TAMWA Zanzibar yaviomba Vyombo vya Sheria kuwachukulia hatua wanaopiga na kuua wanawake na watoto

G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
76
125
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kinaviomba vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa waliohusika na vitendo vya upigaji na uuaji wa wanawake na watoto vilivyotokea hivi karibuni, hapa Zanzibar.

Hivi karibuni msichana wa miaka 23 Sumaiya Mohammed Said mkaazi wa Jambiani Kikadini mkoa wa kusini Unguja amedaiwa kuuwawa kwa kupigwa mapanga na Imani Abdallah Abdallah umaarufu Kichele (38).

Tukio jengine la ukatili dhidi ya wanawake lilitokea huko Fuoni nyumba moja mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja ambapo bi Raya Khamis Mgeni (45) alidaiwa pia kushambuliwa kwa mapanga yeye na mtoto wake aliye chini ya mwaka mmoja.

Mashambulizi hayo yalipelekea kifo cha mtoto huyo asiye na hatia na kumjeruhi vibaya Bi Raya ambaye amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja tokea tarehe ya tukio, 30/8/2021.

Kwa mujibu wa rikodi za TAMWA ZNZ tangu mwaka 2016, matukio 19 ya mauwaji ya wanawake na watoto yameripotiwa (wanawake 15 na watoto wanne) ambapo ni matukio machache tu ndiyo yaliyofikishwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar yakiwemo ya Wasila Mussa (21) na Hajra Abdallah Abdallah (21).

Hivyo, TAMWA-ZNZ inaviomba sana vyombo vya ulinzi kukomesha vitendo hivi kwa kuwatafuta wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wapewe adhabu inayowastahiki.

Hali ya kuvamiwa wanawake na watoto na kupigwa inavunja haki ya msingi ya wanawake ya kuishi kwa amani na pia inawatia hofu katika kuendeleza shughuli zao muhimu za kimaendeleo.```

Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi TAMWA-ZNZ
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,214
2,000
Tanzania Nchi ya ajabu sana matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto mpaka sijui TAMWA wapige kelele ila mambo ya siasa utaona defender mpaka makanisani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom