Kaka tuna-tatizo la kimfumo... lakini kwa bahati mbaya sana tunadhani tunaweza kutibu ukimwi,,, kwa kutibu magonjwa nyemelezi... Mdahalo ni mzuri sana kwa jamii inayoelewa mdahalo ni nini? Sio hii ya kwetu mkuu... well!! Ni muhimu sana uelewi simtetei Kikwete kwenye hili la mdahalo maana anatakiwa asimame mwenyewe kwa kuwa urais anataka yeye... najua anakwepa kwa sababu ni mdhaifu upande huo... tena sana, maana hata pale anapoongea mwenyewe unaona kabisa si mjuzi wa kupangilia hoja zake....
Lakini ukweli unabaki pale pale... mdahalo mzuri but not the only choosing criteria.
Mimi Mtanzania Huru Bwana... na Huenda nisiwe mwanachama wa chama chochote Daima... kwa mfano... chama kinachoamini cheo cha makamu wa Rais ambacho kimetajwa kwenye katiba ni cheo cha mchezo siwezi kuchukua kadi yao of course. CCM pia sijadhirika nayo ndio maana sina hata chembe ya documents zao ... only msomaji mzuri wa ilani za vyama.
Interestingly nchi haiendeshwi kwa matakwa ya mtu binafsi, nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria. Therefore sioni kitakachomshinda mtu mwenye akili timamu kuiongoza nchi.
Kasheshe kwa bahati mbaya hatutafuata standards zako katika hili tunaongozwa na the letter of the constitution.
Hebu niambie ni kipi ambacho Dr. Shein alikuwa anakifanya katika position ya umakamu wa rais ambacho mtu kama mgombea mwenza wa CHADEMA hawezi kukifanya.