Tamu na chungu ziara ya Prof. Lipumba katika mikoa sita (6)

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Mwenyekiti Wa CUF Taifa Prof.Lipumba amefanikiwa kumaliza Ziara yake katika mikoa Takribani Sita nchini.

Ziara hiyo imeleta mafanikio makubwa sana katika Chama hususani kwa hali ya Siasa ya hivyi sasa ya kuzuia kufanya Mikutano ya Hadhara kwa Vyama vya Siasa Nchini,ila CUF Haikukata tamaa kwa kauli hiyo iliyotolewa na Serilkali kuzuia Mikutano ya Kisiasa Nchini.CUF iliendelea kufanya vikao vya ndani vya chama ila bado tunapata Usumbufu kwa Jeshi la Polisi Nchini.

Ziara ya Mwenyekiti ilikutana na Misukosuko hiyo mikubwa ya Jeshi la Polisi kwa kutaka pia kuzuia vikao vya ndani visikaliwe na kuzuia kabisa shughuli za Chama zisifanyike kama kufungua matawi na kupandisha bendera za Chama Jeshi la Polisi walizuia.

Wilaya ya HANDENI VIJIJINI likuwa ni wilaya ambayo mwenyekiti alikamatwa na jeshi la polisi katika Kijiji cha mgwe kwa madai ya kufanya vikao bila kibali.

Misukosuko hiyo imejitokeza karibia wilaya zote ambazo mwenyekiti alitembelea nchini Handeni vijijini,Handeni Mjini, kilosa, malinyi,Hanang,kilombero,Same,Kondoa Vijijini ,Kondoa Mjini, Arusha,Morogoro Vijijini,Morogoro Mjini.

Pia Ziara hiyo ilikuwa na manufaa makubwa sana katika Chama kwani wanachama walipata fursa ya kuzungumza na mwenyekiti na kupanga mambo mbalimbali kwa ajili ya Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu October, Pia wanachama walimuakikishia mwenyekiti wa Chama Taifa kuwa watahakikisha wanasimamisha wagombea katika maeneo yote na kujipanga kikamilifu katika hali ya ujenzi wa Chama.

Pia Wanachama walisema kwamba hatujakata tamaa na hatutakata tamaa katika hali inayoendelea hivi sasa ya baadhi ya Viongozi wa Upinzani Kuhamia CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom