Tamko la Vyama vya Siasa kufuatia hali ya kisiasa nchini. Vyaipinga operesheni UKUTA ya CHADEMA

Hongera vyama makini kwa Tamko makini. Hao wengine sijui hawana kazi za kufanya. Wanapaswa kwenda kwenye majimbo yao waliyoshinda wakahimize maendeleo wao wanasema Nchi nzima hata wasikoshinda! Hii si vurugu jamani? Wananchi wanataka Maji, Elimu, Afya, Barabara na huduma zingine. Hawahitaji kupigiwa kelele na maandamano!! Mbona HAI na MONDULI hamwendi kuandamana?
Tatizo katiba ya nchi ibara ya 3 inahusika hapo na sharia ya vyama vya siasa namba 13..anyway hapa kazi tu siasa mpaka 2020 or 2025
 
Ka Fahmi Dovutwa kamekaa nyumbani kwa kenyewe kakajiandikia barua wenzake walivyogoma kuhudhuria ndo kakaanza kufuta majina ya vyama vingine kwa mkono!!
 
Hopeless. Weka list ya hivyo vyama hapa tuvichambue. Huo mchezo mliufanya miaka ya 90. Amua kutumia mtutu au achia kidemokrasia.
 
Sasa kama wanaunga mkono mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku unategemea nini?

Sasa si ndiyo siasa ilivyo???? Hata CHADEMA si waliwahi kuungana na CUF, NCCR Mageuzi na vyama vingine viwili kuunda UKAWA??? Hiyo ndiyo coalition...mchezo wa siasa hauhitaji hasira...
 
wao pia wana haki ya kuamua mambo yao,hapa tusubiri yale mabehewa yatatoka na tamko gani, hawaeleweki kuunga mkono ukuta au kuupinga wapo kimya!
 
Kuna mdau alishatabiri kutolewa kwa tamko kama hili na akina Dovutwa & Co. Hata hivyo wamechelewa sana kulitoa.
 
Kwani mikutano na maandamano ni haramu? Mbona katiba inaruhusu? Inakuwaje leo Dovutwa anaogopa mikutano na kusema kuwa inavuruga Amani?
 
mbona wameshauri vizuritu

Hapana Mkuu, tamko lao linakuwa kama vile limeandikwa na messenger pale Lumumba.

Wangetaka kuweka uzito, kwanza wangechukua position ya mshauri ambaye yuko neutral, au unatoa ushauri pande zote mbili ili kuleta muafaka. Lakini sasa wameandika kwa namna ya kujipendekeza kwa Raisi Magufuli, bila kutoa solution. Sasa sijui wanajipendekeza kwa kitu gani, maana vyama vyenyewe nadhani hata Magufuli ndio anavisikia kwa mara ya kwanza ndani ya tamko hili.

Na zaidi, hivyo vyama vingine vilivyokatwa kwa peni inamaanisha nini hasa? Kama havikutaka kuwamo kwa nini vikatwe kwa peni badala ya kutotajwa kabisa?

Pia, hivi umewahi kusikia juu ya uwepo wa "Politcal Leaders Club"? Au imeundwa haraka haraka ili kutoa tamko hili?

Na kama wao ni genuine "Politcal Leaders Club" kwa nini wasiorodheshe list ya vyama vyote vilivyo wanachama angalau kwenye footnote? Na katika list hiyo, kina Chadema, NCCR, CUF, ACT wamo? Maana kama hawamo tayari inamaanisha tangu huko nyuma hawa so called "Politcal Leaders Club" hawakukubaliana kimawazo na Chadema na wengine, hivyo hakukuwa na haja ya "Politcal Leaders Club" kutoa tamko la kuunga au kutounga mkono Chadema.

Lakini zaidi ya yote, Chadema hawajasema wanafanya maandamano kwa niaba ya vyama vyote vya upinzani. Sasa tamko toka vyama vingine vya upinzani ni la nini?

Conclusion yangu ni kwamba, kama kweli hii "Politcal Leaders Club" ipo na hivyo vyama vya upinzani vipo, basi ni vyama uchwara tu!
 
Vyama vya siasa nchi leo vyakutana na kufanya tafakuri ya kina juu ya hali ya kisiasa nchini pamoja na tamko la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

View attachment 379605
Mbona hawa pingi kukiukwa kwa demokrasia na kuingiliwa kwa katiba? Mimi naona hivyo vyama ni vile vinavyo tengea uongozi wajipatie maslahi yao binafsi...
 
Back
Top Bottom