TAMWA: Vipigo hupingana na Haki za Binadamu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Utafiti wa viashiria vya afya (TDHS 2015/2016) ulibaini kuwa asilimia 58 ya wanawake na 40 ya wanaume wanakubali kwamba ni sahihi mume kumpiga mke kwa sababu mbalimbali

Tafiti hizi zinadhihirisha wazi, kuwa jamii inahitaji elimu zaidi ya kufahamu madhara ya upigaji ni kupingana na haki za binadamu na huweza kupelekea matatizo ya kiafya na hata kifo.

Kipigo huondoa upendo, furaha, ushirikiano mzuri katika familia, pia husababisha chuki, visasi kwa watoto na athari za kisaikolojia katika familia.

Mazungumzo na majadiliano ni njia bora ya kutatua migogoro.

Baadhi ya makabila nchini Tanzania yana mila za Kurithisha wajane pindi waume wao wanapofariki.

Kurithisha wajane ni aina moja wapo ya ukatili wa kijinsia.

Ukatili huu hupelekea mifarakano katika familia na Jamii, humuathiri mjane kisaikolojia na hata kupelekea maambukizi ya maradhi kama VVU.
 
Back
Top Bottom