Tamko Rasmi Chadema Juu ya Tukio la 15.06.13

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Mh. Mnyika anasema kuwa:

1. Lukuvi amesema uongo huku akijua ukweli
2. Polisi ndio waliotupa Bomu na kumtorosha mhalifu.
3. Hao wanaotetea Polisi ndio wanaowatumia Polisi kufanya mauaji.
4. Wakati wa maombolezo CCM wanafanya Propaganda kama vile waliokufa kwenye mkutano wa Chadema si Watanzania.
5. Tamko hili limelazimika kutolewa sasa kukanusha UONGO ambao kukiachwa utaonekana ni ukweli.
6. Wauaji wawajibishwe
7. Hakuna Serikali inayoendelea kudumu madarakani kwa kumwaga damu
8. Chadema tuendelee kutetea Amani huku tukiendelea kudai haki.

Sehemu ya Tamko la Mh. Mnyika Juu ya Propaganda za CCM wakati wa Maombolezo - Tukio la Bomu Arusha.

a. UZITO WA KAULI YA LUKUVI.
Mwenyekiti Mbowe alizungumza jana, na wakati anaeleza ushahidi uliopo, na ushuhuda uliopo juu ya tukio hili, ameeleza vilevile kushangazwa na kauli za Waziri Lukuvi. Kwa hiyo katika nukta hii, tuongeze tu baadhi ya mambo ya msingi, ikizingatiwa kuwa waziri Lukuvi ni Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge. Kauli yake, akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, inamaanisha ni Ofisi ya Waziri Mkuu imezungumza Bungeni.

b. LUKUVI AMESEMA UONGO HUKU AKIJUA UKWELI
Kauli ya Lukuvi inapaswa kubebwa kwa uzito mkubwa, na kwa kauli hiyo imedhihirika kwamba ni sera ya serikali kusema uongo, huku ikijua ukweli. Kauli yake imedhihirisha kwamba, jambo hili la kutaka kulidanganya Taifa, lina uratibu wa serikali kwa ujumla wake. Kama Waziri wa Uratibu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu ndiye Mkuu wa shughuli za serikali bungeni) anaweza kutoa uongo wa namna hiyo, maana yake kauli hizi zimeratibiwa, na hivyo serikali bungeni imepoteza uhalali wa kimaadili (moral authority) wa kuzungumza, kwa sababu imeratibu uongo wa moja kwa moja.

c. ASKARI WA FFU ALITUPA BOMU NA ALITOROSHWA NA ASKARI WENZAKE
Kauli ya Waziri huyu iturudishe nyuma tu. Wakati anazungumza kwamba polisi walishindwakumkamata mhalifu kwa sababu eti wananchi wamechochewa muda mrefu na hivyo kulichukia jeshi la polisi kwa kiwangu cha polisi kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kumkamata mhalifu, wakati ukweli wa mikanda tuliyo nayo unaonyesha kuwa polisi ndio ambao waliamua kumtorosha mhalifu.

Sio tu kumtorosha kwa magari, bali kwa matumizi ya bunduki na bastola kuwapiga risasi wananchi waliokuwa wanafanya ulinzi shirikishi wa kuelekea kumkamata mhalifu waliyemwona, kwa sababu tu mhalifu huyo amevaa mavazi ya FFU, kwa sababu tu mhalifu huyo ni mwenzao. Polisi hawa wakatekeleza uhalifu mwingine wa kupiga raia risasi ili kulinda uhalifu. Jeshi la namna hii haliwezi kutetewa.

d. WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye ndani ya jimbo lake alituhumiwa bungeni kulitumia vibaya jeshi la polisi, kumtumia vibaya Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda. Lakini Lukuvi aliposimama akaenda mbele zaidi, sio tu ndani ya jimbo lake, akafikia hata hatua ya kumkingia kifua Michael Kamuhanda, ambaye ripoti ya tume ya haki za binadamu na utawala bora inamhusisha moja kwa moja na kusimamia opereshein iliyosababisha mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi.

Kama ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na serikali ni wazi yamepangwa na serikali.

e. SERIKALI, CCM WANAFANYA PROPAGANDA BADALA YA KUTOA NAFASI YA MAOMBOLEZO .
Sote tuna majonzi, sote tunaomboleza. Ni bahati mbaya kuwa serikali, CCM na bunge, badala ya kutoa nafasi kwa maombolezo, wakati ambapo hatujawazika wenzetu, wakati ambapo tuko katika kipindi cha maombolezo, wao badala ya kuomboleza wanafanya propaganda.

f. TAMKO HILI LINAKUJA SASA KUKANUSHA UONGO.
Tumelazimika kuzungumza jambo hili badala ya kuzungumzia majeruhi, ambao wapo hospitali na tunaendelea kuwahudumia mpaka sasa, badala ya kuzungumzia marehemu, ambao lewa wanapewa heshima, wengine watapewa heshima kesho, tumelazimika kuyazungumzia haya kwa sababu UONGO UKIACHIWA, UKASEMWA, UKASEMWA, UKASEMWA, watu wanaweza kuamini kwamba ni ukweli. Lakini ni wazi, UKWELI UKISEMWA WATU WACHACHE WANAWEZA KUDANGANYIKA KWA MUDA MFUPI SANA, LAKINI SIO WATU WOTE KWA WAKATI WOTE.

Watanzania tusikubali kudanganyika, kwa pamoja tuungane katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tuendelee kusimamia UKWELI, kuueleza UKWELI.

g. WAUAJI WAWAJIBISHWE.
Lakini baada ya kipindi hiki cha maombolezo kwa mauaji kama haya na mauaji mengine ambayo yametokea muda mrefu katika taifa letu, ni lazima tufike hatua tuseme hapa imetosha. Ifike hatua tuseme, waliohusika na mauaji haya, si tu yaliyotokea Arusha Juni 15 mwaka huu, bali waliohusika na mauaji ya kuanzia yale ya Arusha Januari 5 2011, na mauaji yaliyofuatia baada ya hapo: mauaji ya Igunga Mwezi Oktoba 2011 ya Marehemu Mbwana Masoud, aliyekutwa ameuawa na kutupwa. Mauaji yaliyofuata Arumeru, alipochinjwa kiongozi wa Chadema Marehemu Mbwambo aliyechinjwa kwa msumeno, na baadaye askari Polisi wakadiriki kumtorosha mtuhumiwa huyo mahakamani na mpaka leo hajapatikana, na mauaji yote yaliyotokea baada ya hapo, ifike hatua tuseme sasa imetosha.

Ifike hatua tuiwajibishe serikali, ambayo baada ya kushindwa kubaki madarakani kwa kuwatumikia wananchi, baada ya kushindwa kubaki madarakani hata kwa kutumia ufisadi na rushwa, kutoa rushwa kwenye chaguzi, lakini wananchi bado wanakubali mabadiliko. Baada ya kushindwa kung'ang'ania madarakani kwa siasa za UONGO, SIASA CHAFU ZA PROPAGANDA ZA UDINI, UKABILA n.k., sasa wanafikiri kwamba wanaweza kung'ang'ania madarakani kwa UMWAGAJI WA DAMU.

h. HAKUNA DOLA ILIYODUMU KWA KUMWAGA DAMU YA RAIA WAKE.
Historia ya dunia inaonesha kuwa hakuna dola iliyokataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, kwa nguvu ya umma, ikafanikiwa kubaki madarakani kwa kutumia askari, kwa kutumia umwagaji damu. Tanzania tunapita njia hiyo. Tusielekee huko.

i. CHADEMA TUTETEE AMANI HUKU TUKIDAI HAKI.
Sisi Chadema tunapenda amani ya nchi yetu, tutaendelea kutetea amani ya nchi yetu. Lakini hatutarudi nyuma katika kudai haki. Haki za sisi tunaoishi, haki za waliokufa na haki za watakaokufa. Hatutaacha, kwa sababu tukifanya hivyo itakuwa ni usaliti kwa imani kubwa ambayo wananchi wameipa Chadema.

(Vichwa vya habari ni mimi nimeweka kwa kurahisisha kusoma tamko).
 
Last edited by a moderator:
This is politics tu hakuna kitu. Kama mharifu ni ccm wapeleeni huko The Hague washitakiwe. Cdm pia mnawadis saana vijana wa polisi wakati mnajua kazi yao ni kutekeleza amri tu. Mnawakosesha raha hawa polisi. Wafuateni wansowatuma.
 
Ndio maana ya sehemu hii:
WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye ndani ya jimbo lake alituhumiwa bungeni kulitumia vibaya jeshi la polisi, kumtumia vibaya Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda. Lakini Lukuvi aliposimama akaenda mbele zaidi, sio tu ndani ya jimbo lake, akafikia hata hatua ya kumkingia kifua Michael Kamuhanda, ambaye ripoti ya tume ya haki za binadamu na utawala bora inamhusisha moja kwa moja na kusimamia opereshein iliyosababisha mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi.

Kama ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na serikali ni wazi yamepangwa na serikali.

Sasa ni wazi CHADEMA inahitaji wananchi waliozinduka ili iendelee na harakati za kuikomboa nchi hii.ni wakati ambao watz wanapaswa kuchagua moja kwa kuwa kila kitu kiko wazi.watz tukiendelea kulala kama vile vyama hivi vina malaika ambao hawachoki kutetea,vitakufa na hawa mafisadi wataendelea kutukandamiza na mimi nasema ikiwa hivyo watastahili kutukandamiza na tusilielie tena,tukae kimyaa!
 
Chadema mnazidi kutukatisha tamaa.yaani mnathubutu kutulupua kisha mnajifanya kuongoza mazishi.hayo ndio mafunzo mliyopewa na CDU ili kuwaaminisha wananchi kuwa serikali yao haifai?shame on you!
 
Chadema mnazidi kutukatisha tamaa.yaani mnathubutu kutulupua kisha mnajifanya kuongoza mazishi.hayo ndio mafunzo mliyopewa na CDU ili kuwaaminisha wananchi kuwa serikali yao haifai?shame on you!

only a simple,poor minded person can argue cheaply like this..
 
Chadema mnazidi kutukatisha tamaa.yaani mnathubutu kutulupua kisha mnajifanya kuongoza mazishi.hayo ndio mafunzo mliyopewa na CDU ili kuwaaminisha wananchi kuwa serikali yao haifai?shame on you!
Wana ushahidi wa wazi wa video, ndio maana wanaongea kwa kujiamini.

Hapo hamna propaganda, video imeshakabidhiwa kwa makamishna toka makao makuu.
 
Chadema mnazidi kutukatisha tamaa.yaani mnathubutu kutulupua kisha mnajifanya kuongoza mazishi.hayo ndio mafunzo mliyopewa na CDU ili kuwaaminisha wananchi kuwa serikali yao haifai?shame on you!
Chadema sio chama cha siasa bali ni chama cha vurugu
 
Polisi ni kama mbwa tu wanaoamrishwa kuuma!!! Mwenye mbwa ndiye anayefahamu kisa na mkasa wa mbwa wake kuuma!Tusikomee kuwalaumu sana polisi tu! Mwenye mbwa yupo... Kikwete ndiye mratibu wa shughuli zote za mabomu makanisani na katika mikutano ya kisiasa pamoja na mauaji na utesaji unaoendelea sasa katika Tanzania!!!
 
mmh! Sasa jaman wanataka tufanane na libya au syria watu wanaleta uchochez hafu wanataka kupigania haki zao kwa aman kwel.
 
Back
Top Bottom