Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Biashara ni ngumu kwavile imeambatana na changamoto ambazo wakati mwingine ni vigumu kuziepuka.

Mfano:

1. Uzoefu
2. Uaminifu
3. Uvumilivu
4. Usimamizi n.k

Kwanza nilianza na ufugaji wa nguruwe mmoja jike. Nikaenda nae vizuri tu. Kushika mimba, kabla hajajifungua akaanza kuumwa. Akawa anakosa nguvu za miguu, kuna jamaa mfugaji mzoefu, nilipomuelezea akasema kuna sindano inabidi achomwe. Tulipomchoma ile sindano, baada ya siku mbili mimba ikatoka. Nguruwe akaja akapona. Akashika mimba nyingine na kujifungua vitoto 5,mmoja akafa. Tukaenda nao pia fresh, ila wanakula kupita maelezo. Vilipoacha kunyonya, tukauza 3 kimoja kikabaki. Baada ya kuona uelekeo sio, mama mtu nikachinja na kuuza nyama buchani. Hela haikurudi. Nikapiga chini huo mradi.


Nikasogea kwenye kilimo. Tikiti na maharage. Hudumia sana shamba. Kwenye kuvuna, tikiti ilinipiga hasara moja matata sana. Nikapiga chini. Nikahamia kwenye kusafirisha maharage toka mkoani kuleta Dar. Nilichora mchoro vizuri tu. Nikanunua mzigo wa kutosha na kuuagiza uje mjini. Huku town alikuwepo jamaa yangu mmoja, mtu wa karibu sana (alikuwa mtu wa karibu sana, maana sio wa karibu tena). Jamaa akaupokea mzigo na kuusimamia kwa wale madalali wauzaji. Daily ananipa mrejesho wa maendeleo, nikawa nafurahishwa na bidii yake. Kumbe daily anaenda kuchukua hela alaf anaweka heshima mitaani na bar (mimi sina habari). Kuja kustuka, kashakula hela 75%, huku mimi ananiongopea madalali hawajampa bado. Biashara ikafa.


Nikageukia kwenye tangawizi. Nikalima vizuri na kila kitu kikawa chini ya usimamizi wangu mwenyewe. Kwenye mavuno mambo hayakwenda vizuri, ila walau niliona mwanga fulani hivi. Ikabidi niwekeze tena kwenye ili zao. Msimu wa pili kilichotokea ni afadhali ya msimu wa kwanza. Kama sijapalaraizi shambani, basi sidhani kama ntakuja kupalaraizi maishani mwangu. Kifupi shambani kitu pekee nilichoambulia ni kuitwa bossi na wale vibarua, zaidi ya hapo niliwafaidisha wao tu mimi sikupata kingine. Nikasema kilimo kwangu bye bye, siingii shambani tena.

Nikaamua kufungua duka la nafaka kwa reja reja. Ushindani niliokutana nao sio wa kawaida. Mara leo mtu aje kuulizia, then anakwambia ntarudi kuchukua kiasi kadhaa siku nyingine. Kumbe nae anafanya biashara hiyo hiyo so alikuja kunichunguza. Mara wamama watake mkopo. Kipindi mchele umekuwa hadimu mtaani, bei ya chini ilikuwaga 1500 kwa kilo, ila watu wanataka mchele wa 1300,tabu tupu. Baada ya miezi 4,nikaamua kupiga chini. Maana mzunguko ulikuwa mdogo saaana, nikawa namfaidisha mwenye fremu tu.


Kutokea hapo ndio nikaamua kuwekeza kwenye kitu kingine kabisa, tena nilianza na mtaji wa 1.5 milions. Nikaamua kusimamia mwenyewe mwanzo mwisho, hapo atleast ndio mwanga kidogo ukaonekana. Now nafikiria ni jinsi gani nitaitanua .

***** ****** ****** ******

Biashara zinahitaji kujitoa. Ukiweza kuweka hela yako sehemu, basi hakikisha unaweza kuweka na muda wako. Vinginevyo utaishia kufaidisha wengine.
Kwel kabisa
 
Nimeshaingiza products kama tano hivi sokoni kama mjasiriamali asiye na kampuni ...
Zote zimekufa kuhusu.

Nikafungua mgahawa .. fanta Sana KAZI ... Human resource chamgamoto kwa sehemu nilipo wanaridhika mapema mno mtu akikunja ila 150 a month humwoni tena .

Means inabidi uanze upya.

Ilibidi niingie front me mwenyewe .. niandae ,nitafute orders na nisambaze/nifaye delivery alone .

Mgahawa ukasimama tena nkasema huu ndo wakati wa kuangalia mitikasi mingine ikiwemo kuraise funds za startups zangu nyingiñe ...
Wiki tatu tuu nilimwachia Yule binti mgahawa ukadedi.

Nikaingia kwenye Biashara ya lubricants ... Kifo cha mende nkapigwa mande ...

Nlikuwa na kaeneo kangu nikakauza last year mwishoni bei ya hasara nikaamua kuitumbua .

Sasa hv naandaa proposal kuomba funds Us embassy 😂😂😂😂
 
Changa'moto niliokutana nayo katika biashara zangu ni 'human resource' kupata mtu mwaminifu self driven and determined katika kazi zangu, limenichelewasha kua millionaire....watanzania wengi wakiwemo na ndugu sio waminifu hawapendi kazi boss wao anachukuliwa kama adui wao
Bosi naomba kazi hautajutia, mm ni mtaalamu wa masoko
 
Back
Top Bottom