Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 3 na 4

winnie9999

Member
Nov 27, 2021
65
102
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE
MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS
SEHEMU: 3 $ 4
WhatsApp: 0746115688

Baada ya walinzi hao kuuliza hali ya bosi wao grace, grace aliwaambia yuko powa na hawana muda wa kupoteza inabidi waelekee mahali mzigo ulipo. Baada ya kusema hivyo grace akaingia kwenye gari pamoja na walinzi wake na safari yake ilianza na kwenda kukomea kwenye jumba moja kubwa la kifahali ambalo lina kila aina ya vitu ambavyo kila binadamu angetamani kuvipata. Grace alishuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo walinzi wake wakiwa nyuma yake mda wote.

Moja kwa moja grace alielekea kwenye chumba kilichokuwa maalumu kwaajili ya mziki na kuamuru walinzi wake wamletee mzigo wake , bila ya kuchelewa walinzi wake walimleta Jackbosi mbele yake na wale wazee wanne ambao Jackbosi aliwapuuzia awali walikuwa mbele yake na kutoa nywele bandai za mvi walizo kuwa wamevaa, jambo lililo mfanya Jackbosi ashangae sana na kuogopa lakini wakati yupo kwenye mshangao alishtushwa na sauti ya mtu aliemuita grace bosi jambo lililo mfanya akacheka sana na kumwambia grace kama huto jali nimiminie kinywaji, grace alimimina kinywaji na kumpatia Jackbosi kisha akawaamuru walinzi wote wa muache pamoja na Jackbosi kwani wanamazungumzo muhimu sana .

Walinzi wa grace Walitoka na baada ya Jackbosi kuona walinzi wote wamesha ondoka alisimama na kumpiga ngumi ya uso grace lakini grace hakuweza hata kutikisika kwa ngumi jiwe aliyo pokea kutoka kwa Jackbosi kwasababu mwili wake yeye ni sawa na chuma kwani unamazoezi ya kutosha na umeshazoea maumivu ya ngumi, Jackbosi baada ya kuona hata mkono wake tu nao umeshindwa kumpiga grace aliamua tu kumuuliza grace huku akiwa anatabasamu aliuliza ' wewe ninani Grace?

Grace alimwambia naitwa grace na hicho ndo kitu muhimu unacho paswa kujua kwasasa kwasababu ukijua hata kidogo kuhusu mimi nakuapia tuta kupoteza. Jackbosi alimwambia grace najua kunakitu unataka kutoka kwangu sijui ninini, lakini unapaswa kujua bila kuniambia wewe ninani siwezi kukwambia chochote. lakini grace alimwambia Jackbosi vip kama nikikwambia nataka wamama wote waliopo katika hospitali unayo miliki, pamoja na wale ulio waficha huku ukiendelea kumdanganya Mr.Kivuli ya kuwa umewaua ? Tafadhali Jackbosi kwa amani tu naomba unifanye mimi kuwa wewe ili niweze kuwasaidia watu wote ulio wahifadhi ukidanganya umewaua ili waweze kuishi maisha yao ya amani.

Jackbosi alimuangalia sana grace na kumuuliza ni kitu gani unajua zaidi ? Baada ya swali hilo kutoka kwa Jackbosi grace alimuuliza pia, 'unajua kwanini watoto wanaolelewa katika hospitali yako wakifika umri wa miaka ishirini wanapelekwa nnje ya nchi na wazazi wao wanachukuliwa na Mr.kivuli na huwaonagi tena mbele ya macho yako? Jackbosi hakuwa na jibu juu ya swali la grace ila grace alimwambia moja kwa moja ya kuwa wewe unahusika pia kwa kinacho tokea kwa watoto hao sema nakuhurumia kwasababu hujui chochote.

Jackbosi huwa hapendi kudharauliwa hivyo baada ya kuona grace anamwambia hajui chochote alimwambia wakinamama unao waona pale tuna wasaidia kukuza mimba zao na kuwapa watoto wao malezi bora na k kila wanacho hitaji pia watoto wao wanapofikisha umri wa miaka ishirini bosi wangu na baba yangu pia Mr. kuvuli anawatafutia nafasi za kwenda kusoma nchi za nnje na huko ndo wenyewe wanapotelea hivyo huna haja ya kunilaumu mimi wala bosi wangu kwani sisi huwa tunafanya kama Msaada kwani wazazi wao hawawezi kukizi mahitaji ya watoto wao.

Grace alicheka sana na kumwambia Jackbosi pole sana kwasababu ya kila kitu ulicho danganywa na kugeuzwa kuwa kama mtoto mdogo anaetii amri bila kujua watu wangapi mpaka sasa anawapoteza kwa kosa la yeye kutii amri zilizoleta madhara makubwa kwenye maisha ya watu wengi sanaa. Jackbosi alimuangalia sana grace lakini grace alimwambia watoto wote ambao ulikuwa ukiambiwa wanapelekwa nchi za nnje ni uongo mkubwa sana kwani kitendo chawewe kuwafuatiliaga viza, kuwakatia tiketi za ndege na kuwasindikiza airport unawapelekea vifo vyao karibu kama ulikuwa hujui basi mimi leo na kwambia watoto hao wanapotoka nnje ya Tanzania wanaenda kuwa marehemu na mama zao hugeuzwa Kuwa machizi tena wasio tibika. Jackbosi alimuangalia sana grace na kumuuliza 'grace unamaanisha nini wewe shetani ?

Grace alipata hasira baada ya Jackbosi kumuita shetani alikupasua glass yake ya kinywaji kwa mkono wake na kusababisha mkono wake kutokwa na damu sana lakini yeye alikuwa hajali na alichofanya ni kumshika mkono Jackbosi na kumwambia leo inabidi wewe ujifunze kitu kuwa mimi na wewe nani shetani na nani malaika. Moja kwa moja grace aliingia na Jackbosi katika chumba ambacho kilikuwa kimejaa wakina mama ambao wanaupungufu waakili na kila mmoja alikuwa amebeba mdoli mkononi akidai ni mwanae, Jackbosi alijikuta akimwaga machozi na kumuuliza grace 'hii inamaanisha nini' ? na hapo ndipo grace alimshika tena mkono Jackbosi na kumuingiza chumba ambacho kinamzee mmoja ambae umri wake umeenda sana hata kupumua kwenyewe ni shida kwake hivyo anatumia mashine kupumbua na mwili wake ulikuwa haufanyi kazi kabisa na jina lake mzee huyo lilikuwa Steven, Jackbosi alizidi kushangazwa sana na maneno ya grace lakini hakuwa na chakufanya zaidi ya kumuuliza tena na tena 'wewe ni nani grace' ? Na mbona unajua mambo mengi ya kutisha hivi?

Grace hakumjibu chochote Jackbosi ila alimuuliza 'kwanini kama bosi wako Mr.kivuli anafanya kazi ya kusaidia watu wenye shida bado anajificha wakati wachungaji, vituo vya yatima na watu wengine wote wanaotoa Msaada wote pamoja na vituo vyao tunaishi nao kwenye mwanga kwanini yeye yupo Gizani tu'? Jackbosi alimwambia grace kama huwezi kuwa muwazi bhasi niue au unitoe nnje ya nyumba yako kwasababu sijazoea methali na mafumbo. Grace akamwambia Jackbosi Mr.kivuli hawasaidii wamama unao waona katika eneo lile la hospitali bali wale wamama ndo wanao kufanya wewe pamoja na yeye muonekane watu wazuri na wenye pesa za kutosha . Wakinamama wote unao waona hapa ndani leo hii walidanganywa wametafutiwa kazi nchi za nnje pamoja na mawakala bandai wa Mr.kivuli na kuahidiwa mishahara mizuri ambayo kwa maisha magumu walio kuwa wanaishi wasinge weza kupata pesa kama hizo hata kama wangeamua kujitoa kufanya kazi usiku na mchana .

Mr.kuvuli alijifanya kuwa mwema kwao kwani kabla hajawachukua alikuwa akiwasaidia ndugu za wakinamama hawa kwenye mambo muhimu kama kuwapa fedha za upasuaji kwa wagonjwa walio nao, na ada za watoto wao kwa wenye watoto ambao wameshindwa kuwaendeleza na masomo kwasababu ya kushindwa kulipa ada, pia kuwapelekea magunia ya vyakula mbalimbali hali iliyo pelelekea wakina mama hawa kushawishika na misaada hiyo na kukubali kutafutiwa viza ili wakafanye kazi nnje ya nchi watengeneze pesa kama Mr.kivuli alivyowaambia . Lakini baada ya viza kukamilika kwakuwa Mr.kivuli tayari alikuwa amejenga uaminifu kwa nduguzao pamoja na wakinamama hawa, ndugu zao hawakuwa na wasiwasi walikabidhi ndugu zao kwa Mr.kivuli na kusaini mikataba ambayo ilimlinda yeye na kumfanya asiusishwe na kurudi au kutokurudi kwa wakina mama hawa.

Kilichofuata baada ya kuwachukua moja kwa moja aliwapeleka kwenye hospitali unayoiangalia wewe kwa sasa na kwakutumia madaktari wake ambao kwasasa wote nimesha waua aliwapandikiza wanawake hawa mbegu za wanaume wasio wajua na kwabahati nzuri au mbaya siku alipokuwa akiwapandikiza mbegu hizo wakinamama hawa mwanamama mmoja alikosa mbegu za kupandikizwa hivyo alimuomba mlinzi wake mmoja amsaidie kutoa mbegu halafu atampa pesa za kutosha, kwasababu mlinzi huyo alikuwa na shida alilizika na kutolewa mbegu kitendo ambacho kilimpelekea yeye kupoteza nguvu zake za kiume maishani mwake na mwanaume mwenyewe ndo mzee huyu unae muona anaitwa Steven,Jackbosi alishangaa sana,

Lakini grace alimwambia Jackbosi baada ya wakinamama hawa kupandikizwa mbegu aliwaambia cha umuhimu ni kuhakisha wanazaa watoto wakiwa salama na kwakuwa hakuna aliejua nini kitawatokea baada ya kujifungua wakinamama hawa hawakuwa na shida walilea mimba na kufanikiwa kupata watoto wao na kwabahati nzuri mwanamke aliyepandikizwa mbegu za Steven alifanikiwa kupata watoto wakike mapacha na mwanamke huyo alikuwa akiitwa Maria ambae aliwapenda sana wanae kuliko chochote na ukizingatia pia yeye alikuwa ndio mwanamke pekee anaemjua baba wa watoto wake.

Miaka mitano baada ya wakina mama hawa kupata watoto , sikumoja wakati Maria alipokuwa akipita ofisini alimsikia Mr.kivuli akipanga mipango ya kuwalea watoto wao mpaka watakapofikisha miaka ishirini kisha atawapeleka nchi Za nnje kuwatoa viungo vya ndani kama figo,ini,pamoja na moyo ilikuweza kuingiza mamilioni ya pesa.

Maria alichukia sana na kwabahati nzuri Steven Naye alimsikia Mr.kivuli pamoja na rafiki ake mmoja aliye kuwa mbunge wakipanga mipango mibaya juu ya watoto hao . Maria na Steven waliamua kuwatorosha watoto wao pamoja na yeye lakini maria hakuona ni busara kuondoka yeye na kuwaacha wanawake wenzie hivyo aliwapa siri ya kinachoendelea pale ili waweze kukubaliana nae na watoroke lakini mwanamke mmoja alieitwa Elizabeth alimuona maria ni muongo naana taka kupata vyeo nakuonekana mwema kwakila mtu hivyo aliwajaza wenzake ujinga na wote wakakataa kutoroka maria hakuwa na jinsi alimuomba Steven atafute usafiri saa tisa usiku wao watatoroka.

Steven aliandaa kila kitu na muda ambao maria alikuwa anatoroka walinzi hawakuwepo upande wa Getini hivyo alifanikiwa kutoka yeye pamoja na wanae salama kabisa lakini baada ya kuingia ndani ya gari maria alijisikia vibaya kuwaacha wenzie hivyo aliamua bora arudi tu ndani kuwaokoa wakina mama wengine au angalau hata mmoja lakini alipo ingia ndani wote walikataa na alipo kuwa akirudi Getini ili aondoke moja ya walinzi wa zamu siku hiyo alimuona na kumpigia risasi ya mguu kisha akafungiwa chumba cha adhabu na chumba chenyewe ni kile chumba cha siri ambacho wewe ulidai ni chumba cha kuhifadhi vifaa kitu ambacho sio kweli kwani chumba kile kilikuwa chumba cha adhabu na ulifichwa kwasababu usingekubali kusimamia hospitali ya baba yako feki , Jackbosi alibaki alimuangalia tu grace huku mate ya kimdondoka kama maji ya tiririkayo katika maporomoko ya milima ya usambala .

Grace aliendelea kwa kusema siku iliyo afuata ilikuwa ndio kiama cha maria kwani alitolewa mbele ya wenzie kwa lengo tu la yeye kupewa adhabu za kawaida na kuendelea kuishi hospitalini hapo hata kama watoto wake walitoroshwa, lakini Maria alimwambia Mr.kivuli unajisikiaje kuwadanganya wakinamama hawa kwakuwapa matumaini ya kuwalea watoto wao halafu baada ya hapo wewe na muheshimiwa mbunge mna wasafirisha nnje na kuwatoa viungo muhimu vya miili yao na kuwatupa kwenye bahari za ugenini wawe chakula cha mamba ?. Mr.kivuli alishtuka sana nakumuua palepale maria kwakumpiga risasi ya kichwa kisha akawaambia wakinamama kwakuwa mmeshajua kazi iliyo waleta hapa pambaneni muifanye yasiyo wahusu yasiwasumbue kabisa kwasababu mkifanya tofauti sio hao watoto wenu tu bali wote mtapotea.

Elizabeth alijisikia vibaya sana baada ya kujua maria alikuwa sahihi na toka siku hio amebakia kujilaumu kwa kifo cha maria na ndio maana mpaka sasa pamoja na kuwa amechanganyikiwa ila kila mara amekuwa akilia 'maria usife nisamehe na twende wote'. Jackbosi alishtuka sana na kumwambia grace ilikuaje wakinamama hawa wakatoroka na je watoto wamaria wako wapi ? Grace alimwambia Jackbosi baada ya kifo cha maria wanawake walijalibu sana kutoroka na watoto wao lakini kila walipo kamatwa waliuliwa mpaka wakabakia wakinamama hawa kumi ambao baada ya watoto wao kufikisha miaka ishirini Mr. Kivuli aliwachukua na kuwapeleka nnje ya nchi kisha akachukua video za watoto wao wakifanyiwa upasuaji mpaka wanapo kufa na bahari ambayo miili yao utupwa na kuliwa na Samaki kisha akawaonyesha wakinamama hao na baada ya kuwaonyesha video hiyo wakinamama wote walifanyiwa upasuaji nakuwekewa chip kichwani mwao ambazo zimewafanya kuwavichaa na kupoteza kumbukumbu kila dakika na endapo utahitaji kuondoa chip hizo kifo ndo matokeo na ndio maana mpaka leo hakuna aliye jalibu kutoa chip walizo nazo kichwani kwani ndo uhai wao, pia grace alimwambia wakina mama hawa walifika hapa kwa msaada wa Steve kwani Mr.kivuli baada ya kazi yake kuisha kwa wanawake hawa aliamuru usiku Wamanane wote wakatelekezwe barabarani na kwakuwa wana muda mrefu maisha yao yamekuwa ndani naukizingatia akili zao hazipo sawa itakuwa rahisi kwa wao kugongwa na magari na kufa kama Ajali.

Baada ya Steve kusikia mpango huo alimuomba Mr.kivuli ruhusa siku hiyo kisha akaenda kutega mahali ambapo wanawake hao wali mwagwa na baada ya walinzi wote kuondoka aliwachukua na kuwapeleka kwake na hapo ndo alianza kuishi nao nakuacha kufanya kazi rasmi na Mr.kivuli bila ya kumpa taarifa yeyote jambo lililo mfanya Steven kuchomwa sindano na Mr.kivuli miaka kumi baadae walipokutana nae katika soko la hisa kwenye kampuni kubwa ya usafirishaji ya GRAJA ambayo Steven ndo alikuwa mwenyekiti.

Jackbosi alimuuliza grace vipi mbona huja niambia kuhusu watoto wa maria ? , grace akamwambia Jackbosi usiku ule watoto wa maria walifanikiwa kutoroshwa na hao ndio watoto pekee ambao tokea hospitali ile kuanzishwa wako hai japo walitenganishwa kwani walipo kuwa na miaka kumi na miwili Mke wa Mr. Kivuli alienda kumtembelea Steve hospitalini nakujua watoto wake wote ni wagonjwa sana na malipo ya hospitalini yalikuwa makubwa kuliko uwezo wake hivyo mke wa Mr. Kivuli aliahidi kumsaidia Steven watoto wake ila kama atakubali kumkabidhi mtoto wake mmoja yeye amchukue na kumfanya binti yake yeye, ilikuwa ngumu mwanzoni kwa Steven kufanya hivyo lakini baada ya hali ya wanae kuwa Mbaya siku hadi siku alikubali sharti la mke wa Mr. kivuli kwani ilikuokoa maisha ya watoto wake wote wawili ilimbidi mmoja amtoe kwa hao mashetani wawili na kwabahati nzuri Mr. kivuli hakukataa kabisa alikubaliana na Wazo la mkewe kwani alijua kabisa kuishi na mtoto huyo itamsaidia kwani Steven hataweza kutoboa siri za biashara zake huko baadae ikitokea wamegombana kwani ndio njia pekee ya kumlinda mwanae na ndio maana hata Steven alipo wachukua wakinamama na kuacha kazi haku mshitaki popote Mr. Kivuli kwasababu ya mwanae na kwabahati nzuri mke wa Mr. Kivuli na Mr.kivuli walimpenda sana mtoto huyo naukizingatia walikuja kugundua hawawezi kupata mtoto na kwataratibu hivi sasa mtoto huyo wanaanza kumrithisha uchafu wao jambo ambalo siwezi kukubali kwani yeye hana damu chafu kama wao na ndio maana leo nakuomba unipe nafasi yako na wewe uchukue nafasi yangu.

Jackbosi alisimama huku akiwa Ametoa macho na kumuuliza grace unamaanisha nini ? Grace kwasauti akamwambia mimi ni grace Steven na wewe ndio Jack Steven hilo jina la Jackbosi wamekupa wao na maanisha wewe ni mdogo angu mimi na huyu mzee aliye lala hapo ni baba yako na wale mashetani walio kulea ndio walio muua mama yako na kumfanya baba yako kilema na kuonekana mzee sana kwa sababu ya maradhi na kuharibu maisha yawakinamama kibao na kusababisha vijana kibao kuzaliwa , kukua vizuri na kupewa kila kitu halafu mwisho wa siku wanauliwa ugenini na kuwa chakula cha samaki.

USIKOSE SEHEMU YA 5 & 6 KESHO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom