Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali lililozinduliwa jana: 21.09.2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali lililozinduliwa jana: 21.09.2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Smiles, Sep 22, 2010.

 1. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wadau,

  Jana lilizinduliwa tamko rasmi la wanaharakati wasio wa kiserikali - kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010, pale Blue Pearl Hotel.

  Please see attachments.  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Picha zaidi za uzinduzi.

  [​IMG]


  [​IMG]
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  AGENDA PARTICIPATION 2000
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
  UZINDUZI WA TAMKO LA WANAHARAKATI WASIO WA KISERIKALI 2010; "WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI2010: TANZANIA IPI TUNAYOITAKA?"
  21.09.2010, Hoteli ya Blue Pearl-Ubungo Plaza


  Ndugu wanahabari,

  Asasi ya Agenda Participation 2000 asasi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi ya kuhamasisha utamaduni wa utawala bora na demokrasia ndani ya Tanzania. Asasi pamoja na mambo mengine inatoa elimu ya uraia, mafunzo na kuhifadhi masuala ambayo yanaweza kuimarisha ushiriki wa wananchi katika utawala, demokrasia na michakato ya maendeleo.

  AP2000, ikiongozwa na Dira ya; "Kuona jamii ya kidemokrasia na yenye amani na dola au nchi inayoendeshwa na utamaduni wa misingi au kanuni za kidemokrasia". AP2000 imekuwa ikiratibu tangu mwaka 2005 na pia mwaka huu 2010 mchakato wa kukusanya na kuboresha maoni ya wanaharakati wasio wa kiserikali katika masuala mbali mbali nyeti kwa maslahi ya Taifa letu.

  Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010, AP2000 imehusika kuratibu uandaaji wa Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali kwa msaada wa mashirika mbalimbali kwa taarifa na ushauri. Sambamba na mashirika hayo, kwa namna ya pekee Shirika la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung, wamehusika kufadhili uchapaji, uzinduzi na usambazaji wa tamko hili.

  Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali tunalolizindua leo kupitia mgeni rasmi Mhe. Jaji Mstaafu Lameck Mfalila, 21.09.2010 katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar-es-Salaam likishuhudiwa na wanaharakati toka Asasi za kiraia, Balozi, Mashirika ya Kimataifa, Wanahabari, na wananchi wote kwa ujumla toka kila pembe ya Tanzania limegusa maeneo makuu yafuatayo;

  1. Tathmini ya Maendeleo Kiuchumu na Haki
  2. Ajira
  3. Mazingira na Maliasili
  4. Kilimo, Uvuvi na Ufugaji
  5. Huduma za Jamii
  6. Uongozi na Utawala
  7. Rushwa
  8. Maisha na Usalama wa Binadamu
  9. Maadili ya Uchaguzi
  Vipaumbele hivi vilivyofafanuliwa kwa kina sana katika chapisho la Tamko hili, vinaangaliwa na Wanaharakati Wasio Wakiserikali kama msingi wa kupiga kura wagombea kutoka vyama vya siasa. Sambamba, kuwataka wagombea ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais pia viongozi na watumishi wa umma kuzingatia maazimio hayo wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2010.

  Maazimio haya yanabeba uzito na masuala nyeti yanayoikandamiza Taifa na kuzidi kuliweka katika hali ngumu na kikwazo kuelekea ustawi na maendeleo endapo hayatashughulikiwa kwa haraka na kiukamilifu

  Uchaguzi Mkuu unatoa nafasi adhimu kwa wapiga kura na wagombea kukumbuka malengo ya msingi ya mfumo wa uchaguzi, yaani kuweka mbele na kulinda maslahi ya Taifa hili. Kwa mantiki hiyo, tunasisitiza uwepo wa mchakato wa uchaguzi wenye uwazi, haki na amani.Lakini pia, tunapinga vikali aina yoyote ya vitisho, rushwa, mizengwe au hila kupindisha ushindi utokanao na kura halali za wananchi.Tunasisitiza katika siasa safi zenye kuzingatia misingi ya kidemokrasia.

  Haya ndiyo tunayoyaamini, tunayoyasimamia, tuna amini yana msingi sasa na hata baada ya Uchaguzi Mkuu 2010. Wagombea watakaoingia madarakani, viongozi wa umma wote wanapaswa kuyasimamia kwa vitendo kwa maslahi na ustawi wa Taifa letu.

  Tanzania tunayotaka kuiona ni Taifa lenye amani na maendeleo ambalo linaheshimu haki za wananchi wake wote bila kujali jinsia, hadhi, dini, kabila, imani ya kundi fulani na uwezo kimwili ama kiuchumi. Tunataka Tanzania ambayo licha ya kutokuwa na wala rushwa, inaendeshwa na viongozi wenye uvumilivu na uadilifu, wenye kutumia ipasavyo maliasili na rasilimali hususan watu. Tunataka Tanzania inayojitosheleza kwa chakula; yenye miundombinu bora yenye misingi ya kiteknolojia; na yenye kutafsiri maendeleo ya kitaifa kwa kuangalia afya, elimu na ustawi wa jamii. Tunaomba wananchi wote wayasimamie haya na kuyafatilia, kwa sababu Tanzania tunayotaka inawezekana!

  Ninawashukuru sana kwa kufika kwenu katika uzinduzi huu. Ni matumaini yangu makubwa mtaupasha umma vizuri juu ya haya tuliyowasilisha kwa umma kupitia tamko hili.

  Mungu Ibariki Tanzania!

  Imetolewa na;

  Prof. Max Mmuya,
  Mwenyekiti, Agenda Participation 2000.
  Tel: +255 22 2460036/2460039
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hii kitu inamtoa mkuku kikwete, ikisambazwa nchi nzima kaisha, nafikiri kitafungiwa
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good! Wanafikiri nchi ni yao; sasa kuna wanaoipenda kuliko wao na walio tayari kupigania haki hiyo
   
 6. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya umma haipingiki
   
 7. M

  Mchili JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inawezekana Mungu kasikia kilio cha Watanzania. Kazi kwenye sanduku la kura. Tusijekuwa kama yule mtumwa aliekuwa anaokolewa na ndugu zake akakataa kwa kupenda makombo ya mfalme matokeo yake akaja kuishia kuzikwa akiwa hai mfalme alipofariki. Hata wanaoshabikia CCM kwa maslahi yao binafsi huku wakijua kuwa ni chama kisichoweza kuiondoa nchi hii kwenye matatizo yake wakumbuke hiyo dezo ni ya muda tu na siku moja watazikwa hai na ccm mfu.
   
Loading...