Tamthilia katika Runinga zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamthilia katika Runinga zetu

Discussion in 'Entertainment' started by Katavi, Nov 18, 2009.

 1. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Jamani hii michezo ya kuigiza na tamthilia za magharibi katika runinga zetu hapa bongo zimekuwa nyingi hadi zinawachanganya wapenzi/wafuatiliaji wake na mara nyingine inakuwa kero kwa watu wengine wasio wapenzi wa vipindi hivyo. Mbaya zaidi wapenzi wa vipindi hivi ni wanafunzi hasa mabinti wanaokaa macho hadi saa tano au sita usiku kufuatilia michezo hiyo badala ya kusoma, na stori zao shuleni mara nyingi huwa juu ya tamthilia hizo.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahaha na hivo vitoto navyo tamthilia zenyewe zinaanza saa tatu au saa nne fungia watoto wote room wakasome hawajui elimu ni ufunguo wa maisha

  dah ila kweli tamthilia zimezidi
   
 3. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  First lady

  We huwa unaangalia ipi?
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hii ni kutokana na rika. maana kila kitu kina wakati wake. wengine hupenda zilipendwa, wengine mpira, wengine kwenda disco, wengine kulala n.k. hii ni kutoka na umri. Sio mbaya kuangalia hata kama ukiwa ni mwanafunzi kuwa unatakiwa usome. pengine huo muda zinavyoonyeswa sio muda kwa baadhi ya wanafunzi kujisomea. lakini ni vizuri wanafunzi wenyewe wajue kipi muhimu wanachopaswa kuzingatia maana unakuta mtu akiangazia hizo tamthilia kumbukumbu haimtoki kichwani atakuelezea A-Z. lakini akisoma kusahau ni rahisi sana.

  kwa maoni yangu ni vyema ile kumbukumbu anayokuwa nayo ya hizo tamthilia au michezo ya kuigiza ndio awe pia anaitumia kukumbuka alichofundishwa darasani. ni jukumu la wazazai/walezi kuwaeleza hayo yote ili wanapokuwa wakiziangalia hizo tamthlia wajue kuwa ni changamoto ya kufeli au kufaulu masomo yao. kupanga ni kuchagua mwana mwerevu ni faraja ya mamaye bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa babaye.
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwa kumfungia tu hawezi kusoma. atakuwa anasikilizia. labda ule muda uliomfungia ukishamfungulia chukua daftari au kitabu alichokuwa anasoma mpe quiz kutokana na alichosoma akiweza utajua kuwa alikuwa anasoma otherwise ni danganyatoto. si unajua tena akili ikijityuni kufanya kitu inakuwa taabu kuacha kukifanya hasa kama unachotaka kukifanya kiko kwenye damu yako. kazi kweli kweli.

  ila kwa kweli tamthilia zimezidi yaani unakuta TV moja zaidi ya habari basi vipindi vinavyofuata kwa wiki kuna tamthilia zaidi ya tano, maigizo zaidi ya matatu kwa wiki, marudio ya vipindi vilivyopita, yaani bora wangepunguza
  hizo tamthilia wakaweka vipindi vya afya, elimu, utunzaji wa mazingira, kuonyesha tamaduni zetu za mikoa mbalimbali angalau tujue kila mkoa una tamaduni zipi inakuwa nafuu zaidi.
   
 6. Jerome

  Jerome Senior Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siyo siri mdada mimi ikishafika saa tatu kama nimewahi kurudi ktk ulabu nanyanganya remote control watoto walale,nimeshawahi rudi kiwanja saa 6 ucku nikawakuta wanaangalia tamthilia tena kibaya zaidi wako na mama yao unajua wamama ni mashabiki namba moja hivyo wanapenda watoto nao wawe mashabiki kama wao
   
 7. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hizi tamthilia zinafanya watu wawe addicted, yaani saa ya tamthiliya kuna watu wanatumbulia macho hapo tu, shughuli nyingine zote kama kuangalia home works za watoto kuhakikisha wanajisomea etc zinasimama wengine hata mtoto mdogo akianza kulia wana ita "dada hembu mchukue mtoto" bila hata ku angalia analia nini

  wakati mwingine unakuta vitoto vidogo chini ya miaka 12 navyo vimekaa na mama zao vina watch tamthiliya, hivi hizi tamthilia hazipo rated? maana zina mambo kama strong languages, violence, some sexual contents na materials nyingine nyingi tu ambazo sio suitable kwa watoto wadogo..kama zipo rated bora hao wanaozileta hewani wa wawahabarishe watu ili wajue nani kwenye familia hapaswi kutizama
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwa ujumla uangaliaji wa TV ni sumu mbaya sana kwa maendeleo ya watu especially wanafunzi.zinaharibu Academic life ya mtu.Ni vizuri wazazi wawe wakali kwa hili kwa watoto wao.Jaribuni kuwazuia wasiangalie badale yake wasome.Mtoto ukimuendekeza unamuharibu.acheni kuwapa upendo wa kijinga watoto.
  Hili pia ni hata watu wazima,tupunguze jamani kupoteza muda kuangalia tv zinadumaza akili,badala yake tusome vitabu jamani vinalipa!
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  kuna tamthilia moja inaitwa Ruby capital Televison ila huyo sterring mwenyewe anatabia za ajabu ajabu kweli kweli
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii kweli kabisa wazazi wanatakiwa wawe wakali kwa watoto wao, kama haiwezekani wawapangie vipindi vya kuangalia.
  Kuna baba mwenye nyumba imebidi afungie tv yake chumbani kutokana na kero alizokuwa anapata kutoka kwa mabinti zake ambao walikuwa wanapenda sana tamthilia. Hivi sasa wapangaji ndio tunapata taabu kutoka kwa hao watoto kila inapofika mida ya hizo tamthilia, nyingine zinaenda hadi saa sita usiku kama zile za kikorea zinazoonyeshwa usiku sana. Hii ni kero!!!!
   
 11. A

  AM_07 Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mimi nilikuwa napenda sana tamthilia ya zombe, sasa naangalia ya liyumba na akina mramba, ila sio bomba kama ya zombe!
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Na ya Sofia Simba haikuvutii
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160

  Binti wa Zion,Kama reli ni Kigoma,Mlima ni kilele cha Knjaro.UMEGONGA BUTTON yenewe
   
Loading...