ANKO JEI
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,278
- 2,364
Habari wadau, naimani kila mmoja yuko poa na kama mambo hayajakaa sawa basi hayo ni mapito tu, yatapita.
Katika maisha ya sasa ujasiriamali ni jambo mtambuka, linahubiriwa kila kona mpaka kwenye nyumba za ibada, vijana kwa wazee wanaanzisha vibiashara iwe ni kuuza chakula mpaka vijuice point kama vya Sinza na Kinondoni.
Tofauti na watu wengi tunavyofikiri kabla ya kuanza ujasiriamali, kiukweli kuanzisha biashara ni ngumu na kuna changamoto nyingi, mpaka muda mwingine unatamani usingeanza hiyo biashara kutokana na magumu unayopambana nayo mpaka biashara isimame vizuri. Katika kutambua hilo ningependa kila mmoja aweze kutoa tamu na chungu alizokutana nazo wakati anaanza biashara ili na wengine wasione kama ni wao tu wanaopitia changamoto.
Nianze na mimi binafsi, baada ya kumaliza chuo nilikuwa nishakomaa kwenye maswala ya Youtube nikawa napata kiasi fulani cha pesa kinachotosha kusongesha life la kibachela. Baada ya kusave sana nikaamua kufungua studio ya picha mkoani, hapo ndipo shughuli ilipoanza kwanza nilifungua sehemu ambayo karibu kuna studio. Kiukweli ile kufungua asubuhi mpaka jioni hakuna anayekuja hata kuulizia picha ya passport size ilikuwa inanipa shida sana.
Yaani unaona wateja wanavyomiminika karibu na kwako lakin wewe hakuna kitu, hadi unatamani ofisi yako ndio ingekuwa ya jirani yako. Muda mwingine unasahau wewe ndio unaanza unataka kushindana na aliyeanza miaka miwili iliyopita. Yote hii ni kitete tu cha biashara ndogo, bado sijasimama vizuri japo naanza kupata angalau wateja wa kuokoteza lakini msoto ni wa hali ya juu.
Itapendeza endapo na wengine watashare changamoto wanazopata.