Tamthilia ya Slay queen - Maisha Magic

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,510
4,224
Habari wanajamii,
Niende moja kwa moja kwenye mada husika

Nimebahatika kuangalia vipindi kadhaa vya hii tamthilia ya slay queen ndani ya Maisha magic na nimeshangazwa sana na ukosefu wa umakini wa waandaaji wa tamthilia hii.Sijajua kama huwa wanashirikisha wataalam wengine au angalau wao wenyewe kurudia kuangalia ili kubaini kasoro ndogo ndogo ambazo zinawaharibia kabisa.

Inashangaza kwakweli kuona team nzima ya production mpaka editing mpaka waigizaji wenyewe kushindwa kubaini au kubuni jina la kampuni ambayo wangeigizia.

Kwenye hii tamthilia kuna kampuni ya mawasiliano inaitwa For connect.Kwa kweli labda huenda binafsi nimekuwa na mtazamo tofauti ila huenda walitaka kumaanisha Four connect lakini makosa ya uchapishaji yalifanyika.

Lakini hata kama mtazamo wangu sio sahihi huenda walitaka kumaanisha ' kuonganisha' yaani ' To connect' Lakini hiyo bado haiendani na jina lao la For connect.'For' ni kiunganishi sawa ila sidhani ni sahihi kwenye 'Connect' badala ya 'To connect'.

Mbaya zaidi mpaka kwenye slogan ya kampuni yenyewe ina makosa.Inasomeka ' Bring people closer' wakitaka kumaanisha 'huleta watu karibu'.Hii ilitakiwa iwe 'Bringing people closer' Lakinì cha ajabu mpaka T-shirts za wafanyakazi mpaka banners zimeprintiwa na haya makosa na wamevaa tu hivyo hivyo bila aibu.

Sasa najiuliza kuwa ina maana wao wenyewe Hawaoni haya makosa kwenye Tshirts zao? Haya mambo kiukweli yanarudisha sana nyuma tasnia ya filamu nchini.Naomba wahusika myafanyie kazi na kurekebisha ili tasnia hii izidi kusonga mbele na kuwa na heshima ndani na nje ya nchi.

Ahsante.

20210310_133540.jpg
 
Humo ndani kuna mwamba anaitwa Dr DOZI ni hatari sana, nlipenda harakati zake.
 
Yale waliokuwa wanafanya kwenye Bongo Movie wamehamishia kwenye tamthilia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom