Tamthiliya: Challenge Made - Sehemu ya 1

TAMTHILIA: CHALLENGE MADE.

MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.

SEHEMU: 9 $ 10

WhatsApp no : 0746115688.

Mr.kivuli alishangazwa sana na kitendo cha jasmini kumshika mkono lakini jasmini alipoona Mr.kivuli anaonekana kuwa na hasira japo anajitahidi kufichaficha jasmini aliangua kicheko na kumwambia Mr.kivuli samahani ila ni kwausalama wa mtoto lazima unawe kabla ya kumshika hiyo itasaidia akue bila maambukizi ya aina yeyote. Mr.kivuli alicheka sana na kila mtu aliyekuwa pale pia alicheka na hapohapo Mr.kivuli hasira zilimpotea na kuchukulia kama tabia ya jasmini inatokana na upendo wake kwa mtoto wake, hivyo aliachana na mtoto wa grace nakuwaomba wakinamama wote wapumzike tu, kwani yeye anamizunguko yake ndani ya hospitali . Basi wakinamama walibakia wote hodini lakini grace wakati walinzi wakihangaika na msafara wa Mr.kivuli yeye alitoroka na pikipiki ya kununulia mahitaji muhimu akaelekea kwenye kampuni yake ya usafirishaji ya Graja kwani alipigwa simu na kujulishwa kuna proposal mpya ya kibiashara kutoka katika kampuni ya Culture.
upande wa pili Mr.kivuli alitembea na james hospitali nzima na kisha james alichagua chumba kitakacho mtoshea yeye kufanya mambo yake na baada ya hapo Mr.kivuli alielekea ofisini akiwa yeye, Jackbosi pamoja na james lakini baada ya wote kukaa Mr.kivuli alimuomba Jackbosi akaendelee nashughuli zake za kila siku kwani alikuwa na mazungumzo ya kibinafsi na james. Jackbosi aliondoka lakini kumbe alikuwa ametegesha kamera kwani safari hii hakutaka kuonekana mjinga tena hivyo wakati kikao kinaendelea na yeye aliingia katika chumba ambacho kilikuwa hakina mtu nakuanza kuangalia na kusikiliza kila kilicho kuwa kinaongelewa na Mr.kivuli pamoja na james lakini ghafla wakati Jackbosi anasikiliza maongezi ya Mr.kivuli na james aliweka simu yake mfukoni nakukimbia moja kwa moja katika chumba cha wakina mama bila kugonga hodi aliusukuma mlango na kuwauliza grace yupo wapi, Ade akamwambia kuna kazi muhimu ameenda kuifanya kwenye kampuni , Jackbosi akawaambia hakikisheni wote mnaandaa vitu vyenu vya umuhimu leo usiku mnatoka hapa na hakuna yeyote anapaswa kukataa juu ya jambo hili kisha akamchukua Ade pamoja na mwenzie mmoja nakuwapa kazi ya kufungua tank za pikipiki zote na kuchukua mafuta kisha kuyaweka kwenye makopo aliyo wapa kwani yata wasaidia wakati wa kutoka hapo. baada ya Jackbosi kuwapa maelezo hayo alitoka na kwenda kukaa katika ofisi ya madaktari na muda haukupita mlinzi alimfuata na kumtaarifu kuwa baba yake alikuwa anamuita hivyo Jackbosi alielekea baba yake alipo na baba yake alimtaarifu kuwa kuanzia kesho James atakuja kuanza kazi yake hapa pamoja na wafanyakazi wake. Jackbosi alimwambia baba yake sawa lakini moyoni mwake aliweka kiapo kwamba ikifika kesho hospitali itakuwa imekwisha sahaulika. lakini kwa upande wa james alimwambia kinafki Jackbosi amsamehe kwakumkosea siku ya part kwani kuanzia sasa watakuwa wakionana mara nyingi. Jackbosi alicheka sana na kumwambia usijali tupo pamoja ni jambo dogo sana lililotokea Siku ile mbona mimi nilikusamehe hofu kwako tu. Mr.kuvuli yeye aliona kawaida kwa vijana kuongea maneno kama hayo hivyo alimwambia tu binti yake kafanya jambo zuri kumsamehe mapema james ukizingatia wao James ni mshirika mwenzao kwasasa. baada ya Mr.kivuli kuongea maneno hayo alimwambia James waondoke wakaendelee na majukumu mengine lakini pia akamwambia binti yake chukua likizo kuanzia kesho mama yako amekukumbuka sana . Jackbosi alionekana mwenye furaha sana nakumshukuru baba yake kwa kumpa likizo, lakini Baada tu ya Mr.kivuli kuondoka Jackbosi alijalibu kuwasiliana sana na grace lakini hakukuwa na majibu yeyote kwani grace alikuwa hapokei simu . Lakini kumbe grace nae alisahau kifaachake anachotumia kuwasiliana na watu kwenye droo yake ya mafaili ofisini kwake alipo kuwa akijiandaa kuelekea kwenye kikao kilichokuwa kinafanyika ili kutoa maamuzi kama kampuni yao itashirikiana na Culture company au haitakuwa tayari.
Maamuzi ya grace alikubaliana na kusaini makubaliano hayo lakini kama Mr.kivuli mwenyewe ataonyesha kujali na kuja mwenyewe kusaini makubaliano hayo ofisini kwake lakini kama hatakuwa tayari makubaliano hayata fanyika.
wawakilishi wa kampuni ya Culture waliona kama vile grace anadharau sana lakini grace hakuwa tayari kubadili sharti hilo na aliwapa masaa mawili wawe wamesha wasiliana na bosi wao nakutoa jibu kama bosi wao yuko tayari au la. kisha yeye akarudi ofisini kwake na kuendelea kupitia kazi mbalimbali hasahasa ambazo hazikupitia mikononi mwake .
Wawakilishi wa kampuni ya Culture walikuwa wakimpigia sana mwenyekiti wa kampuni ya Culture ambaye ni Mr.kivuli lakini kwabahati mbaya Mr.kivuli alikuwa ameacha simu yake ndani ya gari hivyo ilikuwa ngumu sana kuwasiliana nae kwa njia ya simu hivyo walikubaliana muwamkilishi mmoja aende kwenye kampuni kwani walikubaliana na Mr.kivuli baada ya makubaliano hayo watakutana nae kwenye ukumbi wa mikutano wa kampuni ya Culture .
Upande wa pili Jackbosi aliendelea na mipango yake ya kuhakikisha ana watorosha wakina mama wote usiku.
Baada ya lisaa limoja grace alirudi katika chumba cha mkutano wa makubaliano na kuwauliza kama wawakilishi wa kampuni ya Culture wamesha wasiliana na bosi wao lakini kwa bahati mbaya hawakuwa na jibu hivyo grace alisimama nakuwaambia makubaliano hayatakuwepo tena muda umeisha , lakini kabla
grace hajatoka nnje ya chumba cha makubaliano simu ya muwakilishi kutoka kampuni ya Culture iliita na muwakilishi huyo aliweka loud speaker kwani bosi wao Mr.kivuli alipiga na moja kwa moja Mr.kivuli alimwambia grace kesho ntakuja mimi mwenyewe kusaini mkataba , grace bila hata ya kuogopa alimwambia Mr.kivuli saa 3:00 asubuhi na usisahau naenda na muda. Mr.kivuli alikubaliana nae japo alipatwa na hasira sana kwani kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na mtu wakumdharau , Siku zote watu wamekuwa wakimuheshimu lakini grace hakujali. Baada ya mkutano grace alielekea nyumbani kwao ili kuweza kuangalia hali ya baba yake pamoja na wakinamama wote walio kuwa wanaishi katika nyumba yao , wakati huo Jackbosi nae aliendelea kumtafuta grace mara kwa mara lakini grace hakuwa na kifaa cha mawasiliano.Jackbosi alifanya maamuzi ya kuendelea kupanga mipango yake ya kuwatoa wa kinamama wote hospitalini .
Mida ya saa mbili usiku Jackbosi alimuita mlinzi wake na kumwambia kaangalie wakinamama kama wapo. mlinzi alienda na aliporudi alimpa jibu kuwa wakinamama wote wapo, grace akamwambia chukua kufuli hili kawafungie muda huu utawafungulia asubuhi kisha Jackbosi akampa mlinzi ufunguo moja na yeye akachukua mmoja, mlinzi akaenda kuwafungia wakinamama kisha Jackbosi akamruhusu aende tu nnje kuendelea na shughuli nyingine . Mlinzi alipo tòka tu Jackbosi alielekea kwa wakinamama na kuwatoa wote kisha akaufunga mlango kama alivyo ufunga mlinzi wake na baada ya hapo akawatoa wakinamama wote nnje kupitia njia ya siri na kuwaingiza kwenye gari iliyo kuwa ikiwangojea upande huo. kisha akamchukua ade na mmama mmoja wakasaidiana kumwaga mafuta hospitali nzima na baada ya hapo akawaambia wakimbie na wala wasijali kuhusu yeye kwani atakuwa salama . Baada tu ya wakinamama kuondoka na gari iliyowabeba kutoka maeneo ya hospitalini Jackbosi alitupa njiti ya kibiriti ndani ya hospitali na kisha moto ukaanza Kuwaka walinzi na madaktari wote walikimbia kwani moto ulianza kwa kasi sana lakini Jackbosi yeye alitoka nnje ya geti la hospitalini na kunywa vidonge vilivyo mfanya azimie . Moja kati ya walinzi alimpigia Mr.kivuli na kumpa taarifa juu ya kilicho tokea lakini Mr.kivuli alimuuliza mlinzi huyo kuhusu Jackbosi na hapo ndipo mlinzi alipo mpa taarifa Mr.kivuli ya kuwa sikumuona wakati moto ulivyo anza lakini nakumbuka alikuwepo ndani ya hospitali , anaweza kuwa karibu ya hospitalini tu , kwani sisi tuliondoka kabisa eneo lile tupo njiani kuelekea kwenye kampuni kama ulivyotuambiaga .
mke wa Mr.kivuli aliposikia hayo alishindwa kuendelea kusubiri mipango ya mumewe alichukua gari nakuanza safari ya kuelekea hospitalini kumfuata binti yake wakati alipokuwa akiendelea kutafuta alipofika eneo la hospitalini alimuona Jackbosi akiwa amezimia na haraka alimchukua mwanae na kumkimbiza hospitalini kwani hakuwa amesaidika ukizingatia hospitali ilikuwa nnje kabisa ya Mji hakukuwa na watu wakuwasaidia baada ya janga hilo kuwakuta .
walipofika hospitalini Daktari alimwambia Mrs.kivuli binti yako yuko sawa japo anahitaji muda wa kupumzika kwani anaonekana amevuta hewa chafu ya kutosha atakuwa sawa anahitaji kupumzika tu.
wakati grace alipokuwa anataka kurudi hospitalini ghafla aliona kosta ikisimama nnje ya nyumba yake na alipofika nnje ili ajue nini kinaendelea alishangaa kuona ni wakinamama wote wamerudi, grace aliogopa sana na alipo jalibu kushika kifaa chake cha mawasiliano masikioni ili awasiliane na Jackbosi aligundua kifaa hicho hakipo na hapo ndo ilimbidi awe mpole na kuwasaidia wakinamama wengine kushuka kwenye gari hasahasa wale waliozaa kwa upasuaji.
kisha wote grace akawapa vyumba na baada ya hapo akamchukua mtoto wake pamoja na jasmini akawaingiza kwenye chumba chake kisha akawaambia wakinamama wote wapumzike tu watapewa kila wanacho kihitaji na asubuhi wataongea mambo mengi zaidi .
grace aliingia kwa jasmini akamuuliza ' imekuwaje' ?. lakini jasmini alimwambia ghafla Jackbosi alikuja akikutafuta mno naalipo ona hupatikani alituambia tujiandae anatutoa pale hospitalini leo na hospitali nayo mwisho wake ni leo tulihisi kama utani lakini kweli ilipofika saambili Jackbosi alikuja na kututoa wote kisha akawasha jengo la hospitali moto na nahisi mpaka sasa jengo la hospitali litakuwa limesha teketea kabisa.
grace hakuamini anachoambiwa hivyo alichukua pikipiki nakwenda kuhakikisha alichoambiwa ni kweli au kuna uongo ndani yake, lakini alipo fika eneo la hospitalini alikutana na majivu tu, grace alichukia sana na kuchukulia maamuzi ya Jackbosi ni ya kipumbavu sana na kuanzia hapo hakutaka kuwasiliana nae na akaamua kupanga mipango yake ya kumteketeza Mr.kivuli kwa muda wa mwezi .
wiki moja baadae Jackbosi alienda kumtembelea grace kwani alikuwa hampati kwenye simu lakini alipoingia ndani grace na Wakinamama wote walionekana kumchukia sana kwani waliisi yeye amewatoa pale ili wasimmalize baba yake hivyo kila alivyojalibu kuwaonyesha upendo wao walirejesha maneno ya chuki. Jackbosi alipoona amna mwenye furaha na yeye aliamua kuondoka lakini aliacha CD akawaambia kama wakipenda wanaweza kuangalia ni nzuri.
Baada tu ya Jackbosi kuondoka Ade alichukua CD na kuweka katika deki, lakini kabla haijaanza kuplay wakinamama wengine wote pamoja na grace walisimama ili kuondoka eneo lile. lakini Ade alikaa pale pale na kabla grace na wakina mama kuondoka kabisa eneolile Cd ilianza kuonyesha, Jackbosi alikuwa amefuatilia kila biashara za baba yake chafu ambazo walikuwa hawazijui na wanazo zijua kisha akachukua video kila mahali ambapo makontena ya baba yake yapo na ulinzi uliokuwepo lakini mwishoni aliweka kipande cha mkutano wa baba yake na james ambao huo ndo ulisababisha yeye kuwatorosha wakinamama na kuchoma hospitali, na walipo angalia waligundua mpango wa james na Mr.kivuli ulikuwa baada ya kikao kile siku inayafuata james aamie pale, kisha usiku wa siku hiyo saa tisa wakati wakinamama wote wamelala yeye atafanya majalibio ya madawa yake kwenye miili yao ili aweze kuona kama madawa hayo yanauwezo wa kumfanya mtu asiache madawa tena maishani anapo dungwa siku ya kwanza tu, na kama yataleta matokeo mazuri watoto wote wata chukulia nakulelewa palepale kwani wakinamama wote hawatajali tena watoto wao zaidi ya madawa na kisha watoto wasingepelekwa tena nchi za nnje bali wangefundishwa kuwa watumiaji na wasambazaji wazuri ambao hawajawahi kutokea nchini. Lakini pia mama zao wangeishia kuwa wajalibishwaji wa madawa hayo maisha yao yote kwani madawa hayo yana nguvu sana unapoanza kutumia huwezi kuacha mpaka unakufa .
lakini pia mpango mwingine ulikuwa kumtoa Jackbosi katika hospitali ile ili asiingilie chochote na ndio maana baba yake alimwambia achukue likizo mama yake amemkumbuka sana.
mwishoni kabisa Jackbosi alionekana akicheka sana na kuwaambia nakuja kuwa grace hivi karibuni, kwasasa grace karibu kuwa Jackbosi mipango ianze ndani ya wiki nnaimani hakutakuwa na Mr.kivuli tena kwani taarifa zake muhimu ndo izooo na peke yako huwezi, peke yangu siwezi ila pamoja tunaweza. byeeeee.
USIKOSE SEHEMU YA 11 $ 12.
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE.

MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

SEHEMU: 11 $ 12.

WHATSAPP NO: 0746115688 .

Baada tu ya grace pamoja na wakinamama kumalizia kuangalia video ya Jackbosi, wote walijisikia vibaya na kujiona wao sio marafiki wa kweli kwasababu sikuzote kabla ya kufikilia mara mbili wamekuwa wakitoa hukumu, lakini maumivu yalikuwa mara mbili kwa upande wa grace kwani alishindwa kumuamini mdogo wake japo alionyesha kuwa na yeye tangu alipoujua ukweli kumuhusu. Jackbosi alipofika nyumbani alipita moja kwa moja kwenda chumbani kwake na kuanza kulia alikuwa akikumbuka mapokezi aliyokutana nayo kwa grace na kujihisi kuwa mtu asie na mana. Lakini mama yake Mrs.kivuli alipoingia ndani na kumkuta binti yake analia alijisikia vibaya na yeye kwani yeye maishani mwake alisha mpokea Jackbosi kama binti yake wa kumzaa kabisa hivyo alimuuliza ' Jackbosi shida ninini mwanangu ulitoka ukiwa Mzima kabisa lakini umerudi unalia ' . Jackbosi alimwambia ' najisikia vibaya tu kuona rafiki angu anaweza kuhisu kuwa mimi naweza kumsaliti' . Mrs.kivuli bila hata kuwaza mara mbili, moja kwa moja alifurahi sana alihisi binti yake kwasasa yupo kwenye mahusiano hivyo ategemee Jackbosi kuolewa siku sio nyingi. Kwa furaha alimkumbatia na kumwambia ' usijali binti yangu wakati mwingine watu wetu wakaribu huwa hivyo hasa wanapohisi tuna wasaliti lakini usiwe na wasiwasi kabisa kwani watu wetu haohao wanapogundua hawakuwa sahihi hurudi kwetu na kutuomba msamaha kisha maisha yanaendelea '. Jackbosi alifurahi sana kusikia hivyo na alipata matumaini kuwa grace pamoja na wakinamama wakiangalia tu video ile watamuelewa na kumuomba msamaha pia. hivyo alifurahi sana na kuachia kicheko kwanguvu sana kwa furaha. mama yake alifurahi sana na kumwambia Jackbosi ' usichelewe kunitambulisha kwa huyo rafiki yako ' na Jackbosi akamjibu usijali mama hivi karibuni tu utakutana nae.
wakati wako pale grace na mama yake Mr.kivuli alikuwa amerudi nyumbani nakuwaulizia wako wapi na alipoambiawa wako chumbani kwa Jackbosi Mr.kivuli alielekea moja kwa moja chumbani huko na kumwambia bintie na mkewe ya kuwa yeye ameingia kwenye siasa rasmi na amejaza fomu ya kugombea nafasi ya ubunge . Mrs.kivuli alifurahi sana lakini Jackbosi alionekana kutokuwa na furaha kabisa kwani alijua Mr.kivuli akifanikiwa tu upande wasiasa na kuwa kiongozi hawatafanikiwa katika mipango yao ya kumuangusha kwani atakuwa na nguvu sana kushinda hata sasa na atazidi kuwa shetani .
Mrs.kivuli aliwaambia Mr.kivuli na Jackbosi leo tutoke wote tukafurahie habari hii njema kwenye hoteli moja kubwa yenye manyota yake ya kutosha na mimi ndo nitalipa. lakini Mr.kivuli aliomba yeye alipe lakini mwisho Jackbosi pia aliwaambia naomba mimi ndo nilipe kwasababu nimekuwa ni kitumia kila siku pesa zenu angalau leo na nyie tumieni ya kwangu . Mr na Mrs.kivuli walicheka sana na kumkumbatia kwa furaha kumuonyesha Jackbosi kuwa wameridhika na ofa yake.
Grace nae alijalibu sana kumpigia Jackbosi ili amuombe msamaha lakini Jackbosi alishindwa kupokea simu kwani ilikuwa ndani ya pochi na pochi yeye aliiacha chumbani kwake kwani alitoka na pochi nyingine .
Walipofika hotelini wote walifurahia sana chakula na kisha wakarudi nyumbani. lakini Jackbosi aliporudi nyumbani alimkumbuka grace hivyo alitafuta simu yake ili ampigie, lakini alipo ipata tu alikuta grace amempigia mara nyingi sana na alipo taka kumpigia grace, grace alipiga kabla yake na kumuomba Jackbosi amsamehe lakini Jackbosi alimwambia usijali ndugu hawaombani msamaha bali wanakumbatiana kwa furaha na kuombeana mema maishani . Grace alifurahi sana kuona Jackbosi amemsamehe lakini pia Jackbosi palepale bila kupoteza muda akampa taarifa mbaya ya Mr.kivuli kuingia rasmi kwenye siasa kama mgombea ubunge .
Grace alimwambia Jackbosi inabidi umshawishi wewe kuwa mmoja wapo wa wapambe wake pia katika kampeni zake. Jackbosi alimwambia grace 'sawa usijali', na Kweli Jackbosi alionyesha kuwa na nia ya dhati ya kumuunga mkono baba yake katika siasa na kweli alifaanikiwa alichotaka kwani baba yake alimwambia inabidi asaidiane na watu wengine katika kupanga ni jinsi gani anaweza kufanya kampeni na kushinda kwani siku za mbeleni anaimani Jackbosi pia atagombea. Jackbosi alimwambia grace kila kitu na grace alimwambia Jackbosi, 'namjua baba yako vizuri kwasasa atakuwa anajalibu sana kutafuta njia ya kuweza kushinda kinyume cha sheria lakini mimi sitaruhusu hilo kwani ntatumia huohuo uchafu wake kumuharibia' .
Jackbosi alifurahi sana kusikia hayo siku zilienda na Mr.kivuli akafanya kampeni za kutosha huku akiwa na familia yake nzima yaaan Jackbosi na mkewe, lakini nyuma yao alikuwa akiwahonga viongozi mbalimbali wa uchaguzi pamoja na wasimamizi mbalimbali wa vituo vya kura ili tu yeye aweze kupata nafasi hiyo ili iweze kumsaidia katika biashara zake.
lakini kumbe kila hatua chafu aliyo kuwa anaipitia grace alikuwa anamfuatilia na kumrekodi kila kitu kwa kutumia kamera. kisha baadae akaunganisha matukio yote sehemu moja ya jinsi Mr.kivuli anavyo tumia njia za ajabu ili kupata kura siku ya uchaguzi na Siku moja kabla ya uchaguzi grace alifungua akaunti mbili mpya na kuachia video hiyo iliyo kuwa ikionyesha rushwa zilivyo mwagwa na Mr.kivuli ili tu apate nafasi ya ubunge .
Mr kivuli alichanganyikiwa sana na baada ya kuona video hizo alijalibu kuhitaji kujua nani muhusika wa akaunti zote zilizo tuma video hiyo na hapo ndo aligundua muhusika wa hayo yote aligundua watamtafua hivyo alifungua akaunti mbili za mtu asie julikana lakini pia akatumia akaunti za wanafamilia wote wa Mr.kivuli jambo lililo mfanya akosejibu nani muhusika wa mambo yote . Asubuhi na mapema Mr.kivuli pamoja na mkewe na Jackbosi walijiandaa kuelekea kituo cha kupiga kura, lakini Mrs.kivuli alichukizwa sana na tabia ya mumewe kwani alijalibu kufanya mambo yake mwenyewe bila ya kumshirikisha na moja kwa moja alihisi mumewe hakumuamini ndio maana alifanya mambo hayo kimya kimya. Hatimaye familia nzima ya Mr.kivuli ilifika katika kituo cha karibu na nyumbani kwao kwenda kupiga kura lakini kabla ya familia ya Mr.kivuli kupiga kura waandishi wa habari wali wazunguuka na kuwauliza mambo mengi yanayo onekana kwenye video ile iliyosambaa mtandaoni lakini Mr.kivuli alijiliza kinafki huku akisema kasingiziwa Jackbosi alichukizwa san na maelezo ya baba yake ya kuwa kasingiziwa kila kitu kwani yeye alijua wazi kabisa kuwa baba yake amefanya kweli yote yaliyo tokea lakini hakuna jinsi kwani hata yeye alipohojiwa ilibidi amtetee baba yake kwa kuwaambia waandishi kuwa lawama zote juu ya baba yake nizauongo tu , ukweli baba yake ni mtu mwema sana na baba Bora. Kisha familia nzima wakachukua vikaratasi vya kupigia kura na baada ya kujaza, walipo kuwa kwenye mstari kuelekea kukusanya kura kwenye sanduku la kupigia kura ghafla wananchi walianza kumpiga na mayai Mr.kivuli na wakati ana kwepakwepa mayai hayo na uchafu aliokuwa anatupiwa aliona sura za wanawake waliokuwepo katika hospitali yake na hapo ndo akazidi kuchanganyikiwa zaidi na kuogopa sana . Walinzi wa Mr.kivuli waliwaondoa Mr.kivuli pamoja na familia yake eneo la tukio baada ya wao kuweka kura zao kwenye sanduku na kuwarudisha nyumbani.
waliporudi nyumbani kila mmoja aliketi kwenye kochi lake akiwa na huzuni lakini Mr.kivuli haikuwa huzuni tu bali kila alipo kumbuka alivyo zalilishwa na kuona sura za wakinamama wale alijisikia hasira sana na kuanza kutupatupa vitu kisha akaamua kuwasha TV lakini alipo washa tu tukio lake yeye kupigwa mayai na raia lilikuwa likionyeshwa kila chaneli, kwa hasira akatupilia mbali TV na kusema nani wewe unae sogelea kifo chako kwa kasi. Mrs.kivuli alimwambia Jackbosi aingie ndani kwani aliona baba yake kashaaza kuongea maneno ya kutisha ambayo hakuwahi yaongea mbele ya Jackbosi. Hata hivyo mama yake aliamini Jackbosi bado hajajua kazi chafu za baba yake. Mr.kivuli alipokuwa akiendelea kufanya Fujo alijiumiza mkono wake kwani vitu vingine alivyo kuwa akitupa vilikuwa ni vya chupa . Hivyo Mrs.kivuli alimuomba mumewe akae kwenye kochi huku yeye akiendelea kumfunga kidonda, Mrs.kivuli akamwambia mumewe usipo kuwa makini na hasira kiukwel tu zita kuharibia kwani watu wakikuona katika hali hiyo hawatakuwa najinsi yeyote ya wao kupinga kuwa hauusiki na mambo yote yaliyo vuja mtandaoni lakini ukiwa mpole mambo yatakuwa sawa .
Baada tu ya Mrs.kivuli kumfunga mumewe Askari wa kuzuia rushwa na wapelelezi walifika nyumbani kwa Mr.kivuli huku wakiwa na kibali cha kumkamata Mr.kivuli. Mr.kuvuli alichukia sana akili yake yote ilijua wahusika ni wale wakina mana lakini hakuweza kufanya chochote kwani hakuwa anajua hata wakinamama hao wanakaa wapi. Mr.kuvuli alichukuliwa na kupelekwa katika mahojiano na alipoona mambo ni magumu sana alijifanya kama amechanganyikiwa hivi, hivyo askari waliona bora familia yake ikae nae kwanza mpaka akili yake iwe sawa. Mr.kivuli alipofika nyumbani alikuwa sawa kabisa na kwabahati mbaya matokeo yalitoka na alikuwa ameshindwa lakini bado Mr.kivuli alifurahi sana baada ya kusikia anakura tatu tu! kwani aliamini pamoja na yote familia yake inamjali lakini hakukuwa na ukweli wowote kwani Jackbosi hakuwa amempigia yeye kura bali wapinzani wake na baada ya Jackbosi kusikia Mr.kivuli anakura tatu alichukia sana kwani aliamini kunabaadhi ya watu ni wasaliti tu kwani hata baada ya kujua ukweli kuhusu baba yake bado mtu akampigia kura. lakini kumbe haikuwa hivyo kwani grace ndio alikuwa amepiga kura hiyo ilikuhakikisha Mr.kivuli hawezi kumuhisi vibaya Jackbosi ikitokea raia wote wameshindwa kumpigia kura akute tatu ili aone familia yake bado ina muunga mkono .
Mr.kuvuli alitafuta wanashera wazuri nchini ili waweze kumsaidia katika kesi yake na kweli alifanikiwa kwani aliwapata wanasheria walio bora kabisa lakini pia hawakuwa msaada kwake kabisa kwani walichomsaidia ni kuhakikisha hafungwi, lakini faini alilipa kwani ushahidi ulikuwa na nguvu sana hivyo hakuweza kukwepa ilimbidi alipe milioni 50 kama faini ya uchafu wake, na bado aliwalipa wanasheria walio msaidia angalau akapata nafasi ya kulipa faini tu bila kwenda jela .
Wakati Mr.kivuli anarudi nyumbani kwake baada ya kesi familia yake ilimpokea kwafuraha kwa kummwagia pombe za bei ghali, jambo lililomfanya yeye afurahi sana, lakini palepale alipokuwa kasimama simu yake iliita na mwenyekiti wa kampuni ya usafirishaji ya Graja ambae ni grace alimpigia simu na kumwambia kesho inabidi tukutane tujuane na tupange mipango ya kazi kwani toka mr.kivuli aliposaini mkataba wa kazi na mfanyakazi wa grace hajawahi kuiona kabisa sura ya grace ambae ndo mmiliki wa kampuni hiyo ya usafirishaji ya Graja kwasasa baada ya baba yake kupata maradhi .
Mr. kivuli aliamini ni baraka hivyo aliipa taarifa hiyo familia yake na kucheza kwafuraha lakini Jackbosi alicheza pamoja na baba yake kwani alijua kabisa hata siku ya kesho kwa upande wa baba yake itakuwa mbaya pengine zaidi ya kesi yake iliyoisha.
Siku iliyofuata asubuhi mida ya saa mbili Mr kivuli alielekea katika kampuni ya Graja pamoja na bintie baada ya kujua mmiliki ni wakike ilikumvutia kufanya kazi nae na walipofika secretary aliwapeleka ofisini kwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ambae ni grace kisha akampa taarifa mwenyekiti wa kampuni ya culture amefika. grace vilevile akiwa amegeuka pembeni alimwambia Mr.kivuli karibu sana na pole kwa majanga kisha akugeuka na kumwambia Mr.kivuli karibu tena sana mimi naitwa grace Steven . lakini Mr.kivuli alibakia kaduaa tu bila kujibu chochote macho yote juu ya grace na bintie Jackbosi .
USIKOSE SEHEMU YA 13 $ 14
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE.

MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.

SEHEMU: 13 $ 14.

WHATSAPP No: 0746115688.

Mr.kivuli alimshangaa sana grace lakini Jackbosi alijifanya ndo aelewi kabisa kwani alisimama na kumwambia baba yake ' hivi kwani baba mimi nina pacha , Mana sikumbuki kama mlisha wahi kuniambia hilo na nikimuangalia huyu mwenyekiti wa kampuni ya Graja najiona mimi kabisa bila kupinga . grace nae alimshangaa sana jackbosi kama vile hakuwahi kukutana naye kabla.
Wakati wawili hao wakishangaana kinafki Mr.kivuli alicheka sana na kuwaambia kweli duniani watu wawiliwawili, kisha akamwambia grace tunaweza kuendelea na kikao mana kama sikosei wewe ni mtu unae jali muda sana. Grace alimwambia sawa tunaweza kuendelea japo binti yako anaonekana bado yupo kwenye mshangao mkubwa sana . Mr.kivuli alimwambia Jackbosi azingatie mkutano kwanza mambo mengine wataongea watakaporudi nyumbani. Bhasi Mr.kivuli akaingia mkataba mwingine na grace wenye lengo la kulinda mkataba wao wa awali kwani mkataba huo ulikuwa ukisema yeyote atakae taka kuuvunja mkataba, au kujalibu kuhujumu mali yeyote ya mshirika mwenzie atamlipa mwenzie fidia ya shillingi milioni miamoja. Baada ya mkutano huo grace alimwambia Mr.kivuli sasa inabidi twende nikakutambulishe kwa wafanyakazi wangu wakubwa wanao husika na usafirishaji ambao nimewaajili hivi karibuni ila kazi yao ni nzuri kwani mzigo wako ukiongozwa na wao kuwa naamani maana utafika sehemu salama na huta wahi kuiwazia hasara shida walipwe vizuri .
Mr.kivuli alikuwa na shauku ya kuwaona wafanyakazi hao kwani yeye lengo la kujiunga na kampuni ya usafirishaji ya Graja ni kuweza kusafirisha kwa urahisi madawa yake kwani graja ni kampuni inayoaminika sana kwa usafirishaji na serikari haiwezi kuitilia mashaka yeyote kuhusu kujihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya kwasababu ni kampuni ya miaka sana na haijawahi kukutana na kashfa ya usafirishaji wa madawa au mizigo yeyote haramu hivyo ni ngumu kutiliwa mashaka na ukizingatia inawafanyakazi wazuri ambao pengine angekuwa nao asinge saini mkataba nao angejitegemea mwenyewe . Mr kivuli , Jackbosi pamoja na grace walifika nakuingia mahali ambapo wafanyakazi hao wapo. Lakini cha kushangaa hawakujali kuwa kuna mtu ameenda kuwatembelea anafanana na bosi wao au la walicho jali wao ni kuendelea na kazi tu , kitendo ambacho kilimfanya Mr.kivuli awaone wao ni wafanyakazi wazuri kushinda hata wafanyakazi wengine aliokwisha wahi kuwaona.
grace akamwambia Mr.kivuli nilitamani kumitambulisha lakini kiukweli wako na kazi nyingi kwa sasa hivyo inabidi tuwaache tu mana hata useme nini wakati wa kazi hawajibu kitu jambo ambalo lililopelekea mr.kivuli kuvutiwa sana na wafanyakazi hao .
Mr.kivuli alitoka nnje ya eneo lile na kuondoka lakini baada ya kufika nnje wafanyakazi wote waliondoa maski zao na kucheka sana na wala hawakuwa wengine bali wale wakinamama alokuwa akiamini walikufa hospitalini kwani walifungiwa chumbani na mmoja kati ya walinzi wa Jackbosi kabla ya moto kuunguza hospitali. Mr.kivuli alipofika tu eneo lile la kampuni ya Graja alianza kufanya michakato ya kuweza kuwapata wafanyakazi wa grace kwa kumtumia moja kati ya meneja wa kampuni hiyo, lakini meneja alimwambia wafanyakazi wenyewe hawajawahi toa maksi mbele yetu wewe utawezaje kufanya nao kazi ikiwa huwajui,? . Mr.kivuli kwa kuwa ni mtu watamaa sana aliwataka wafanyakazi hao hivyohivyo bila kujali chochote na hatimaye alimpa meneja yule fedha za kutosha ilikuweza kuwapa wafanyakazi hao ili waweze kufanya nae kazi. Meneja alielekea moja kwa moja kwa grace na kumpa pesa zile grace. Na grace akawapanga wakinamama na siku iliyofuata wakiwa wamevalia maski walienda kukutana na Mr.kivuli na wala Mr kivuli hakuweza hata kujihoji kwanini wamevalia maski alicho fanya ni aliwapa mikataba ili waweze kusaini lakini wakati mambo yote yanaendelea grace alikuwa akirekodi video na baada ya Mr.kivuli kusaini pia mikataba hiyo aliwalipa wafanyakazi hao pesa alizo ahidi kuwapa katika mkataba wao kisha wote wakatawanyika na kuendelea na shughuli zao. Siku iliyofuata Mr.kivuli alipo wasili ofisini kwake alikuta karatasi ya madai ya shilling milioni mia kwa kosa la kujalibu kuharibu kampuni ya Graja kwakuwachukua wafanyakazi wa kampuni hiyo hivyo anahitajika mahakamani na hakimu . Mr.kivuli alijiandaa huku akiamini hakuna kitu kinaweza kumtokea kwasababu wafanyakazi wanamaamuzi ya kuendelea kubaki au kuondoka katika kampuni wanapo pata kampuni yenye maslahi zaidi ya wanayo fanyia kazi. Mr.kivuli alijiandaa na moja kwa moja akaeleke mahakamani yeye pamoja na Mwanasheria wake walipo fika mahakamani walitegemea kumuona grace pia akiwa na Mwanasheria lakini ilikuwa tofauti kwani grace yeye alienda peke yake bila ya Mwanasheria yeyote yule zaidi ya karatasi alizobeba mkononi mwake. Hakimu alimsikiliza Mr.kivuli ambaye yeye alimwambia hakimu kuwa wafanyakazi hao c watoto wanaakili timamu hivyo wanamaamuzi ya wakuchagua ofa bora kwao. Lakini grace alicheka sana na kumwambia Mr.kivuli hii sio issue ya wafanyakazi na umri wao ni issue ya wewe kuuvunja mkataba baada ya kuvunja moja kati ya kipengere muhimu cha kuhujumu wafanyakazi wa kampuni unayoingia nayo Ubia ambacho wewe ndo ulichofanya badala ya kuwalinda umewaiba na kuifanya kampuni leo ishindwe kufanya kazi na kwakuvunja kipengele icho kama ulivyo saini unapaswa kulipa milioni 100 leo laasivyo ukae ndani mpaka utakapo lipa pesa hiyo kwasababu nahitaji kupata wafanyakazi wapya katika kampuni yangu mana wewe umewaiba na kwasababu hiyo kazi zimekwama kule kiwandani.
Mr.kivuli alimuangalia sana grace kwa hasira kisha akachukua hundi na kuandika kiasi cha shilingi milioni mia na kumkabidhi grace, kisha hakimu akatangaza rasmi uwekezaji wa Mr.kivuli katika kampuni ya Graja umefutiliwa mbali rasmi baada ya yeye kuvunja kipengere muhimu cha mkataba huo na baada ya kutangaza akawaomba wakumbatiane ili apate kuhakikisha kama hakuna tatizo kati yao ukizingatia wote wawili ni wafanya biashara wakubwa ambao wanaiingizia nchi kodi kubwa tu . Mr.kivuli alisimama na kumkumbatia grace kwanguvu sana kisha akamwambia nitahakikisha ndani ya wiki grace huna kampuni tena, lakini grace alicheka sana na kumwambia Mr.kivuli naitwa grace Steven mtoto wa yule mmiliki wa kampuni ya Graja ambae kuna muoga mmoja aliye mchoma sindano ili kujificha. kisha grace akacheka sana nakumuachilia Mr.kivuli na kumshukuru hakimu kwa msaada wake kisha grace akapotea zake maeneo ya mahakamani kabisa. Mr.kivuli alibakia kucheka sana na kumtumia grace picha ya ndugu yake WhatsApp na kumwambia unamjua huyu binti? . grace akamwambia ni binti yako Jackbosi . Mr.kivuli alimtumia emoji za kucheka na kumwambia ukicheza nampoteza. Lakini grace alituma emoji za kununa na kumwambia huwezi kupata mtoto ndo mana hujui uchungu mimi nna mtoto hivyo ukijalibu kucheza na mdogo wangu na cheza ma mke wako mana ndo kitu ambacho unajua maumivu yake. Mr.kivuli alitupa simu kwenye siti na kumwambia dereva ampeleke kazini. grace alimtumia message zile mke wa Mr.kivuli pamoja na Jackbosi , mke wa Mr.kivuli akamwambia grace inabidi Jackbosi aondoke hapa uje wewe kwasababu akiendelea kukaa hapa mume wangu atamtumia vibaya na mpango wetu utashindwa na mume wangu ataendelea kupotea zaidi jambo ambalo ctaki kuliona wala kulisikia tena. grace akamwambia Mrs.kivuli inabidi nimwambie mimi Jackbosi lakini Mrs.kivuli alimwambia hawezi kubali kwani anachogopa yeye ni Mimi kukaa hapa mwenyewe, ila akijua nipo ndani ya mchezo atakubali kukupa wewe nafasi japo nahisi atatuchukia wote kwakumficha jambo hili. grace akamwambia Mrs.kivuli sawa mwambie Jackbosi uKweli wote .
Mrs.kivuli aliingia chumbani kwa Jackbosi na kumwambia nadhani unakumbuka kila kitu alicho kwambia grace na mimi niko hapa tu kukwambia ni ukweli kama kuna sehemu ulihisi anakudanganya na mchezo anaocheza grace na mimi nipo ndani yake. Hata hivyo najua lazima utakuwa unajiuliza kwanini mama anamgeuka baba angali anaonekana anampenda sana lakini huo si ukweli baba yako nilishaachana nae siku alipo nitoa kizazi, tangu siku hiyo alikufa maishani kwangu, Jackbosi akamuuliza mama yake ' kwanini baba alifanya hivyo wakati anakupenda sana' ? .hapo ndo Mrs.kivuli kivuli akamwambia miaka miwili baada ya mimi kukabidhiwa wewe nilikupenda sana kama binti yangu wa kumzaa. lakini sikumoja huyo shetani Mr.kivuli alipata tamaa ya pesa baada ya moja kati ya mabosi wake wa nchi Za nnje kumwambia binti yake anahitaji moyo na akifanikisha kumpatia ata mpamilioni 800 , Mr.kivuli alimwambia bosi wake atume vipimo vya binti yake ili yeye awapime watoto alio nao ili aweze kujua nani vipimo vyake vinaenaenda na mtoto huyo, basi vipimo vikatumwa na yeye akawapima watoto wote kituoni kwake lakini kwabahati mbaya hakukuwa na mtoto yeyote anaeweza kufanya upandikizaji wa moyo kwajili ya binti yule. Mr.kivuli alichanganyikiwa sana kwani pesa aliyo ahidiwa ni kubwa. tamaa ikamtafuna na hapo ndo akakuchukua wewe kwa siri bila ya kuniambia na kwenda kukuchukua vipimo na baada ya vipimo majibu yakaonyesha asilimia 99.9% unaruhisiwa kumtolea moyo mtoto wa bosi wake na akawa salama. baada ya moja ya walinzi wake kuona Mr.kivuli kamaanisha kukutoa wewe moyo ufe na ampe mtumwingine kwa pesa mlinzi huyo alinifuata na kuniambia kilakitu na nilipo muuliza hakukataa na hakuonyesha kujuta na hapo ndio mimi nikaamua kupinga suala hilo na Mr.kivuli ili kunikomoa akaniambia nichague kukulinda wewe au kizazi changu na hapo ndo nikakuchagua wewe, lakini nilijalibu sana kuhakikisha na kukomboa wewe bila ya kupoteza kizazi changu ila ilikuwa ngumu sana kwangu hivyo nikafanya maamuzi ya kuwa na wewe tu maishani kwani niliamini naweza kuwa na kizazi na nisipate mtoto vilevile au nipate halafu afe na hapo ndo nikakubali bila kujali madhara. Nikakuchukua wewe nikaenda kwa Daktari aliye mchagua yeye nikafanyiwa upasuaji na kutolewa kizazi na tokea hapo nilikuwa chizi sana na mimi nilitafuta watu wakampiga kiasi cha yeye kupoteza uwezo wa kupata mtoto na bado sikuridhika nikawatafuta waathirika wa mambo yake machafu , baada ya miaka nikakutana na grace pamoja na rafiki yangu Steven na hapo ndo kazi ilianza na kwasasa kazi inaenda kuisha lakini kwamaelezo baba yako aliyompa grace hii sio sehemu salama kwako binti yangu inakubidi umkabidhi grace nafasi yako sitaki kumipoteza na nyie kwani nitakufa. najua pengine unatuchukia mimi na grace kwasasa lakini bado nakuomba umpenafasi yako grace ili apate kumalizia alicho kianza na mwishoe mimi, wewe na grace kwa pamoja na wakinamama wale na baba yako Steven tutaishi kwa furaha. Jackbosi machozi machozi yalimtoka kisha akachukua simu yake na kumwambia grace njoo nyumbani kuanzia sasa wewe ni Jackbosi mpaka kazi itakapoisha mimi niachie kampuni nitaendelea kuwasimamia. Lakini nataka hiii misheni yenu iishe mapema nifurahie maisha yangu na nyie mnipendao na niwapendao pia .
USIKOSE SEHEMU YA 15 $16
 
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE.

MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.

SEHEMU: 13 $ 14.

WHATSAPP No: 0746115688.

Mr.kivuli alimshangaa sana grace lakini Jackbosi alijifanya ndo aelewa kabisa kwani alisimama na kumwambia baba yake ' hivi kwani baba mimi nina pacha , Mana sikumbuki kama mlisha wahi kuniambia hilo na nikimuangalia huyu mwenyekiti wa kampuni ya Graja najiona mimi kabisa bila kupinga . grace nae alimshangaa sana jackbosi kama vile hakuwahi kukutana naye kabla.

Mama umejua kunipa furaha japo kimoja tu kila siku , ahsante Sana mkuu

Sent from my CPH1933 using JamiiForums mobile app
 
TAMTHILIA : CHALLENGE MADE.
MUANDISHI : WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS.
SEHEMU: 15 $ 16.
WHATSAPP : 0746115688.
Grace alihamia rasmi nyumbani kwa Mr.kivuli na Jackbosi alihamia nyumbani kwa grace . grace alimkabidhi Jackbosi kampuni na biashara zote za familia na kumwambia kila kitu ni cha kwetu na sio cha kwangu tu , kwasababu utafutaji wa baba haukuwa kwaajili ya binti mmoja tu bali binti zake wote wawili yaani grace na Jack ndio maana hata kampuni aliita Graja. mimi naenda kwa Mr.kivuli kutafuta uhuru wako mdogo wangu pamoja na mimi na watu wote wanaoteseka kwaajili ya Mr.kivuli na pia kila mtu ajue kuwa wewe ndio Jack mtoto wa mzee wetu Steven na mimi ndio dada yako na Mrs.kivuli ndo mama yetu, kwasababu amekupenda wewe kama mwanae mimi sina tatizo nae kabisa kwasababu furaha yako mdogo wangu ndo ya dada yako kumbuka hilo . Grace alipoondaka Jackbosi alianza rasmi kusimamia kampuni na kwakuwa yeye alisoma biashara alipofika tu hatua ya kwanza alifuta project zote ambazo hazina faida na kupunguza wafanyakazi wasio kuwa na ulazima na kila mfanyakazi aliyekuwa anamfukuza alimlipa fedha za kujikimu Siku hiyohiyo aliyoondoka.
Mr.kivuli yeye hakuweza kujua hata kama pale nyumbani wanaishi na grace kwani hakuwahi kukaa na Jackbosi muda mrefu kiasi cha kujua huyu ni grace na huyu ni Jackbosi.
Baada ya wiki moja rasmi wakinamama wale walio saini mkataba na Mr.kivuli walienda kuanza kazi na Mr.kivuli aliwagawanya katika kila biashara zake akaweka mwanamama mmoja. Kwasiku za mwanzoni kila mwanamama alisimamia vizuri wafanyakazi waliokuwa chini yake lakini hawakuruhusu kabisa mtu yeyote kuona sura zao pamoja na kazi nzuri waliyofanya. Kwabahati nzuri Ade alibahatisha kufanya kazi katika eneo ambalo ndo madawa ya kulevya yanapotengenezwa na james lakini pia huyohuyo james ndo alikuwa kiongozi wa eneo hilo kwa upande wa utengenezaji. Lakini kwabahati nzuri pia Ade aligundua hakuna madawa yaliyo toka nnje ya eneo lile kwani ilikuwa ni ngumu kwao kusambaza amigo kwani James ni mgeni alihitaji mwenyeji kwanza iliasome ramani na ndio maana Ade akaajiliwa ili aandae mpango wa madawa hayo kusafirishwa nnje ya nchi na kusambazwa kwa watumiaji wadogowadogo.
Upande wa grace yeye alijiweka karibu sana na Mr.kivuli na kumfanya amuamini sana kiasi cha yeye kumruhusu kuingia katika chumba ambacho kinanyaraka na karatasi mbalimbali za mikataba yake pamoja na viongozi wa siri ambao walikuwa kwenye mtandao wa Mr.kivuli.
taratibu Mr kivuli alimuamini grace kuwa ni Jackbosi na wafanyakazi alio waajili na baada tu ya wote kupata imani ya Mr.kivuli walipanga Siku ili wakutane wapange mpango wa mwisho wa kumuangusha sasa Mr.kivuli , ambae wao waliamini ndie kiongozi wa biashara zote hizo chafu. Walipo kutana siku hiyo watu walishangaa sana kuona kumbe grace na yeye anateam ya viongozi wa kubwa wa nchi ambao wao ni waaaminifu na wanaopenda nchi yao kiasi cha kujitolea kuungana na grace pamoja na Mrs.kivuli ili waweze kupata uhuru wa nnchi na vijana kwa ujumla kwasababu biashara haramu za Mr.kivuli ziliwalejenga zaidi vijana. kwapamoja walikubaliana kwanza kabisa kuteketeza biashara zote zinazo mhusu Mr.kivuli.
kisha kupata nyaraka za watu wanaoshirikiana nae ili kuweza kuwatishia waweze kutoa ushahidi juu yake ili ahukumiwe, halafu bila ya wao kujua wakati wanatoa ushahidi ndio watakuwa wamejiangamiza pia. wakinamama wanaofanya kazi katika vituo vya Mr.kivuli walipanga mipango ya kuweza kuteketeza sehemu hizo, na baadhi ya wafanyakazi wa Mr.kivuli waliamua kuwasaidia kwani hata wao hawakufurahia kufanya kazi katika biashara zake lakini yeye aliwalazimisha na kuwatishia kuteketeza ndugu zao kama watakataa na hio ndio sababu ya wao kufanya nae kazi hivyo walivyogundua kuna mtu anahitaji kumteketeza Mr.kivuli waliungana nae kwani walikuwa wamesha choka na wanahitaji uhuru wao .
Basi siku moja wakati Mr.kivuli yupo katika Tafrija na wafanyakazi wake mtu mmoja alimtumia ujumbe afungue WhatsApp kuna zawadi yake na Mr kivuli alipofungua aliona jinsi biashara zake zinavyo teketea kwa moto na pia aliwaona wale wakinamama walio vaa maski wakiwaongoza wachomaji wa biashara hizo. Mr.kivuli alipokuwa akijiuliza ni wakina nani hasa hawa wakinamama na kwanini wanafanya hivi wakati niliwaajili na kuwapa pesa nzuri tu, palepale kwenye video wakinamama walivua maski huku wakimcheka sana Mr.kivuli kisha kwapamoja wakamwambia Mr.kivuli wewe ni binadamu tu na kama ulihisi wewe ni mungu bhasi ulikosea sana kwani toka mwanzo ulipaswa kujua wewe ni binadamu tu. Kisha wakinamama kwa pamoja wakavaa maski na kuondoka katika eneo lile .
Mr.kivuli akawagawanya wafanyakazi waliokuwepo katika Tafrija hiyo haraka ili waende sehemu mbalimbali za biashara zake kwani alihisi pengine labda ni utani tu na mambo ya kuedit ili kumkatisha tamaa yeye.
Lakini baada ya muda mchache mfanyakazi wa kwanza alipofika eneo la tukio alimpigia bosi wake video call kumuonyesha kuwa kweli moto umewaka na hakuna jinsi ya kuokoa chochote, baada ya taarifa hizo grace na Mrs.kivuli waliwaambia wageni wote waondoke Tafrija imeghairishwa kisha wakaiingia ndani pamoja na Mr.Kivuli,
wote walikuwa wamekaa kwenye kochi kusubiri taarifa mpya kutoka kwa wafanyakazi walioenda kuangalia maeneo yaliyo bakia na baada ya muda kidogo James alimpigia simu Mr.kivuli na kumpataarifa ya kuwa biashara zote zimeteketea kilichobakia ni majivu tu hakuna cha zaidi.
Hapohapo Mr.kivuli alianguka kwa presha, ndani ya wiki moja alikuwa akiamka analia ntakuwa masikini mimi kisha anazimia, madaktari walijalibu kumuhudumia kwa kadiri walivyoweza na kweli hali yakuzimia zimia ikapotea kabisa na madaktari waka ahidi siku inayo fuata watamruhusu Mr.kivuli. Wakati Mr.kivuli anaugulia hospitali grace alichukua nyaraka zote za siri nakuzificha lakini pia akayapa taarifa mabenki yote aliyokopa kuwa Mr.kivuli kafirisika na hivi karibuni atatoroka hivyo mabenki yote yakaungana na Siku iliyofuata wakati Mrs.kivuli na grace wanamchukua Mr.kivuli kumpeleka nyumbani Mr.kivuli alipofika nnje ya hospitali akaona kulikuwa na mnada wa live kwenye tv uliokuwa ukionyesha jinsi nyumba, magari na mali nyingine za Mr.kivuli zinavyo pigwa mnada na hapo ndo Mr.kivuli alianguka tena na kurudi hodini.
Lakini upande wa Jackbosi bila kumpa taarifa mtu yeyote aliongea na Daktari bingwa wa nchizannje wamasuala ya ubongo na kumueleza afya za wakina mama wote waliochanganyikiwa na akamuelezea pia kuhusu chip walizonazo na Daktari alimpa taarifa Jackbosi anauwezo wakuwasaidia kwasababu upasuaji wao una asilimia sabini na tano za wao kuishi , baada ya jibu hilo Jackbosi alimuuliza Daktari anahitaji kiasi gani lakini Daktari akamwambia nataka wapone tu kwasababu kwa stori uliyo ni hadithia kuhusu wao mimi pia ni muathirika, kwani nililetwa huku kutolewa viungo tu lakini moja kati ya madaktari aliniokoa na kunisomesha mpaka sasa mimi ni Daktari bingwa na nafanya hivi kwaajili ya watu wote walio uwawa kwa amri ya Mr.kivuli kwani sisi ni ndugu tulikua pamoja na kupendana sana kama si yeye naamini tungekuwa pamoja mpaka sasa . wakati grace anammaliza Mr.kivuli taratibu kwa Jackbosi nayeye Daktari aliwasili jijini dar es salaam na kuwafanyia upasuaji wakinamama wote na akafanikiwa kutoa chip kwa wakinamama wote na wote wakatoka katika upasuaji salama lakini pia akaanza kumtibu Steven taratibu taratibu na kweli nafuu ilianza kuonekana.
Mr.kivuli alipo amka kwenye mshtuko wa safari hii alimwambia ukweli wote grace akijua ni Jackbosi kuhusu biashara alizo fanya , Mr.kivuli bila kujua grace alikuwa anamrekodi kwa kamera aliyokuwa ameivaa kama kifungo katika shati lake lakini kikubwa zaidi alimpa siri ambayo hata grace alikuwa hajui kuwa yeye sio bosi wa hizo biashara bosi wake alikuwa ni mstaafu mmoja wa Udaktari ambae anaduka dogo tu la madawa la kuizugia serikari na pia akawaambia mtaa alipo ili wakamwambie anahitaji msaada wake lakini kwa bahati mbaya grace ,Mrs.kivuli pamoja na wakinamama walipoelekea mahali ambapo Daktari huyo yupo walikuta msiba kwani Daktari huyo alijinyonga baada ya kujua mambo yameharibika ili familia yake isimchukulie yeye ni jambazi na kweli japo wakina grace waliwaambia ndugu zake ukweli wa mzee huyo lakini ndugu hawakuamini kwani hawaku wahi kuona dalili yeyote kwa mzee huyo ya kuonyesha anafanya biashara hiyooo.
Wakina grace waliona hamna haja ya kuwalazimisha watu, kwanza kashajiadhibu mwenyewe na kwaupande mwingine bado Mr.kivuli ndo hatari zaidi kuachiwa huru kwani yeye ndo alikuwa mpangaji mkuu na msimamizi wa biashara hizo hivyo akiwa huru mambo yataharibika hivyo grace pamoja na Mrs.kivuli walimua kumfungulia mashtaka Mr.kivuli kwa kujihusisha na biashara za madawa, na viungo vya binadamu mashtaka ya madawa yalipelekea james kukamatwa .
wakati Mr.kivuli yupo hospitalini alishangaa kwenye tv kuona mkewe na grace wamemshitaki yeye tena bila woga hapo ndo Mr.kivuli akili alimjia akavua nguo za hospitalini na kutoroka hivyo polisi walipo kuwa wakimtafuta hospitalini ili akamjibu mashtaka Hawakumpata.
grace nae alimwambia Mrs.kivuli asiwe na wasiwasi kwani Mr.kivuli hana pakwenda chaumuhimu ni kuwalaghai washirika wake , na kweli grace akakutana na washirika mbalimbali wa mr.kivuli na kuwaonyesha ushahidi wa kuwamaliza kama hawatatoa ushahidi dhidi ya Mr.kivuli na kweli washirika wake wote baada ya kuona ushahidi huo hawakuwa na jinsi walikuwa tayari kusimama mahakamani kama mashahidi . Usiku mmoja polisI walipo kuwa katika windo walimuona Mr kivuli akiwa amepitiwa na usingizi chini ya gari la kubeba mataka na hapohapo wakamkamata na baada ya mwezi kesi ilipelekwa mahakamani na mashahidi wa kwanza walikuwa ni wakinamama waliokuwa na grace hospitalini ambao ushahidi wao ulikataliwa kwani mahakama ilishindwa kuamini kua kweli Mr.kivuli anapandikiza mbegu kwa wakinamama kwani wao watoto walikuwa ni wawanaume zao ambao wanadai wameuwawa na Mr.kivuli, hivyo mahakama ili mwambia grace atafute ushahidi mwingine. grace akawashawishi viongozi walioshirikiana nae na kweli waliwasili mahakamani na kutoa ushahidi lakini baada ya grace kutoa ushahidi mwingine wa video ambayo ilikuwa inaonyesha hadi wao walikuwa pamoja na Mr.kivuli mahakama ili kataa kuwaamini pia kwani waliamini grace kuwatishia kwani ni ngumu mtuhumiwa kutoa ushahidi wa kujizulu bila sababu za msingi hivyo hakimu aliomba utulivu mahakamani na kumwambia grace kama hana ushahidi wa kueleweka kesi itafungwa mana hapangilii ushahidi hivyo Mr.kivuli atahukumiwa kwa makosa yenye ushahidi tu na makosa yenye ushahidi yalikuwa madogodogo tu ambayo anaweza epuka kwa faini tu .
grace alichoka kwani alikuwa hajui atapatia wapi ushahidi mwingine wakuwafanya Mr.kivuli na wenzake wasitoke jela kabisa lakini ghafla hakimu kabla hajatamka hukumu Jackbosi aliingia akiwa na wakinamama wale walio kuwa wamechanganyikiwa tena wakiwa wazima pamoja na Steven na Daktari yule ambae ni ushahidi tosha wa suala la upandikizaji wa mbegu kwani yeye pia mamayake alipandikizwa tu mbegu hivyo yeye hamjui hata baba yake zaidi ya mama yake, lakini pia anajua hadi hospitali wanayotolewagwa vijana hao viungo baada ya kutolewa nchini na Mr.kivuli.
hakimu alimuuliza wewe ni nani na Jackbosi alimwambia muheshimiwa hakimu mimi naitwa jack Steven ila maarufu kama Jackbosi na hawa unao waona mbele yako ni waathirika waliotokana na huyo Mr.kivuli yaani namaanisha baba yangu mlezi.
Mr kivuli alishangaa sana kwani aliyekuwa akimuhisi kama Jackbosi ni grace lakini pia alijua ni ngumu kupona tena kwa ushahidi aliokuwa nao Jackbosi hivyo alimwambia muheshimiwa hakimu inatosha , kwasasa naomba tu nafasi ya kuongea kidogo, muheshimiwa hakimu akampa Mr.kivuli nafasi aliyo itaka na Mr kivuli kwanza akakubali shutuma zake na kumwambia hakimu hata hawa viongozi kweli wanahusika na taratibu akawageukia viongozi wale pamoja na wafanya biashara wakubwa tu na wengine ni viongozi hadi wa dining ambao alikuwa wanaoshirikiana nao kisha akawaambia wakubwa Inatosha hakuna njia ya kutoka tena na wote wakainamisha vichwa chini kwa aibu . Mr kivuli akamuomba hakimu tena nafasi ya kuongea japo kidogo na hakimu alimpa tena nafasi, Mr.kivuli akasema nashukuru sana wote nyie mlioshirikiana kuhakikisha leo najuta kwa ubinafsi na tamaa zilizo kuwa zina niandama, lakini pia nashukuru kwani nyie mmenifundisha kuwa changamoto zinaweza kujenga usipo jali ujenzi huo utachukua muda gani, mimi umaskini tu ulinifanya nikaogopa kabisa kupambana nikashawishiwa na Daktari john ambae ni marehemu kwasasa nakwapamoja bila kujali tukatumia uhai wawatu wengine kama pesa kwetu, mpaka sasahivi najiuliza kama umaskini tu umenifanya nikawa mtu mbaya hivi je ingekuwa ndugu zangu ndo wamepitia waliyo yapitia ndugu zenu sijui nchi yangu leo ingekuwa inapambana na mtu wa namna gani, kisha mr.kivuli akatoa bunduki aliyokuwa ameificha na kuisalimisha kwa askari wakaribu yake kisha akasema nilitamani mambo ya kiwa magumu nijipige risasi nifie mbali ili aibu isinipate lakini nimegundua hata nijikatekate vipande kama nyama cwezi lipa madhambi niliyo tenda hivyo muheshimiwa hakimu naomba nipe adhabu itakayo wafanya watu waogope kabisa kufikilia kufanya nilicho kifanya mimi. kisha Mr.kivuli akamwambia Jackbosi ahsante sana wewe pamoja na dada yako grace kwa mlicho kifanya pamoja na mke wangu kaeni mkijua sijawachukia wala sinakinyongo na nyie nisameheni sana kama inawezekana na nawapenda sana kuanzia sasa kwani mmenifundisha upendo ananguvu kiasi gani . Baada ya maneno hayo Mr.kivuli alihukumiwa kunyongwa pamoja na washirika wake wote.
grace aliendelea kuwa Daktari na kumlea mwanae, lakini pia Jackbosi aliolewa na Daktari yule na alipata watoto wake wawili , wakinamama waliendelea nashughuli zao kwa wale waliokuwa na taaruma zao na wengine waliajiliwa katika kampuni ya Graja chini ya usimamizi wa mwenyekiti Jack steven

MWISHO.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom