TAMWA: Ukimya kuhusu masuala ya rushwa ya ngono unapaswa kuvunjwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mila na desturi zimetufundisha ya kwamba masuala ya rushwa ya ngono hayazungumzwi, hivyo tuvunje ukimya kuanzia ndani ya vyombo vya habari mpaka katika jamii yetu kwa kuwa tunajua tatizo lipo tulifanyie kazi liweze kumalizika" Dk Rose Reuben: Mkurugenzi Mtendaji - TAMWA

Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zilizotolewa mwaka 2020, zinaeleza kuwa, kuanzia mwaka 2016-2020, matukio ya ubakaji yalikuwa kama ifuatavyo, 2016(7645),2017(8039), 2018(7617), 2019(7837) na 2020 matukio(7263).

Elimu na sheria kali hazina budi kutekelezwa ili kupunguza kasi ya matukio haya.

Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa, watumiaji wa huduma za mitandao ya kijamii wameongezeka kutoka 19,862,525 mwaka 2016 hadi 28,470,506 mwaka 2020.

Inaelezwa kuwa ongezeko hilo linaenda sambamba na ongezeko la ukatili wa kijinsia kwa njia ya mtandao.
 
Rushwa ya ngono hii vita ni ngumu sana hasa kwa nchi kama zetu ambapo ukosefu wa ajira unazidi kupasua mawingu.

Hivi sasa msailiwa awe wa kike ama kiume yuko tayari kutoa rushwa ya ngono apate kazi bila kushurutishwa kabisa.

Bado safari ni ndefu.
 
Back
Top Bottom