Tamthilia: Challenge - Sehemu ya 2

winnie9999

Member
Nov 27, 2021
65
102
TAMTHILIA: CHALLENGE MADE
SEHEMU: 2
MUANDISHI: WINIFRIDA FRANCIS THOBIAS

Jackbosi alishangaa sana kumuona mtu anaefanana nayeye katika hospitali ambayo yeye pamoja na washirika wenzie wamekuwa wakifanya uchafu wao, Jackbosi alitamani kumuuliza maswali mengi sana grace lakini muda haukuwa rafiki kwasababu tayari mtoto alikuwa ameshaanza kutoka tumboni mwa grace hivyo Jackbosi ilimbidi awafukuze walinzi wote kisha amsaidie grace kujifungua na kwabahati nzuri grace alifanikiwa kujifungua salama na kupata mtoto wakike jambo ambalo lililomfanya grace atabasamu nakusahau shida zote alizokuwa akipitia wakati alipokuwa amebeba ujauzito wa mtoto huyo.

Jackbosi alimsafisha mtoto huyo na kumwambia grace hongera umepata mtoto wa kike, grace alimuangalia Jackbosi kwa hasira na kumwambia huyo mtoto unauhakika ni wangu ?. Jackbosi hakumjibu chochote grace alichofanya ni kuamuru walinzi wamchukue mtoto wampeleke hodini na grace apelekwe ofisini Kwake kwa mahojiano zaidi . Lakini Kabla ya Jackbosi kufika ofisini kwake na grace simu ya Jackbosi iliita na aliye kuwa akipiga alikuwa anaitwa Mr.Kivuli ambae huyo ndo msimamizi wawanachama wote wanaoshirikiana kuendesha shuhuli zote zinazo fanyika hospitalini hapo. Jackbosi aliongea na Mr.kivuli faragha na alipomaliza kuongea na simu aliwaambia walinzi wake waongozane nae pamoja na grace kuelekea hodini ataongea na grace atakaporudi kwasasa anahitajika kwenda kufanya jambo muhimu.

Lakini kabla hajaondoka Jackbosi alienda kuwaambia wakinamama wote hodini akiwemo grace kuwa atakae jalibu kutoroka wakati huu sitamuua yeye tu bali wote mtakufa kwenye mikono yangu kumbukeni hilo. Wakina mama wote walijenga chuki na grace kwani waliamini kama sio yeye kujalibu kutoroka jasmini asinge kufa lakini pia vitisho visinge kuwepo kila wakati . Hata hivyo grace huwa hajali kabisa kutengwa na wakinamama hao kwasababu sikuzote wamekuwa wakifanya hivyo japo grace hakuwa anajua nini haswa kiliendelea hodini alipo kuwa akijalibu kutoroka, mpaka pale ambapo Ade alipo muuliza mlinzi kama watapata nafasi ya kumzika jasmini na mlinzi akamjibu ucjali kuhusu yeye ameshakufa jali kuhusu wewe ambae kama si leo ni kesho utakuwa umekufa ' kisha mlinzi alicheka sana na kuondoka zake.

Wote waliogopa sana lakini mwanamke mmoja kati yao aliuliza 'hivi inawezekanaje jasmini apigwe risasi halafu tusione damu hata tone baada ya mwili wake kuondolewa pale' ?, Ade aliwaambia kwa hasira hayatuhusu tufanyeni kazi zinazo tuhusu kama vile kuhakisha tunajifungua salama na kukabidhi watoto wakiwa hai la sivyo chakula hatuta pata na ndugu zetu wataisha wote.wakinamama walinyamaza nakumtupia maneno ya lawama grace japo grace hakuonekana kujali chochote na ndio kwanza alijifunika kwa shuka lake na kuwaambia 'mda wenu wakutamba huwa ni mchana na ndio maana nyie niwaongeaji sana na usiku mnakuwa mmechoka sana lakini mimi usiku ndio muda wangu mzuri nandio maana nawekeza akili yangu yote mchana ili usiku niwe macho kwaajili yenu wote' .

Ade alimuangalia sana grace nakuongea moyoni mwake ya kuwa 'grace Leo haijalishi nini kitatoke lakini lazima tutatoka wote kwasababu natamani kujua kwanini ulinishawishi kuja hapa halafu unaonekana haujali kabisa kuhusu mimi'.

Jackbosi alipo kuwa njiani akielekea kwa Mr.Kivuli simu yake iliita na alipo pokea Mr. Kivuli alimpa kazi ya kwenda airport kumpokea muwekezaji wao mpya, Jackbosi alimwambia Mr.kivuli sawa nimekuelewa na hapohapo akampa amri mlinzi wake ageuze gari waelekee airport. lakini chaajabu wakati Mlinzi wa Jackbosi anabadili muelekeo wa gari yao ili waelekea airport kumpokea muwekezaji mpya gari iliyo kuwa nyuma yao nayo ikaonekana kuwafuatia kwa nyuma na alipokuwa akipunguza mwendo nayo pia ilipunguza mwendo kama wao, Jackbosi alipata hisia mbaya alihisi pengine ni wapinzani wenzao wa kibiashara hivyo aliamuru gari isimamishwe kisha akachukua bunduki yake nakuweka risasi pia akawaambia walinzi wake Msitoke nnje ya gari kisha yeye akalifuata gari lile kwani nalo lilisimama baada tu ya gari ya Jackbosi kusimama.

Jackbosi aliwasogelea na kuwanyooshea bunduki lakini alipo waangalia watu waliokuwa ndani ya gari hiyo aligundua wote ni wazee hivyo alipasua tu magurudumu ya gari Lao kwa bunduki bila kuongea chochote na kuwafanyia chochote kisha akarudi kwenye gari yake kuelekea airport. baada ya magurudumu ya wazee hao kupasuliwa kwa bunduki waliwasiliana na mtu na kumpa taarifa ya kilicho tokea haikupita mda pikipiki nne zililetwa kwaajili yao na hapo ndo safari yao ikaamza rasmi tena kumfuata Jackbosi kwani kwa namna yeyote ile Jackbosi anahitajika na bosi wao.

Jackbosi alipofika airport alimpokea muwekezaji kwa heshima na kumuomba aongozane na mlinzi wake yeye kunamajukumu muhimu anahitajika kuyafanikisha , muwekezaji alikubaliana nayeye kwani hata hivyo mkutano wa uwekezaji ulikuwa siku inayofuata na yeye alihitaji kupumzika kwani alikua amechoka sana na safari, Jackbosi alimpakazi moja ya mlinzi wake ampeleke muwekezaji huyo nyumbani kwake yeye ili na yeye akaongee na grace.

wakati mlinzi wake anaanza safari ya kumpeleka muwekezaji huyo nyumbani kwa Jackbosi na Jackbosi naye alianza safari kuelekea hospitalini akiwa katikati ya safari ghafla mbele yake alishtuka kuona pikipiki nne mbele ambazo zilimzuia yeye kuendelea na safari yake , Jackbosi alimuamuru mlinzi wake asimamishe gari kisha akatoka nnje kuwafokea kwani alihisi ni watu wanaojifunza kuendesha pikipiki kwenye Barabara kubwa na kama kawaida yake aliwaambia walinzi wake wasimfuate. Alipokuwa akikaribia pikipiki hizo madereva wa pikipiki wote walivua kofia za pikipiki na hapo ndipo jackbosi aligundua ni walewale wazee aliowadharau awali na hapo ndipo aliona kumbe wapo serious hivyo moja kwa moja aliwauliza 'mnataka nini kwangu' ? , lakini hawakumjibu walimpiga na kitukizito kichwani na palepale akapoteza fahamu kisha watu hao wakampigia bosi wao simu kumjulisha kwamba kazi imeisha. Chakushangaza zaidi ni kuwa walinzi wa Jackbosi nao walikuwa pamoja na watu waliomteka Jackbosi kwani baada ya Jackbosi kupoteza fahamu wao walili sukuma gari la Jackbosi sehemu ambayo mtu hawezi ona kisha wakafuatana na watekaji tena wakiwa na furaha.

Mida ya saambili kama kawaida grace aliiba mavazi ya mlinzi kisha akavalia kama mlinzi na akambusu mtoto wake kisha akawaambia wakinamama usiku mwema na nisameheni kwasababu nafanya hivi kutokana na nyie hamuwezi kufunga midomo yenu, wote walimuangalia kwa hasira lakini grace hakujali alitoa dawa mfano wa vumbi na kuwapulizia wote na hapohapo wakapitiwa na usingizi mzito kisha akawalaza vizuri na kuanza kutoka nnje na kila alipopita safari hii alipuliza dawa nakupiga kamera za ulinzi risasi kisha akachukua pikipiki inayotumikaga kuchukua mahitaji muhimu ya hospitalini na alipofika Getini alifunguliwa geti bila kikwazo chochote kwani alikuwa amevalia kofia ya pikipiki pamoja na Miwani hivyo ilikuwa ngumu walinzi kujua ni grace na kabla ya kutoka aliwapulizia dawa walinzi wa Getini kisha akatoka nakufunga geti ili watakapoamka wasihisi kitu chochote kibaya.

Alipo toka tu Getini na pikipiki alienda nayo umbali mdogo tu kisha akaificha sehemu ya msituni kidogo na yeye akaanza kutembea kwa miguu umbali kidogo tu kisha mbele yake kulikuwa na Magari manne ya kifahali na walinzi wasiopungua Kumi na wote baada ya kumuona grace waliinamisha vichwa vyao chini na kumwambia grace unaendeleaje bosi.

* End **

USIKOSE KUSOMA SEHUMU YA 3 HAPO KESHO ILI UWEZE KUJUA JE GRACE NI NANI ? NANI KWANINI ANAONEKANA NI MTU MZITO MWENYE PESA ZAKE LAKINI BADO YUPO NDANI YA HOSPITALI YENYE MATESO KIASI KILE? NA JE JACKBOSI KWANINI KATEKWA PIA KWANINI YEYE ANAFANANA SANA NA GRACE ? NA JE KUNA KAZI GANI GANI INAYOFANYIKA HOSPITALINI AMBAYO WATU WA N'JE HAWATAKIWI KUJUA ?
ASANTENI SANA.
 
Fanya kuzionganisha na ile sehemu ya kwanza
 
Sehemu ya kwanza tutaipata wapi?
 
Jitaidi sasa kuwa unatupia ata vipande viwili kwa siku sio kila siku kipande kimoja kimoja
 
Iko vizuri Sana ila fupifupi Sana halafu neno ...END... Sijajua kwa Nini unalotumia wakati unaenda kipande kinachofuata?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom