Tamko la waziri wa elimu sifa za kujiunga na chuo kikuu


VendoPatrick

VendoPatrick

Member
Joined
Jun 12, 2016
Messages
15
Likes
5
Points
5
Age
35
VendoPatrick

VendoPatrick

Member
Joined Jun 12, 2016
15 5 5
Habarini wapendwa wa Jf, kwanza naomba kuwashukuru wadau wote wa masuala ya elimu kwa michango na mawazo yenu mazuri ambayo mmekuwa mkiitoa pale mtu anapohitaji msaada wa jambo lolote linalohusu elimu. Moja kwa moja naomba niende kwenye mada iliyonisukuma kuwaandikia na kujiuliza kwenu. Mimi ni mwalimu wa secondary ambaye nilianza kufundisha mwaka 2007 baada ya kapata mafunzo ya muda mfupi ya ualimu (induction course) maarufu kama crush programme baada ya kukosa sifa za moja kwa moja (direct entry qualifications) za kujiunga na chuo kikuu,matokeo yangu ya form six ktk combination ya EGM yalikuwa ni E, D &amp; F respectively, nilipangiwa kufundisha masomo ya Geography na biashara/civics baada ya kufundisha kwa Muda wa miaka miwili mwaka 2009 nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya kufaulu mtihani wa pre-mature entry ambao ni mfumo ulioangalia vigezo vya ufaulu kidato cha nne ambapo nilipata division 1 ya point 14. Baada ya kumaliza degree yangu ya elimu katika biashara (BEDCOM) mwaka 2012 nilirudi kituo cha kazi na kuendelea kufundisha, mwaka 2013 nilijiunga na masters of education in curriculum and Instruction ktk chuo kikuu cha kikatoliki cha Ruaha-Iringa(RUCU) na 2015 nilifanikiwa kugraduate na kuwa the best student in the faculty of education of RUCU , jambo hilo lilinitia moyo na nikaamua kuendelea na PhD ambapo mwaka huu(2016)niliapply na kutuma proposal yangu ktk chuo kikuu huria cha Tanzania na kukubaliwa kujiunga na chuo hicho ambapo kwa sasa nipo mwaka wa kwanza wa Phd yangu. Sasa ninachotaka kujiuliza kwenu ndugu zangu wanna Jf ni kwamba hivi karibuni mheshimiwa waziri wa elimu ametangaza kuwafuta kazi wale wote wenye degree waliozipata bila ya kuwa na direct minimum qualifications kama zilivyoainishwa na tcu yaani 4points in two subjects. Na kwamba wale wote waliopitia equivalent qualifications Eg. mature age entry na foundation course kama mimi watabatilisha degree zao. Je hivi ndivyo mh. waziri alivyomaanisha? Na je amebatilisha kuingia chuo kikuu kwa njia ya mature age?na kama ni kweli maana yake mimi nitafutiwa cheti cha first degree na masters na kwamba sina sifa ya kusoma Phd kwa kuwa nilijiunga chuo kikuu kwa mature age ambayo ipo kisheria na inatumika duniani kote <br />Naomba michango yenu tafadhali. Ahsante.
 
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
2,081
Likes
1,885
Points
280
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
2,081 1,885 280
Usijali kuhusu hilo kinachoangaliwa ni wakati ambao ulisoma wewe hicho kitu kilikuwa kinaruhusiwa au vipi kama kilikuwa kinaruhusiwa basi hakuna tatizo kwa mfano mwaka Jana kuingia chuo kikuu kutokea form 6 minimum entry ni E+E lakini mwaka huu ni D+D hiyo haimaanishi kuwa wa mwaka Jana hawana sifa au wataondolewa chuoni hapana wana sifa kwa wakati ule lakini kwa sasa wapya ndio watakaotumia hizo habari mpya wale waliopita heri kwao(kwa njia salama lakini)
 
mtembea kwa miguu

mtembea kwa miguu

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Messages
1,006
Likes
1,310
Points
280
mtembea kwa miguu

mtembea kwa miguu

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2012
1,006 1,310 280
Mkuu ulivyoelewa ndo hivyo hivyo waziri alimaanisha.

Kuna rafk yangu mmoja ni kada wa kindakindaki na ni mmiliki wa chuo frani waziri alivyobadilisha point za kujiunga chuo akafrahia kuwa chuo chake kitashain, kitapata wanafunzi wengi. Sasa kuna tamko jingine la waziri huyu huyu limemkumba amebaki sasa amebaki kutoa puvu.

My take msiwe mbasubiria tatzo likupate direct ndo mjue kumbe mfumo mbovu. Huu mfumo wa mtu mmoja kuamua hatima ya watz wengine kwa jinsi atavyo ni mbaya na unapaswa kipingwa vikali na wanachi wote. Tusisubiri hadi likukute ndo ushitke
 
Abdchota

Abdchota

Member
Joined
Jul 23, 2016
Messages
35
Likes
17
Points
15
Age
30
Abdchota

Abdchota

Member
Joined Jul 23, 2016
35 17 15
Mm nmemuelewa yule wa wizara ya elimu anasema qualification za mwaka husika hazitahusishwa katika hili ila alichokiongelea kuwa wengi wamefeli form 4 alafu wakaenda moja kwa moja foundation courses then chuo au kafika form six kafeli hajapata sifa za wakati husika huyo ndio mwenye matatzo
 

Forum statistics

Threads 1,274,998
Members 490,874
Posts 30,530,038