Tamu na Chungu katika mahusiano

VINS

JF-Expert Member
May 10, 2014
293
195
Kila mtu anapoingia kwenye mahusiano huwa anatarajia mambo furani(mfano; amani, furaha, upendo, heshima, etc) atayapata kwa mwenzi wake. Mara nyingi hasa siku za mwanzo mwanzo, mambo yanakuwa ya furaha sana.
Kadri siku zinavyosonga tukiwa ndani ya mapenzi, mambo huwa yanaanza kubadilika, na vitu kama hasira, chuki, nk vinaanza kujitokeza. Hapa kwa kifupi mambo yanaanza kuwa mabaya. Ebu tujadili kama wanna JF, nini tufanye mahusiano yawe ni ya shida na raha?



MAMBO 10 YA KUFANYA UHUSIANO UBAKI KWENYE FURAHA SIKU ZOTE

1. FANYA UCHAGUZI SAHIHI

2. JIELEZE
Migogoro mingi baina ya walio kwenye uhusiano husababishwa na wenzi kutowafahamu vyema wenzao. Usiingie katika mkumbo huu, ni suala la kujieleza tu. Kumweleza mpenzi wako ulivyo, kutamfanya ajue vitu unavyopenda na usivyopenda. Aidha, kama unao udhaifu wowote wa kiafya na kadhalika, mweleze mwenzako.
Kumweleza kutamfanya ajiamini kuwa anapendwa. Kunaonesha unavyojiamini na unayetaka mwenzako ashirikiane na wewe katika hali uliyonayo. Si vibaya mwenzio kukufahamu kwamba una hasira sana. Yes! Maana akishajua hilo, ataacha utani unaokaribia kukuudhi maana anajua vizuri kuwa una hasira za karibu.
Ipo mifano mingi sana, lakini kikubwa cha kushika katika kipengele hiki ni kuwa mkweli kwa mwenzako kuhusu maisha yako. Acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa, wakati ni wa kawaida. Kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni hazina iliyojificha ndani ya moyo.
Kama anakupenda, anakupenda tu! Siku akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana. Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka ndani ya moyo wako. Naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro.

3. MPE UHURU
Wengi wanaamini kumbana mpenzi ni njia sahihi ya kumfanya awe mwaminifu, si kweli. Kuna wenye tabia ya kuvizia simu za wenzao na kuzipekua, si utaratibu mzuri. Mpe uhuru, usimbane! Kuonesha kumwamini sana mpenzi wako, kunamfanya naye aishi ndani ya uaminifu.
Kumchunga hakumnyimi kuendelea na mambo yake, sana sana atafanya kwa siri kubwa. Kumpa uhuru, kutamwogopesha, atajua yupo na mwaminifu ndiyo maana hafuatiliwi, hapo utakuwa umechochea naye awe mwaminifu kama

4. MSIFIE
Kati ya mambo muhimu kabisa kumfanyia mpenzi wako na kulifanya penzi kuwa jipya ni kumsifia. Unapomwambia mwenzako kauli nzuri za kumbembeleza kuwa yeye ni mzuri, anakuvutia kwa kila hali, unajenga penzi.
Unamfanya anajihisi wa thamani, atajiamini kuwa yeye ni mkamilifu, si kwa watu wanaomzunguka pekee, bali hata wewe ambaye umemchagua na kumfanya awe wako.
Kama huna utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, huu ni wakati wako wa kufanya hivyo kwa lengo la kuzidisha mapenzi na kuyapa nguvu.

5. SAIDIA KUKUZA UHUSIANO WENU
Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha penzi linazidi kukua siku hadi siku. Kwa maana hiyo, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kukuza uhusiano wenu.
Kuna mambo mengi sana ambayo yakifanyika, yanakuza uhusiano. Vipo vitu vya kufanya, kutoka pamoja ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano. Rafiki zangu, mnapokwenda katika matembezi, husaidia kubadilisha mapenzi na kuonekana mapya.
Si lazima kwenda nje ya mji, kikubwa ni kuzingatia mfuko wako. Hata mkienda mahali pa kawaida tu, mkanywa juice na keki, bado ni nafasi nzuri kwenu ya kukuza uhusiano huo.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya hivyo, lakini hutakiwi kumsubiri mwenzako afanye, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unamfanya mwenzi wako afurahie uhusiano wenu. Kufanya hivyo, kutampa deni na yeye la kufanya hivyo kwako.

6. MPE NAFASI
Hapa hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu. Mathalan unataka kununua kiwanja Gongo la Mboto; Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako.
Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao.
Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake.
Kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako. Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako

7. TUMIA MAJADILIANO ZAIDI
Yamkini wote wawili mlifanya majadiliano kabla ya kufikia maamuzi ya ndoa, basi ni wajibu wenu kuishi katika majadiliano kila siku. Wapo watu wasiopenda kuona ndoa za watu zinakuwa na furaha. Wataingilia na kuwafanya mgombane. Inawezekana pia mkapishana kauli katika mazungumzo, busara huhitajika.
Kutofautiana kwa kauli pamoja na vitu vingine, vinaweza kumalizwa kwa njia ya majadiliano. Jadilini katika lugha nzuri itakayomfanya mwenzio aone thamani yake.
Mkijadili yote kwa uyakinifu, mwisho mtagundua kumbe kilichokuwa kinawatatiza ni kitu kidogo ambacho hakikuhitaji nguvu kubwa kukitatua. Mnapojadiliana ni rahisi pia kutambua kosa lilikuwa wapi au lilisababishwa na nani, hivyo ni rahisi kumuepuka.

8. PALIZI YA NDOA
Kama ilivyo kwa mazao yakiwa shambani yanavyohitaji kupaliliwa ili yaweze kushamiri, vivyo hivyo katika ndoa. Ndoa inapaswa kupaliliwa kila siku. Jaribu kila wakati kusoma alama za nyakati, vitu gani anavipenda mwenzako basi umfanyie kila wakati.
Mfano unaweza kupanga siku moja katika wiki ukamchukua mkeo au mumeo na kumtoa nje kimatembezi. Ndoa hupaliliwa na vitu kama hivyo. Zawadi za hapa na pale zisipungue, acha kuishi kwa mazoea eti kwa kuwa tayari ni mkeo au tayari ni mumeo.
Unapoipalilia ndoa katika staili za zawadi, mitoko na vitu vingine huifanya ionekane mpya kila siku. Mnunulie mkeo au mumeo vazi unaloona linaendana na wakati mlionao.

9. EPUKA MANENO YA KUUDHI
Kuna wakati wenzi wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa! Kwa mfano, unakuta mpenzi anamwambia mwenzake: "Mh! Na wewe unanuka sana mdomo!"
Kauli gani hiyo kwa mpenzi wako? Mwanaume unalala naye kila siku, kwa nini umwambie ananuka? Wewe ukifanya hivyo, huko nje wamuambieje? Kwanza kama ni kweli ana tatizo hilo, ni jukumu lako kumtibu, lakini pia kumtunzia siri.
Kama nje anachekwa, ndani ya familia pia anachekwa, wapi atapata faraja? Yapo maneno mengi sana yenye kuudhi, lakini hapa nitataja machache. Wengine wanawaambia wenzao wananuka kikwapa, hawajapendeza, hawana akili nk.
Haya ni maneno ya kuudhi. Hebu fikiria kauli kama hii mtu anamtamkia mkewe! "Yaani kweli wewe huna akili, kitu kidogo kama hicho kweli unaweza kukosea? Ndiyo maana wenzetu wanafanikiwa kimaisha, wanatuacha. Sijui nilikutana na wewe wapi?...maisha yangu yanazidi kuwa giza tu, nikiwa na wewe!"
Acha maneno ya kufuru, kwani siku zote hukuona upungufu wake? Kuwa makini na kauli zako. Ndoa yako utaivunja wewe mwenyewe, pia kama ni kuijenga, utaijenga wewe mwenyewe!

10. UBORA KATIKA TENDO LA NDOA
Hapa ndipo panapotakiwa kupewa heshima kubwa zaidi kuliko vipengele vyote vilivyotangulia.
VINS, tendo la ndoa ni la heshima. Halitaki papara na linatakiwa kupewa nafasi na kila mmoja kuridhika. Acha kujifikiria mwenyewe, maana hapa ndipo panapopatikana mianya ya kutoka nje ya ndoa.
Hakikisha mwenzako anaridhishwa na wewe mnapokuwa chumbani. Tafuta elimu zaidi ya kufurahia tendo hilo ili mwenzako awe na sababu ya kuwa na wewe. Sikia nikuambie, tendo la ndoa kwa wanandoa hasa waliozoeana linachosha!
Huu ni ukweli ambao wengi wanaupinga. Yes! Linachosha na kukikanaisha. Hakuna kipya. Mwanaume yule yule. Kitanda kile kile, chumba kile kile. Lazima umchoke.
Hata hivyo, ukiwa mbunifu utaendelea kumuona mwenzako mpya kila siku. Badilisheni mazingira, tafuteni muda wa kutoka pamoja angalau mara moja ndani ya miezi mitatu – kwa mwaka mara nne.
 

