Tamthilia mpya ndani ya radio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamthilia mpya ndani ya radio

Discussion in 'Entertainment' started by Kabota, Jun 6, 2010.

 1. Kabota

  Kabota Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Aug 15, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  "Detour of Real Love" ama "Njia Ndefu ya Penzi la Dhati" ni tamthilia mpya ya radio ambayo imeandaliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwapa burudani wapenzi wa tamthilia za radio wenye hamu ya kupata drama yenye mfumo wa filamu kupitia radio.Tamthilia hii ya ukweli inamhusisha kijana handsome aitwaye Ian ambaye anapata mkate wake wa kila siku kwa shughuli ya ukonda wa daladala. Katika kazi zake za kila siku anakutana na dada mrembo, msomi na mtoto wa tajiri aitwaye Rachel ambaye anapanda daladala hiyo akiwa na mpenzi wake Erick ambao wanasoma chuo kikuu. Upole, werevu na mvuto alionao Ian unampagawisha Rachel na kumfanya afanye kila aliwezalo kumpata kijana huyo bila kujali tofauti zao za maisha. Baada ya Erick kunyang'anywa mpenzi wake na konda Ian, anaamua kulipiza kisasi kwa kuwawinda wapenzi hao wapya.

  Furaha fupi na ahadi aliyoipata Ian kwa kupendwa na Rachel inadumu kwa muda mfupi na kuyaona maisha kama jehanamu. Fuatilia tamthilia hii kila siku za jumatatu saa tano usiku na kurudiwa jumapili saa sita usiku kupitia Radio Free Africa.

  "Detour of Real Love" imeandikwa na mwandishi anayekuja juu Tanzania aitwaye Victor Chuma na kutayarishwa na Fredrick "Skywalker" Bundala. Muziki katika tamthilia hiyo umetayarishwa na Skywalker na Amba producer kutoka Iringa.

   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Itarushwa Radio gani saa?...Tuambie basi
   
 3. Kabota

  Kabota Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Aug 15, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Itarushwa kupitia Radio Free Africa na hapo kwenye maelezo imeandikwa hivyo.
   
Loading...