Tamko rasmi la Dr. Slaa kuhusu CCM kustisha midahalo TBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko rasmi la Dr. Slaa kuhusu CCM kustisha midahalo TBC

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 10, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dr. Wilibrod Slaa amesema; Uamuzi wa CCM kukataza wagombea wake kushiriki midahalo ya kisiasa ni aibu kwa mwelekeo wa demokrasia nchini. Kiongozi anayetaka nafasi ya kisiasa anayekwepa nafasi ya kuzungumza na wananchi anaotaka kuwaongoza na anataka kuwahubiria tu ni mwoga na hafai kuwa kiongozi wao. Chadema tuko tayari wakati wowote na mahali popote kujadiliana na mtu yeyote wa chama chochote.

  My take: Kwanini uogope kukutana na wananchi unaowaomba kura?

  Dr. Wilbrod Slaa 2010
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,500
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu mpaka kieleweke!!!!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi naona CCM wako sahihi. Kwa nini upeleke watu wako kwenye TV ili waumbuke? Wanajua kuwa wanayo maswali mengi sana ya kujibu na hawana majibu ya kuridhisha. Kwa maana hiyo ni sawa tu kuamua kukwepa hicho kitimoto.

  Tatizo liko kwetu wananchi kwani hilo lilitakiwa kuwa sababu ya kutosha kutowapa nafasi nyingine hadi watakapokuwa tayari kuongea na sisi.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mdahalo ni ngumu. Mathalani Jimbo fulani miaka mitano iliyopita shida kuu ilikuwa ni maji, hadi sasa hukuweza kuwaletea maji, unarudi unawaahidi wakikuchagua tatizo la maji litakuwa historia, Je unafikiri hao wanaoelezwa hivyo wakipewa fursa ya kuuliza maswali majibu yatapatikana?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nadhani CCm WATATUMIA NAFASI HII kucopy&Paste sera za vyama vingine ili na wao wazitumie kwenye mikutano yao, ndio sababu kubwa ya kusepa!
   
 6. k

  kakakuonap Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ingelikuwa uwezo wa kukariri ngonjera na kutapika mbele za watu kwa staili ya mdahalo ndio kigezo cha kuwa kiongozi wa watu basi kiongozi wa kwanza angekuwa Shehe Mtopea, Rev. Mtikila n.k Ila Uongozi una vigezo vingi kama vile uadilifu, ukweli, elimu, kukubalika na watu , mapenzi yako kwa watu. JEE TUKIANDAA MDAHALO SUALA LAKO LA NDOA LIKIULIZWA UTALIJIBU!!!!! . Tusubiri Oktoba 31 ndio siku ya mdahalo mzuri.
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kutoa hii sentensi inahitaji mtu aliyejiandaa haswa, nakumbuka kama sikosei kauli kama hii ilishawahi kutolewa wakati fulani na Kingunge alipokuwa anajibu wito wa Mkapa wakati huo kushiriki mdahalo kwenye uchaguzi wa 1995, CCM wamezipeleka wapi hizo guts.
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  mdahalo kujadili ndoa ya mtu mmoja?nani ana nafasi hiyo?manake mi ntabadili channel niangalie michezo au mapishi niboreshe ya kwangu.wenzio tunaongelea maslahi ya nchi hii ndugu.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  dr slaa aendelee kujieleza sera za jinsi gani ataleta ukombozi.hizo habari ambazo hazina manufaa kwa taifa awaachie ccm manake wana jipya lipi la kutuambia tena?manake yote walishaahidi toka enzi.waseme tu 'as above' au ze same to you waendelee na ngoma zao.alaaaaa:mad2:
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
 11. P

  Pokola JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mwenye dhambi hukimbia, hata asipofuatwa na mtu. CCM wana dhambi, ndio maana wanakimbia.
   
 12. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Si lazima kuchangia kila post. Kama hujui kinachoongelewa ni bora kukaa kimya soma post za wengine ujifunze.
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Natinal standard unit ya ccm ni Makamba, hivyo basi kwa kuwa Makamba anajijua uwezo wake wa kujibu maswali na kujenga hoja ni kwanini asiwazuie makada wenzake kujiaibisha mbele ya jamii?
  Jingine ni ccm wameamua kwa makusudi kuifanyia taaluma vurugu na kuufanya ujinga wa watanzania walio wengi kuwa mtaji wao wa kisiasa.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wapo wengi hawa kazi yao ni kujaza upupu hapa na kwenda kusign check kwa Makamba!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Enzi zile kauli kama ilikuwa kama hii iliweza kutolewa na CCM, lakini leo hii wameweka mpira kwapani na kutimka!
   
 16. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Juu ya hili hata mm limenishtua, sijui kuna nn maana sababu zilizotolewa na Katibu wetu hazijaniridhisha.


  kwenye mijadala ndio tungeweza kuwaonyesha hawa ambao CCM haijafanya kitu kuwa imefanya na kuwapa muda wananchi kuelewa nn CCM imefanya na imepanga kuwafanyia

  pia ingesaidia kuondosha na kuua kabisa kasumba na propaganda za wapinzani


  nnarejea sijui kuna nn ambacho hakijaelezwa ambacho ni zaidi ya kilichoelezwa(hata hivyo nnaamini busara za chama zilitumika )
   
 17. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu wa nchi anayembea na msafara wa magari ya zaidi ya Tsh Bil moja zilizo kodi za mwenyenyumba hii, anamwahidi tena kwa mara nyingi ikiwa atamrudisha katika ulaji kwa kura yake atamkumbuka kwa kumnunulia baiskeli ya miguu mitatu (Bajaj) ili aitumie kwa mkewe kama ambulance ya kumpeleka clinic wakati wa ujauzizo. DOUBIOUS!!!
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unajua Mzee Mwanakijiji dawa ya tatizo si kulikimbia ni kuli face kama wamekimbia huoni wameongeza tatizo jingine, kweli kuna wakati timu za Simba na Yanga zikiona upepo si mzuri huwa wanatia mpira kwapani lakini ndiyo hukaribisha matatizo zaidi klabuni, labda CCM wameona heri fedheha kuliko udhia.
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  You sound a bit like a comedian broda!...!

  Hapo nimecheka mpaka basi, maana unatusaidia kushangaa malimwengu ya MAKAMBA!
  Ndugu yangu huyo mtu wenu nadhani anatokea sayari mpya ya Kleptomaniac!...huh!
  Wewe MTU WA PWANI UNAONEKANA NI MWANAMAGEUZI KABISA ILA UNAHOFIA MACHO NA MANENO YA WAYAHUDI!
  Achana nao hao SISIEM broda, hamia hii ng'ambo ya pili ili upambanue mambo kwa akili!...huh!
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wewe una matatizo makubwa, kama ni msomi basi basi umitia hasara familia yako kama haya ndiyo maono yako ya kwamba uandaliwe mdahalo wa kujadili ndoa si kujadili kwa kina kwamba kwa nini tumeshindwa kufikia japo robo ya ahadi zza utawala unaoondoka madarakani na kujadiri kero za wananchi ebooo, kumbe kina makamba mko wengi hata humu ndani, kwani mambo ya kuyajadiri yamekwisha mpaka tujadiri ndoa za watu ambazo hazina faida kwa taifa zaidi wanandoa na wenyewe kwa wakati maalumu?
   
Loading...