Tamthilia ya Game of Thrones imenifanya niitilie shaka Biblia

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,692
Pasi na shaka kwa waliobahatika kuitazama series ya GAME OF THRONES mpaka mwisho watakiri kua kwa upande wa mpnagilio wa matukio wahusika mzingara story..... ile series haina mpinzani

Ni series ambayo ukiacha kuitazama huku una fananisha au kuipambanisha na series fulani basi unaweza ukaachwa mdomo wazi na jinsi wale jamaa walivyo iandaa

Mimi ni moja kati ya watu walio tazama series hii zaidi ya mara 4 na kati ya story ambayo nimekua nikitamani kujua zaidi ni ya familia ya Tygarius (ile ya Mother dragon Daenerys )

Shahuku yangu ikanifanya niangukie kwenye vitabu vyake ambvyo vina Original story kuanzia Book one mpaka 5 ambapo kuna Dance with dragon,clush of kings ,song of ice and fire ,game of thrones a feast of crows ....

Hii story iko deep sana na sidhani kama itakapo kuja kupita miaka 100 au zaidi watakao simuliwa watasimuliwa kama fiction ..

Ni simulizi iliyo timia haswaa kuanziaa koo vizazi ramani mazingira mpaka vitu vidogo vidogo kama mapanga yale ya verilian steel yani unaweza sema ni kweli

Hii imekuja kuibua maswali mengi sana kichwani kwangu ambayo kimsingi sifurahishwi nayo ila ndio yamesha kuja..

Kama mtu mmoja au wawili wanaweza kusuka story ikatimia namna hii haiwezekani kweli kukawa na kundi la watu walio timia akili kua walikaa wakasuka zile simulizi za kutembea juu ya maji au kupasua bahati au kupaa angani au adamu na eva ... ?

Kwasababu hizi story za huku kwenye kitabu tusicho ruhusiwa kuhoji nazo zina ungano wake ila huyu jamaa wa game of thrones asee alipika bwana ...

Mimi binafsi baada ya kumaliza hivyo vitabu nimeingiwa sana ba wasiwasi juu hizi simulizi za kwenye vitabu vya kidini inawezekana zikawa ni Ngano tu ila sisi tuna zichukulia serious. .
JamiiForums-1315151482.jpg
 
Kiukweli hata mimi nimewaza sana ni mwandishi wa aina gani anaweza kuandika simulizi iliyokamilika kiasi kile.Sijawahi kuona tamthilia iliyosukwa ikasukika kama GOT.zaidi sana haiishii kwenye video tu Bali mpaka kwenye vitabu vyake (song of ice and fire... e.t.c) Kwa uandikaji ule sishangai kuona mtoa mada akiyumbishwa kuhoji kuhusu uandikaji wa Biblia.
 
Sikiliza mtoa maada! dunia hii kuna nguvu mbili tu ya shetani na ya Mungu, Nguvu zote hizi zinatenda kila moja kwa kusudi lake Shetani anajua na Mungu nae anajua na wote hawa hutoa uweza wao kwa yoyote atakae taka, Swali ni ipi iliyo sahihi kutenda katika hali ya kiubinadamu bila kuumiza mwingine? hapa ndipo kwenye tatizo.
 
Ukisema uta question biblia unamaanisha ufahamu wako katika Mungu ni Mdogo sana.
Maana ungekuwa na ufahamu mkubwa katika Mungu ungesema kama binadamu tu wanaakili hivi Mungu ni zaidi.

Pia ungekuwa msomaji wa biblia wapo watu waliokuwa wenye akili kipindi cha farao lakini ulipokutanishwa na Mungu wa Musa akili zao hazikufua dafu.

Mshangae na Kumtukuza Mungu kwa kuwaumba watu kama hao.

Biblia imetusisitiza sana neno la Mungu likae kwa wingi ndani yenu.
Imani zetu zimekuwa nyepesi sana kutikiswa kwasababu ya uhaba wa neno la Mungu ndani mwetu.

Suleiman alikuwa na akili (hekima) sana hata malkia wa kusini alimwendea kila wakati lakini bado ukisoma kitabu chake cha muhubili utajifunza anachokwambia
MUHUBIRI 7;29
MATHAYO 12:42
 
Tatizo una uelewa mdogo wa masuala ya Imani ya Kimungu. Na kamwe Imani haithibitishwi na "Idea" za watu. Imani hujithibitisha yenyewe ukiwa unatafuta vitu vya kusoma ili kuProve imani basi hata Hadithi ya Sadiki na chitemo unaweza kuitumia.

Hiyo ni talent tu inayotoka kwa Mungu, ukisoma Kazi za Tolkien au Stan Lee utakuja kusema kwamba hawa watu walikua mashetani kwa kutengeneza imaginary characters and universe. Kwa Tolkien na Stan Lee, George RR Martin haiingii hata robo.

Soma, nikikupa kitabu kimoja cha Saint Thomas Aquinas ukakisoma kitakuondolea ufinyu wote wa imani utakaokuanao
 
Pasi na shaka kwa waliobahatika kuitazama series ya GAME OF THRONES mpaka mwisho watakiri kua kwa upande wa mpnagilio wa matukio wahusika mzingara story..... ile series haina mpinzani

Ni series ambayo ukiacha kuitazama huku una fananisha au kuipambanisha na series fulani basi unaweza ukaachwa mdomo wazi na jinsi wale jamaa walivyo iandaa

Mimi ni moja kati ya watu walio tazama series hii zaidi ya mara 4 na kati ya story ambayo nimekua nikitamani kujua zaidi ni ya familia ya Tygarius (ile ya Mother dragon Daenerys )

Shahuku yangu ikanifanya niangukie kwenye vitabu vyake ambvyo vina Original story kuanzia Book one mpaka 5 ambapo kuna Dance with dragon,clush of kings ,song of ice and fire ,game of thrones a feast of crows ....

Hii story iko deep sana na sidhani kama itakapo kuja kupita miaka 100 au zaidi watakao simuliwa watasimuliwa kama fiction ..

Ni simulizi iliyo timia haswaa kuanziaa koo vizazi ramani mazingira mpaka vitu vidogo vidogo kama mapanga yale ya verilian steel yani unaweza sema ni kweli

Hii imekuja kuibua maswali mengi sana kichwani kwangu ambayo kimsingi sifurahishwi nayo ila ndio yamesha kuja..

Kama mtu mmoja au wawili wanaweza kusuka story ikatimia namna hii haiwezekani kweli kukawa na kundi la watu walio timia akili kua walikaa wakasuka zile simulizi za kutembea juu ya maji au kupasua bahati au kupaa angani au adamu na eva ... ?

Kwasababu hizi story za huku kwenye kitabu tusicho ruhusiwa kuhoji nazo zina ungano wake ila huyu jamaa wa game of thrones asee alipika bwana ...

Mimi binafsi baada ya kumaliza hivyo vitabu nimeingiwa sana ba wasiwasi juu hizi simulizi za kwenye vitabu vya kidini inawezekana zikawa ni Ngano tu ila sisi tuna zichukulia serious. . View attachment 2053525
Hauna akili .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom