Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Ndugu @kichangirl, hongera sana kwa hatua hiyo,mm namiliki mawazo kama matatu hv ambapo kabla ya mwaka kuisha mawili yatakuwa yameshaanza coz mtaji ninao tayari ila kiukweli haya mawazo nimeyachakata kweli na nimejipanga kisawasawa.Hapo kwenye viazi mabibo ni biashara ambayo naiadmire sana coz mwakani nafumua kama ekari 5 za viazi coz nishagain experience ya kutosha in this field,ila nitataka nipate connection ya wanunuzi au madalali hapo mabibo,kwa kuwa upo hapo dar na ulishapita mitaa ya mabibo sokoni,nikuombe tu bibie kama unaweza wa kunitafutia mawasiliano ya watu wanaodeal na hii kitu kwa ajili ya maandalizi ya mapema ya soko mwakani.
 
Ndugu @kichangirl, hongera sana kwa hatua hiyo,mm namiliki mawazo kama matatu hv ambapo kabla ya mwaka kuisha mawili yatakuwa yameshaanza coz mtaji ninao tayari ila kiukweli haya mawazo nimeyachakata kweli na nimejipanga kisawasawa.Hapo kwenye viazi mabibo ni biashara ambayo naiadmire sana coz mwakani nafumua kama ekari 5 za viazi coz nishagain experience ya kutosha in this field,ila nitataka nipate connection ya wanunuzi au madalali hapo mabibo,kwa kuwa upo hapo dar na ulishapita mitaa ya mabibo sokoni,nikuombe tu bibie kama unaweza wa kunitafutia mawasiliano ya watu wanaodeal na hii kitu kwa ajili ya maandalizi ya mapema ya soko mwakani.
Okay mi ni ME sio bibie. Nakutumia namba ya dalali mmoja PM ni mshkaj mwelewa mcheki unaezapata ABC za sokoni kutoka kwake
 
Kumradhi sana @Kichangirl kwa kudhani ww ni KE kumbe ni ME,nilidhani girl ya mwishoni kwenye id yako inamaanisha jinsi,all in all thanx for your support.
 
Ndugu mkewangu ni mrokole ana imani kali sana anasali karibia siku zote za week, hata chanzo cha kufilisi duka ni sababu alikuwa anafungu muda mchache muda mwingi yuko kanisani

Ulimuoa akiwa mlokole au ameokoka ndani ya ndoa?
Kama ni ndani ya ndoa mpige stop huo ukichaa wewe ni kichwa cha familia hakuna kinachokushinda hapo
 
Mim nakumbuka siku ya kwanza nafungua biashara yangu nilipata wateja 5 siku ya pili nilipata mteja 1 ilinichukua km miezi3 mpka kuanza kuchanganya nimshukuru mungu Leo Nina miaka7 kwenye hii biashara Nina nyumba 2 hapa mjin na kiwanja
Unaweza kunijuza hiyo biashara mkuu?
 
Biashara mbaya toka mwezi 7 na mwezi ujao natakiwa nilipie kodi ya flem
Akiba sina ,bidhaa zimepungua ,pesa ya kuongezea bidhaa sina

Huwa inafika muda natamani hata ningeajiriwa tu,
Nikasubiri hiyo pesa ya mwisho wa mwezi.
JAMANI KUJIAJIRI KUNA CHANGAMOTO KUBWA.
 
Ndugu @kichangirl, hongera sana kwa hatua hiyo,mm namiliki mawazo kama matatu hv ambapo kabla ya mwaka kuisha mawili yatakuwa yameshaanza coz mtaji ninao tayari ila kiukweli haya mawazo nimeyachakata kweli na nimejipanga kisawasawa.Hapo kwenye viazi mabibo ni biashara ambayo naiadmire sana coz mwakani nafumua kama ekari 5 za viazi coz nishagain experience ya kutosha in this field,ila nitataka nipate connection ya wanunuzi au madalali hapo mabibo,kwa kuwa upo hapo dar na ulishapita mitaa ya mabibo sokoni,nikuombe tu bibie kama unaweza wa kunitafutia mawasiliano ya watu wanaodeal na hii kitu kwa ajili ya maandalizi ya mapema ya soko mwakani.
Nakushauri kabla hujaamua kuwavaa madalali moja kwa moja ni bora uende mwenyewe kwenye masoko ya viazi na ujifanye 'dalali' kuwa eti tayari una mzigo wa viazi kwa bei ya 000 tshs utakaopatikana tarehe x. Halafu chukua na mawasiliano yao hao wauzaji. Mimi niliwahi kufanya hivi kipindi namsaidia mjomba kuuza nanasi kutoka kiwangwa bagamoyo na kuzileta mjini. Madalali wa kibongo ni wakandamizaji sana. Walishangaa Canter inashusha mzigo bila wao kujua na unauzwa fresh tu.
 
Nilianzaga biashara ya mpesa huko vijijini nkamuweka wife changamoto take ni chuma ulete mingi sana ukipata faida laki 4 wao wanachukua lak6 sio mchezo mpaka nilifunga

Ila ntarudi tena kuifanya kwan inalipa sana
 
Kumradhi sana @Kichangirl kwa kudhani ww ni KE kumbe ni ME,nilidhani girl ya mwishoni kwenye id yako inamaanisha jinsi,all in all thanx for your support.
Wewe ndiye unakosea kuisoma Id yake...ni Kichangiri na siyo Kichangirl. Id yake haina neno "girl"
 
Nakumbuka nilikuwa na dem huyo....yan yeye aliamini kwenye ajira...aliona cwezi biashara kabsaaaa...!!na ubaya zaidi mimi nd nlmpenda mno so mostly mtaji ulienda kwake kwa vizawadi na vijihela vya shule

Dem anajua hali n ngum...sina ajira...na ndo kwanza naanza biashara anauliza "lini utakuwa na kwako?"

Msekemseke mwsho wa siku nkaamua tuachane....hapo nd nkapata hasira zaidi ya kutafta

Nilipambana kwa hali na mali
Nilijinyima just kuprove kuwa nnaweza
Nilitafta ushaur wa kibiashara mitandaon na kwa wafanyabiashara wenzangu....!!

Kuna watu nakumbuka walinicheka wkt naagza bidhaa za elf 30...!!lakini now tunaheshimiana maana nnaagiza mpk za laki 3

Biashara imenona
Nmepanga na chumba kimejaa
Kiwanja mwakani natk kuanza ujenzi

Juzi juzi yule kima akataka kurudi...!!nikakumbuka kuwa yawezekana nmefanikiwa kwakuwa sipo nae....!!nikampa jibu simple "siwezi kukuamini tena"

Biashara zina chngamoto zake....lkn znazotuua ni changamoto za nje...!!
Mkuu umetoa hamasa kubwa sana na funzo ndani yake,hongera kwa kua na msimamo na kutambua nn unataka maishani.
 
Biashara ni ngumu kwavile imeambatana na changamoto ambazo wakati mwingine ni vigumu kuziepuka.

Mfano:

1. Uzoefu
2. Uaminifu
3. Uvumilivu
4. Usimamizi n.k

Kwanza nilianza na ufugaji wa nguruwe mmoja jike. Nikaenda nae vizuri tu. Kushika mimba, kabla hajajifungua akaanza kuumwa. Akawa anakosa nguvu za miguu, kuna jamaa mfugaji mzoefu, nilipomuelezea akasema kuna sindano inabidi achomwe. Tulipomchoma ile sindano, baada ya siku mbili mimba ikatoka. Nguruwe akaja akapona. Akashika mimba nyingine na kujifungua vitoto 5,mmoja akafa. Tukaenda nao pia fresh, ila wanakula kupita maelezo. Vilipoacha kunyonya, tukauza 3 kimoja kikabaki. Baada ya kuona uelekeo sio, mama mtu nikachinja na kuuza nyama buchani. Hela haikurudi. Nikapiga chini huo mradi.


Nikasogea kwenye kilimo. Tikiti na maharage. Hudumia sana shamba. Kwenye kuvuna, tikiti ilinipiga hasara moja matata sana. Nikapiga chini. Nikahamia kwenye kusafirisha maharage toka mkoani kuleta Dar. Nilichora mchoro vizuri tu. Nikanunua mzigo wa kutosha na kuuagiza uje mjini. Huku town alikuwepo jamaa yangu mmoja, mtu wa karibu sana (alikuwa mtu wa karibu sana, maana sio wa karibu tena). Jamaa akaupokea mzigo na kuusimamia kwa wale madalali wauzaji. Daily ananipa mrejesho wa maendeleo, nikawa nafurahishwa na bidii yake. Kumbe daily anaenda kuchukua hela alaf anaweka heshima mitaani na bar (mimi sina habari). Kuja kustuka, kashakula hela 75%, huku mimi ananiongopea madalali hawajampa bado. Biashara ikafa.


Nikageukia kwenye tangawizi. Nikalima vizuri na kila kitu kikawa chini ya usimamizi wangu mwenyewe. Kwenye mavuno mambo hayakwenda vizuri, ila walau niliona mwanga fulani hivi. Ikabidi niwekeze tena kwenye ili zao. Msimu wa pili kilichotokea ni afadhali ya msimu wa kwanza. Kama sijapalaraizi shambani, basi sidhani kama ntakuja kupalaraizi maishani mwangu. Kifupi shambani kitu pekee nilichoambulia ni kuitwa bossi na wale vibarua, zaidi ya hapo niliwafaidisha wao tu mimi sikupata kingine. Nikasema kilimo kwangu bye bye, siingii shambani tena.

Nikaamua kufungua duka la nafaka kwa reja reja. Ushindani niliokutana nao sio wa kawaida. Mara leo mtu aje kuulizia, then anakwambia ntarudi kuchukua kiasi kadhaa siku nyingine. Kumbe nae anafanya biashara hiyo hiyo so alikuja kunichunguza. Mara wamama watake mkopo. Kipindi mchele umekuwa hadimu mtaani, bei ya chini ilikuwaga 1500 kwa kilo, ila watu wanataka mchele wa 1300,tabu tupu. Baada ya miezi 4,nikaamua kupiga chini. Maana mzunguko ulikuwa mdogo saaana, nikawa namfaidisha mwenye fremu tu.


Kutokea hapo ndio nikaamua kuwekeza kwenye kitu kingine kabisa, tena nilianza na mtaji wa 1.5 milions. Nikaamua kusimamia mwenyewe mwanzo mwisho, hapo atleast ndio mwanga kidogo ukaonekana. Now nafikiria ni jinsi gani nitaitanua .

***** ****** ****** ******

Biashara zinahitaji kujitoa. Ukiweza kuweka hela yako sehemu, basi hakikisha unaweza kuweka na muda wako. Vinginevyo utaishia kufaidisha wengine.
Ukiskia wapambanaji bhasi ndio kama weae mkuu
 
Mnamo tar21 mwez wa tisa mwaka huu nlifungua wakala (mpesa, tigo, airtel, na halotel) kariakoo nakumbuka cku hyo ckufanya muamala hata mmoja. Nliwaza nkamwambia Mungu n nini hiki sasa. Daah wateja wakawa kidogo wanakuja mwanzo wa mwez wa kumi ka kamishen kakaja hakafiki hata elfu hamsini daah kweli nkavunjika moyo sana.

Leo namshukuru Mungu kidogo wateja wanakuja japo nnaamini hadi mwakani nitasmama kwa kudra za mwenyezi Mungu. Sitaki kabisa kuajiriwa kwakuwa nishaajiriwa miaka miwili skuambulia chochote zaid ya kulipa kodi na kununua vitu vya ndani bas
Ukawa unajiuliza watu wote hawa wanakuja kariakoo na sipati mteja hata mmoja wa kutoa hela.Hongera mkuu Mungu atafungua njia mambo yatakaa sawa
 
Mkuu Ilikuwa MKAA nikiwa Iringa naaangalia Fursa nikapata wazo la kusafirisha mkaa kwenda Dar.

Nikampigia simu jamaa yangu Dar akaniambia huku mkaa ni mali mvua zinanyesha hataree ukileta huo mkaa unapata hela nzuri.

Kwa kweli niliingia porini nikaandaa magunia 150, nikakata vibali vyote. Jamaa yangu ananisumbua huo mkaa mbona hauji nimeshapata wateja wa mastore. Nikapata moto zaidi wa kumalizia maandalizi.

Kwa kweli safari ilipoanza kwenda dar njiani nilikuwa nawaza kama jamaa atakuwa amenidanganya huu mzigo nitaupeleka wapi na ni mara yangu ya kwanza kukanyaga dar.

Gari iliingia dar saa 12 jioni jamaa akanipokea akawapigia simu wateja aliowaandaa akawaambia kesho asubuhi gari itashusha. Nimelala guest usiku usingizi hauji bei jamaa yangu aliyokuwa ananitajia nikipiga hesabu na faida ya milioni 2 na laki 6.

Asubuhi na mapema nikaenda eneo la tukio sikuamini kuona wateja wamesimama nyuma ya gari wanahimiza mlango ufunguliwe, wengine wanapanda kwenye Bomba wanachungulia mzigo ndani wanausifia.

Mlango ukafunguliwa wakaanza kugombania wanashusha wanapanga kimafungumafungu kwa kweli nikalipwa hela cash tena kwenye ile bei nikaongeza 5000 kwa gunia baada ya kuona wanagombania.

Ilikuwa biashara yangu ya kwanza baada ya kumaliza chuo ila nilishaachana nayo now nafanya biashara nyingine.
Kuna rafiki yangu alikua anatoa mkaa hukohuko iringa kuleta dar,kilichomkwamisha ni dhuruma za madalali.
 
Kikubwa katika dunia hii hakuna biashara ambayo hailipi....Maisha ya binadamu na viumbe vingine ili yaende yanahitaji matumizi ya bidhaa...fikiria mtu anaagiza contena ya vijiti vya kusafishia masikio au kusafishia meno anauza na vinaisha....wengi tunaanza biashara bila kufanya utafiti wa kutosha wa mahitaji ya soko....mtaji unaohitajika....bei ya kuuzia na kununulia...eneo la kufungulia biashara... uvumilivu ni wa muhimu sana...biashara nyingi sio rahisi ukafungua leo na kupata faida...inahitaji muda kwani wakati unaifanya ndio pia unajua vitu ambavyo mwanzoni ukuvijua...biashara ni kitu hai ... ni kama mtoto...anaziliwa ..anakaa...anatambaa...usimamizi wa biashara pia ni muhimu sana...Niliwahi kwenda Guangzhou baada ya kupata maoni hapa Jf....nilipofika sokoni nakuta bei ya bidhaa nilizohitaji ni kubwa kuliko hata hapa kariakoo...kwa kweli nilichanganyikiwa sana...na huku niliambiwa wewe nenda tu bei ni rahisi sana.
 
Kuna mazingira mabaya ya kibiashara ndani ya hii nchi.Msihangaike kumtafuta mchawi.
 
Sometimes inabidi uangalie sababu hasa ya issue kugoma. Huwezi kuendelea kukomaa tu eti ukitegemea mambo yatajipa wakati unaona odds are against you.

Ufe na tie shingoni? No way out man.

Kingine mkuu, the way unavyosoma nilichoandika unaweza ukahisi things were simple. No broh. The hustle was real.
Sawa sawa, nimekusoma mkuu kwa ufafanuzi zaidi ulioleta.
 
Back
Top Bottom