Attachments

  • 1400780322721.jpg
    1400780322721.jpg
    33.2 KB · Views: 400
  • 1400780337938.jpg
    1400780337938.jpg
    17.8 KB · Views: 354
  • 1400780597554.jpg
    1400780597554.jpg
    54.5 KB · Views: 336
  • 1400780617007.jpg
    1400780617007.jpg
    18 KB · Views: 333
tangia nianze mahusiano na huyu mtu hayajawah kuchuja wala kupungua makali hata siku moja utathan tuna wiki kumbe tuna miez kumi tayari, kila siku inakuwa zaidi ya jana. hili huwezekana tu kama wote mpo really.. hamdanganyan, i really enjoy the life
 
tangia nianze mahusiano na huyu mtu hayajawah kuchuja wala kupungua makali hata siku moja utathan tuna wiki kumbe tuna miez kumi tayari, kila siku inakuwa zaidi ya jana. hili huwezekana tu kama wote mpo really.. hamdanganyan, i really enjoy the life


guuuuud
 
mkuuu kikubwa nikijua umuhimu wa mahusiano pia kila mmoja anapokosea akubali lisa haraka na aombe msamaha, pia kila mmoja ajifunze kishusha presha ya mpenzi wake pindi anapo kasirika
 
Nini kifanyike ili mahusiano yawe ni ya shida na raha?

looh mkuu nahisi kuna kitu unataka kusema ila kufafanua umeshindwa ila nitajaribu kuchangia


MAHUSIANO YA RAHA NA SHIDA INABIDI WOTE MUWEKE MEZANI MIOYO YENU KUSIWE NA TOFAUTI KUBWA NA HATA IKITOKEA MNAKUA WILLING KUREKEBISHA NA KUENDELEA

au labda ulikua unaongelea hela

huwezi lazimisha amani kama hamna hela(shida side)
INAEZA FIKIA HATUA HATA KUSIMAMISHA HUSIMAMISHI
UNAWAZA TU PESA
ila pia raha ya material thing ni ya kudumu kwa sharti moja kuu USIFILISIKE
SASA MKUU KUFILISOKA KUPO KUFULIA KUPO LAKINI KUPATA PIA KUPO huwezi force chochote kila kitu hutokea
 
Moyo wa mtu kichaka. Kama umempenda wewe mpende tu,hakuna namna utajua kama naye atakupenda kwa shida na raha.
Ni kwa Neema tu!!!
 
tangia nianze mahusiano na huyu mtu hayajawah kuchuja wala kupungua makali hata siku moja utathan tuna wiki kumbe tuna miez kumi tayari, kila siku inakuwa zaidi ya jana. hili huwezekana tu kama wote mpo really.. hamdanganyan, i really enjoy the life

Ni mapema mno!!
 
looh mkuu nahisi kuna kitu unataka kusema ila kufafanua umeshindwa ila nitajaribu kuchangia


MAHUSIANO YA RAHA NA SHIDA INABIDI WOTE MUWEKE MEZANI MIOYO YENU KUSIWE NA TOFAUTI KUBWA NA HATA IKITOKEA MNAKUA WILLING KUREKEBISHA NA KUENDELEA


au labda ulikua unaongelea hela

huwezi lazimisha amani kama hamna hela(shida side)
INAEZA FIKIA HATUA HATA KUSIMAMISHA HUSIMAMISHI
UNAWAZA TU PESA
ila pia raha ya material thing ni ya kudumu kwa sharti moja kuu USIFILISIKE
SASA MKUU KUFILISOKA KUPO KUFULIA KUPO LAKINI KUPATA PIA KUPO huwezi force chochote kila kitu hutokea
Mbona umemalisa ile maneno yote ya kwelyi mamayeyoo kila kitu imesema hii ndito ni kuweli kapisa ngoja nifae surpale nije.Takwenya
 
Mbona umemalisa ile maneno yote ya kwelyi mamayeyoo kila kitu imesema hii ndito ni kuweli kapisa ngoja nifae surpale nije.Takwenya

kwenu kuna ngombe

maana kwa vyovyote vile utaambiwa utoe

MI MASAI BWANA NASEMA MI MASAI TAMADUNI ILIOBAKI YENYE NGUVU AFRICA

r.i.p mr Ebo
 
tangia nianze mahusiano na huyu mtu hayajawah kuchuja wala kupungua makali hata siku moja utathan tuna wiki kumbe tuna miez kumi tayari, kila siku inakuwa zaidi ya jana. hili huwezekana tu kama wote mpo really.. hamdanganyan, i really enjoy the life

Mambo huwa yanaanza kubadilika baada ya miezi 2 hadi miaka 2; subiri itakukuta tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom