Tamthilia kali kuliko zote bongo. Hii ndiyo kiboko ya bongo movie, lazima uipende

Aug 2, 2020
1
0
TAMTHILIA: CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL)
(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA MAISHA YANGU)
MWANDISHI/MTUNZI: MANSHYNE
Email address: manshinef@gmail.com
instagram: @manshynee

Sehemu ya 01.

DARASANI:
Ilikua ni muda wa kipindi cha ujasiriamali kwa Wanafunzi wanaosomea kozi ya biashara. Lecturer (Mwalimu wa Chuo) alikuwa mbele ya Darasa akifundisha. Kutokana na ukali wa Mwalimu huyo, darasa lilikua kimya sana.
Frank akiwa mmoja wa wanachuo, alikua makini sana kusikiliza. Ilifikia hatua alitikisa kichwa juu chini kuonyesha namna ambavyo alikua anaelewa katika kipindi hicho. Wakati kipindi kikikaribia kuisha, Mwalimu aliuliza swali;

MWALIMU: Wanafunzi, nani anapenda kuwa mfanyabiashara? kwanini? Na mtaji utaupata wapi?

(binti flani aitwaye Loveness alinyosha mkono, aliambiwa ajibu swali. Love alisimama kisha alijibu)

LOVENESS: Mimi sipendi kuwa mfanyabiashara kwa sababu biashara zina hasara nyingi, ni ngumu kupata mtaji kwa sababu watu wengi wanaitaji fedha na fedha ni ngumu kupatikana.

(Kabla mwalimu hajaongea chochote aliona mkono wa Frank.)

MWALIMU: Eeh! nawe una jibu jipya? Ebu tupe jibu lako.
FRANK: (Baada ya kusimama) Mwalimu nataka nimjibu Loveness. Love, unaposema hupendi kuwa mfanyabiashara una maana gani? Na kama hupendi tuambie kwanini unasomea biashara?
LOVENESS: Mfanyabiashara ni sawa na mtu aliyejiajiri, sasa mimi nikijiajiri kuna faida gani za kusoma? Si nitakua nimepoteza fedha zangu. Sasa si bora ningekaa nyumbani na hizo fedha za ada ningezitumia kama mtaji. Nasomea Biashara kwa sababu Serikali itanipa ajira zinazohusu usimamizi wa biashara za wananchi.
FRANK: Hapana, kumbe una mawazo finyu hivyo?...Tena wewe mwanachuo wa elimu ya juu unaweza ukatupatia majibu kama hayo? hata hiyo Serikali haiwezi ikakuamini kwa sababu huwezi kuongoza wafanyabiashara wakati hupendi biashara.
LOVENESS: Kwani tatizo lipo wapi? Jamani kila mtu ana ndoto zake. Humu ndani kuna watu wanawaza kujiajiri na kuna wengine akina sisi hatuna mpango huo. Mimi nachoamini ni kwamba baada ya kuhitimu chuo, kinachofuata ni kusubiri ajira tu. Pia naamini kuwa nitaajiriwa. Siwezi kupoteza muda wangu na fedha zangu bure! hata wale wenzangu walioko uko mtaani si watanicheka?
FRANK: Loveness, kwanza serikali ni nini? Unataka kusema Serikali haifanyi biashara? Hivi hujawai kusikia Serikali inanunua au kuuza vitu kutoka nje? Tena ni juzi tu tulimaliza mada ya biashara za kimataifa (international trade), unataka kusema ile mada hukuilewa au?
LOVENESS: Kwanza wewe unataka nini? Kama unaona jibu langu sio sahihi basi tupatie jibu lako. Kwa sababu naona unapinga sana mawazo yangu. (aliongea akiwa na hasira alafu aliamua kukaa chini)
FRANK: Haina haja ya kukasirika kwa sababu swali liko wazi kwa sisi wote ambao tunachukua kozi ya biashara. Mimi sijamaanisha kwamba sitaki kuajiriwa au sijamkataza mtu kuajiriwa, ila kutokana na swali majibu ya dada yetu Love sidhani kama ni sahihi. Mwanachuo aliye kamili kifikra hawezi kutujibu majibu kama hayo....

(Kabla Frank hajamaliza kuongea Loveness alisimama akiwa amefura kwa hasira na jazba)

LOVENESS: Kwahiyo mimi sina fikra, sifai kuwa mwanachuo, unaamua kuni…. (kabla hajamaliza kuongea alianza kulia kwa kwikwi kisha alitoka nje ya darasa pasipo kugeuka nyuma)

(Baada ya tukio hilo kulitokea ukimya mzito, wanachuo walikausha kimya. Kuna watu walimuonea huruma Love, wengine waliona ni jambo la kawaida. Frank bado alisimama, alitaka kukaa lakini alisimamishwa na mwalimu, aliambiwa ajibu swali kwa faida ya wengine)

FRANK: Mimi napenda kuwa mfanyabiashara, hata kama ikitokea nikapata ajira selikalini; sitoacha kufanikisha ndoto zangu za kuwa mfanyabiashara. Na ndio maana niliamua kusomea kozi hii. Napenda biashara kwa sababu inapatikana kila sehemu. Biashara ipo kwenye sekta za umma hata sekta binafsi. Kuwa mfanyabiashara kuna faida nyingi; kwa mfano uhuru wa maisha, uhuru wa maamuzi, pesa zisizo na kikomo na faida nyinginezo. Biashara inatengenezwa na bidhaa pamoja na huduma za kijamii. Na ndio maana hata serikali inatengenezwa na biashara. Kuhusu mtaji ni rahisi tu, kuna mikopo kutoka benki na mashirika, akiba binafsi, misaada toka kwa watu wa karibu (familia na marafiki), wadhamini na kadhalika.
MWALIMU: Safi sana, nadhani hakuna hasiyekuelewa, hii inaonyesha ni jinsi gani una upeo wa kielimu hasa katika kozi yako ya biashara. Darasa tutaonana kipindi kijacho. (Mwalimu aliondoka darasani).

Baada ya Mwalimu kuondoka, huku nyuma kulisikika minong'ono na mijadala kuhusu yaliyotokea, kuna waliosema Frank amekosea sana kwa kumdhalilisha Loveness, wengine walisema Frank ameongea sahihi. Ilikua ni kelele tu, kila mtu aliongea neno lake.

Wanachuo walitawanyika, walielekea hosteli. Ndani ya darasa alibaki Frank pekee. Ilikuwa ni mida ya saa sita mchana, aliona bora ajisomee akisubiri muda wa chakula cha mchana. Alitoa daftari na peni kisha alianza kupiga pindi. Hakutaka kuwaza sana kuhusu kilichotokea kwa sababu aliona ameongea vitu ambavyo mtu yeyote angeweza kuongea. Akiwa anajisomea mara aliingia mdada flani hivi aitwaye Maria.

MARIA: Frank vipi? mbona umebaki peke yako humu ndani?
FRANK: Nimeamua tu, nimeona nikiwa nasubiri muda wa msosi niwe napitia pitia kidogo.
MARIA: Hivi una taarifa kuwa mwenzio kapelekwa hospitali?
FRANK: Mwenzangu gani?
MARIA: Loveness. Baada ya kususa kipindi alikimbilia hosteli akiwa analia. Sie tumetoka kipindi, tumefika hosteli tumekuta mtu kazidiwa, ilibidi tumuwahishe hospitali ya chuo.
FRANK: (Akishangaa) Eeh! lakini si alikua poa tu!! amezidiwa kwa tatizo gani?
MARIA: Hospitali wanasema alizidiwa na maumivu ya kichwa. Na inasemekana kuwa chanzo ni wewe!

Frank alikodoa macho, alishindwa kuelewa! Balaa zitoooo!!!

IMEANDIKWA NA MIMI FRANK TITUS KAPINGA. INSTAGRAM NATUMIA JINA @MANSHYNEE

MAWASILIANO: 0743857349 WASAP INAPATIKANA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom