa wamehofiwa kufa baada ya Hiace hiyo kugongwa na lori na kufunikwa

Taarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni wakati Hiace hiyo ikitoka Iringa kwenda Ulete na Lori likitokea Mafinga kuelekea Iringa mjini na kuwa ni dereva pekee wa Hiace ndie kapona na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Chanzo: Matukio Daima"

------
Ajali mbaya imetokea leo jioni eneo la Tanangozi mkoani Iringa ambayo imehusisha gari dogo la abiria (Daladala) na Lori la mizigo.

Katika ajali hiyo watu wengi waliokuwa katika daladala wanahofiwa kuwa wamefariki dunia.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amesema ajali hiyo imetokana na lori la mizigo kupata hitilafu katika mfumo wa breki hivyo kuligonga gari dogo.

Akizungumzia idadi ya waliofariki, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa hadi sasa kuna maiti nane lakini akasema kuwa anafatilia hivyo huenda wakakuta miili zaidi ya watu waliofariki.

Mkuu wa Mkoa ametoa tahadhari kwa madereva ambao magari yao ni mabovu kuhakikisha wanayatengeneza kwanza kabla ya kuyaingiza barabarani kwani yanahatarisha maisha ya watu wengi.
.......... .
tmp_26985-IMG-20161205-WA01281104303649.jpg
tmp_26985-IMG-20161205-WA0125-840280681.jpg
tmp_26985-IMG-20161205-WA0123-951679288.jpg
tmp_26985-IMG-20161205-WA0124-119326347.jpg
tmp_26985-IMG-20161205-WA0126-1342170884.jpg
 
Ajali mbaya sana hii, nahisi watu zaidi ya 10 watakuwa wamepoteza maisha. Hizi siku za mwisho wa mwaka zinakuwaga sio njema kabisa.
 
Mungu awatie nguvu wafiwa woote na wote walioguswa na ajali hiyo
 
Dec Hamas awajafunga mahesabu Labdaa mpandebasi lamaiti mtasalimika
 
Polen sana wafiwa wote pamoja na wanairinga kwa ujumla, Mungu awatie nguvu hususan katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom