Tamko la wanafunzi wa elimu ya juu kuhusu upigaji kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la wanafunzi wa elimu ya juu kuhusu upigaji kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Saint Ivuga, Oct 22, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,508
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  TAMKO LA TAHLISO KWA UMMA KUTAARIFU JUU YA UPOTOSHWAJI


  WA HABARI ZINAZOHUSU UPIGAJI WA KURA KWA WANAFUNZIWA

  VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA.

  UTANGULIZI:

  TAHLISO ni umoja huru wa wanafunzi, wa Vyuo vya Elimuya ya Juu Tanzania na umoja huu ulianzishwa na kusajiliwa rasmi tarehe 5/5/2004 na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na namba ya usajili wake ni SO No. 14245 ina wanachama wapatao 53 (Vyuo). Hivi karibuni mjumbe wake mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa TAHLISO ametoa taarifa katika vyombo vya habari kuhusiana na suala la upigaji wa kura kwa wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania. Na hivyo basi suala hili kuchukua kasi katika vyombo vya habari kila siku.TAHLISO inasema ndugu Katongo amezungumza kama mtu binafsi bila kuitisha kikao cha Kamati ya Utendaji (EX-COM), na huu ni ukiukwaji wa katiba ya TAHLISO kama chombo chetu. Baada ya EX-COM kukutana kwa dharura kuhusiana na matamko haya ya Mwenyekiti wa TAHLISO, imetafakari kwa kina na kwa kuzingatia katiba ya TAHLSO ikaibaini mapungufu yafuatayo;

  1.Ni kwamba mwenzetu huyu amekurupuka katika kutoa matamko haya, tunasema hivi kwa sababu, kwa mujibu wa katiba yetu ya TAHLISO wa Ibara ya 19 inayozungumzia kazi na wajibu wa Katibu Mkuu wa TAHLISO Ikiwa ni pamoja kutoa matamko,taarifa katika vyombo vya habari, mwenyekiti TAHLISO amevunja kipengele hicho na kufanya kazi ambayo si yake kinyume na katiba, kanuni na taratibu za TAHLISO.

  2.Mwenzetu huyu ameonyesha ubabaishaji mkubwa kwa kutokuwa makini katika tamko lake kwa kuhusisha Tume ya vyuo vikuu (TCU) na hoja ya upigaji kura kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. Tunasema hivi kwa sababu yeye ni mjumbe wa bodi ya TCU kwa mujibu wa katiba yetu ya TAHLISO, na katika kikao cha TCU kilichofanyika mwezi wa nne ambacho yeye alihudhuria tulitegemea kuwa katika suala hili kama halidhiki nalo angeanza kupinga kwenye kikao kwanza na kama ingeshindikana angekuja kutushawishi sisi wajumbe wa EX-COM kuhusiana na hoja hii ili kama ni maandamano ya amani tuyafanye kipindi hicho. Hata hivyo wakati tunapokea taarifa ya mjumbe kutoka bodi ya TCU katika mkutano wetu wa senate ambao ulifanyika pale chuo kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) ndugu Katongo alidiriki kusema hana taarifa yoyote ya kuhusiana na utendaji wa bodi hiyo. Iweje leo aje na kauli hii ya bodi ya TCU kuwa imehusika katika kupanga vyuo vifungue lini ili wanachuo hawa wa elimu ya juu wasipige kura? Kufanya hivi kwanza ni kukiuka msimamo wa bodi hiyo. Hivi ndugu zangu waandishi wa habari mjumbe akitaka kuzungumzia msimamo wa bodi/kikao cha baraza la mawaziri si lazima ajiuzulu ndipo azungumzie msimamo wa baraza hilo? Si mnakumbuka Mh. Mrema alipotaka kupinga msimamo wa baraza la mawaziri alijiuzuru kwanza ndipo akayazungumzia.

  Hivyo basi sababu za wanafunzi kutopiga kura kama alivyobainisha katika tamko lake si za kweli.

  Aidha, tunachokiona sisi kama TAHLISO huenda mwenzetu huyu anatumiwa na watu kutufikisha hapa tulipo. Tunasema hivi, Kwa kuwa tunashangaa kwanini hakutuita sisi wenzake EX-COM atueleze haya na tumpe baraka za kuzungumzia haya kikatiba.

  3. Kauli ya ndugu Katongo kwamba serikali kwa kuamua vyuo vifunguliwe mwezi Novemba inafanya hivyo kwa makusudi kuwanyima wanafunzi wapatao 60,000 haki yao ya kupiga kura ni kauli isiyo sahihi na ni yenye lengo la kuwapotosha wananchi kwa sababu zifuatazo;
  Si kweli kwamba wanavyuo wote wa mwaka 2010/20111 wanapaswa kuwa vyuoni kwa ajili ya kupiga kura.

  Mwaka wa kwanza.

  Hawa walikuwa form 6 na wengine majumbani, muda wa kujindikisha kupiga kura,hivyo si kweli kwamba wataathirika na zoezi hili maana wao wakati huo hawakuwa wanavyuo. Kitendo cha kuwapeleka vyuoni kabla ya tarehe 31 mwezi Oktoba kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha,ni kuwanyima haki yao ya upigaji kura, ambalo tunadhani Ndugu Katongo hakulifanyia utafiti wa kina. Mfano mwaka huu wanafunzi waliodahiliwa kuingia katika vyuo vya elimu ya juu nchini ni zaidi ya wanafunzi 38,000

  Mwaka wa tatu & nne.

  Wengi wao wamekwisha kumaliza masomo yao ambayo kwa kawaida huishia mwezi julai. Hivyo hata kama vyuo vingefunguliwa mwezi septemba /October wao wasingepaswa kuwa vyuoni wala hawatakatazwa kupiga kura wakiamua.
  Mwaka wa pili.

  Hawa wengi wao wapo kwenye mazoezi ya vitendo (field) ni suala lao binafsi kwenda chuo na kupiga kura maana hajazuiwa na yeyote na ni utaratibu wa kawaida kila mwaka wao kwenda field. Wengine wapo kwenye mikoa husika hivyo watapiga kura
  Kutokana na tukio hilo TAHLISO inatoa taarifa rasmi kama ifuatavyo:-

  A.MSIMAMO WA TAHLISO

  Umoja huu upo kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wanafunzi wake wa vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania.

  TAHLISO inatambua na kukubaliana kuwa madai yote ambayo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu waliyokuwa wakiyadai kuhusiana na kupata utaratibu wa kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha vyuoni ni sahihi na ni halali kabisa na ndiyo maana iliyaanisha na kuyawasilisha serikalini September mwaka huu.

  Hata hivyo TAHLISO ni chombo kinachoongozwa kwa kuheshimu maamuzi ya vikao halali katika kuleta umoja na kulinda maslahi ya wanachama wake; kama ilivyoainishwa kwenye katiba kutokana na ukweli TAHLISO haitambui matamko na mipango ya maandamano inayoendelea kufanyika ikiratibiwa na Mwenyekiti Ndg. Katongo, na wala haiamini katika maandamano hayo kwa sasa kutokana na sababu kuu zifuatazo:

  1.TAHLISO inaheshimu maamuzi ya vikao halali ambavyo vitafanyika na wanachama wake na vingine ambavyo vimeshafanyika tayari katika kuleta umoja na kulinda maslahi ya wanachama wake kama ilivyoanzishwa kwenye katiba yake (Objectives of TAHLISO ).

  Maamuzi aliyoyafanya Ndg. Katongo ya kwenda katika vyombo vya habari na kutangaza maandamano na kuipa serikali saa 48 kutoa majibu kwa TAHLISO yalikwenda kinyume na utaratibu, kanuni na katiba ya TAHLISO kwani kwa mujibu wa katiba ya TAHLISO kiongozi mmoja hana haki ya maamuzi makubwa kuhusu hatma ya WanaTAHLISO bila ya kutumia vikao halali vya TAHLISO.

  2.TAHLISO inatamka kwamba maandamano yaliyotangazwa na ndugu Katongo si halali kwa mujibu wa katiba na hatuyaungi mkono kwa kauli moja.
  3.TAHLISO ipo kwa ajili kutekeleza majukumu yake kikatiba na si kutumiwa na mtu, au kikundi au chama chochote cha siasa, kwani kwa kufanya hivyo ni kupingana na katiba yetu ya TAHLISO na lengo zima kuanzishwa kwa chombo hiki.
  HITIMISHO

  TAHLISO inatoa wito kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini Tanzania kutoshiriki maandamano hayo na wapokee fursa yao kikatiba kwenda kupiga kura katika maeneo waliyojiandikisha, bila kushinikizwa na mtu au kikundi chochote kwa manufaa yao binafsi.
  Imeandaliwa na
  ……………………………………

  NG'ORO PROSPER GEORGE

  KATIBU MKUU TAHLISO

  20.10.2010
   
 2. N

  Nanu JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  UUMHH hawa nao watoto!!!! Wakikua wataacha!!!!!
   
 3. H

  H6MohdH6 Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. u

  urasa JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu na barua yake ndiye amekurupuka hata sahihi hapo chini amesahau kuweka kinyume na sheria za uandishi wa barua za aina hiyo,
  anataka tuseme kwa wananchi wamwelewe kuwa naye ni miongoni mwa wale wanachuo wasaka tonge waliochaguliwa na ccm kuzunguka na ridhiwani tz yote?mjinga kabisa na fikra zake mgando
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  i said earlier this is a total waste of time...
  Sidhani hata wanaelewa what are they up to...
  does everybody need to play this game really? kukinzana kwao tayari kunamfanya mtu awafikirie mara mbilimbili.
  Huu msimu na uishe watu wafikirie pa kupatia umaarufu na ulaji.
   
 6. N

  Njaare JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Ndugu zangu wanajamii,

  Huyu muandaaji wa hii taarifa anaonekana ni mtoto tena mwongo anayekaribia kumaliza chuo na huenda ameahidiwa ajira. Utoto na uwongo wake unajidhihirisha katika mambo matatu Kama nilivyoyawekea rangi.

  Moja ni kwenye nyekundu anatumia nafsi ya kwanza umoja (1st person singular). Hii inaonekana kaiandaa yeye na kuiwasilisha. Kama kuna EX com wengine wa Tahiliso wamehusika basi wamesomewa tu.

  Pili huyu dogo ni mwongo (kwenye Blue) sijajua huyu anaongelea field za chuo gani kwani vyuo vingi walishamaliza field na wameshamaliza mitihani yao ya supplimentary na wako nyumbani. Atuambie ni chuo gani. Labda mzumbe ambao huwa wanakuwa na semesta nzima ya field.

  Tatu Huyu hajakua na hajui analolifanya. Kwenye Kijani anaonekana kueleza mambo ya TAHILISO na kujiuzulu kwa Mrema. Hajui hata katiba ya TAHILISO anayoingoza kama katibu mkuu inasemaje mtu anapokiuka utaratibu anapotumwa kuwawakilisha mahali. Pia hawajui hata wajumbe wa TCU.

  Sijui huyu mwenzetu darasani huwa anafanyaje kwa maana hawezi kuandika mambo yanayoeleweka na kwa ufupi.
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ametumwa nini?
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  hehehe... kweli kabisa isipokuwa kwa wanafunzi wa medicine muhimbili ambao corse yao miaka 5 nao nafkiri ni batch kama mbili tu hivi ambao LBDA kama wanaishi mbali na DAR watakosa kupiga kura! na sidhani wasomi wa udactari wnaweza kumchaguwa mtu kama slaa na elimu yake ya kuunganisha unganisha, mbaye hata kabachelor cha elimu dunia hana
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nikiachana na mtiririko mbaya na uwasilishaji hovyo wa hoja, hata aina ya uandishi tu inaonekana huyu ni kihiyo aliyetumwa na mafisadi na ndiyo mbinu za mafisadi zinazotumika maeneo yote duniani. Kwa ujumla, nimepuuza yote uliyoongea kwenye barua yako. Inaonekana hata kujiunga kwako chuoni kulikuwa kwa kuchakachua kwani usingeandika utumbo huo.

  Pipoooooooooooooooooz .................
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,596
  Likes Received: 18,592
  Trophy Points: 280
  .
  Njaare, asante kwa observation yako, nilibahatika kuwepo ukumbi wa karimjee wakati akiwakilisha taarifa hii kwa wanahabari.

  1. Alionekana anaisoma kwa kukosea kosea, anasita sita huku ana hema-hizi ni ishara kuwa taarifa hii hakuiandaa yeye, ameandaliwa na kazi yake ilikuwa ni kuisoma tuu, mtu akisema kitu alichoandika mwenyewe, written speech inakuwa ni talking points tuu,sio asome yote na stammering kibao.
  2. Alipoulizwa maswali na wanahabari, alijibu kwa kujiuma uma sana.
  3. Kwenye taarifa yake kuna kipengele hiki"Aidha, tunachokiona sisi kama TAHLISO huenda mwenzetu huyu anatumiwa na watu kutufikisha hapa tulipo. Tunasema hivi, Kwa kuwa tunashangaa kwanini hakutuita sisi wenzake EX-COM atueleze haya na tumpe baraka za kuzungumzia haya kikatiba". Niliwauliza kwa taarifa yao ile jee wao wamemshirikisha?, au nao wanatumiwa?, swali hili halikujibiwa!. Hivyo jibu unajaza mwenyewe.
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mnalo hilo .....................
   
Loading...