Nina mdogo wangu hapo chuoni na amesema mbona hawajashirikishwa kuandaa msimamo wa chuo? Hivi huu ni msimamo wa nani?...........lakini la msingi kama hawa kweli ni wasomi hapo chuoni wamekwenda kufanya nini?.............................nijuavyo wasomi wapo makazini wanatatua matatizo ya jamii ...............aliyeko chuoni anautafuta usomi kwa hiyo hana ubavu wa kujiita msomi................hususani pale hata wale anaodai kuwawakilisha hata hataki kuwashirikisha kwenye maamuzi nyeti kama haya..................
Leo ndiyo nimeamini kuwa humu JF kuna vilaza na mbumbumbu wakubwa. Hiyo taarifa ya vijana inajieleza na iko wazi kabisa. Oneni aibu na muwashauri wabunge wa Chadema. Soon or later they will go out of sight mirror completely
Hongera kwa kuwafumbua macho vilaza wanojiita wasomi humu JF kwa kutokujadili na kutoa shutuma bila tafakuri za kina juu ya tamko hilo.
MSOMI ni mtu mwenye kuvutiwa na fikra na mwenye mbinu za kizisarifu na kuzitumia vilivyo(fikra hizo) baadhi au zote. Profesa Ali Mazurui.
Typical SISIEMU..........! Masikini watoto hawa, hata hawajuia abcs za haya wanayoyasema........!.....kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo.............
Leo ndiyo nimeamini kuwa humu JF kuna vilaza na mbumbumbu wakubwa. Hiyo taarifa ya vijana inajieleza na iko wazi kabisa. Oneni aibu na muwashauri wabunge wa Chadema. Soon or later they will go out of sight mirror completely
Hongera kwa kuwafumbua macho vilaza wanojiita wasomi humu JF kwa kutokujadili na kutoa shutuma bila tafakuri za kina juu ya tamko hilo.
MSOMI ni mtu mwenye kuvutiwa na fikra na mwenye mbinu za kizisarifu na kuzitumia vilivyo(fikra hizo) baadhi au zote. Profesa Ali Mazurui.
wapuuzi wakubwa ninyi!!
mnazan jf ni kijiweni? mtaburuzwa hadi dk ya mwisho.....chambeni mkalale wehu wakubwa ninyi
Hao ni wasomi CCM na wanawakilisha CCM, ngoja tusubiri tamko la wasomi Chadema
Waraka huu umesomwa muda si mrefu mbele ya vyombo vya habari zaidi ya 15 huko Dodoma.
TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.
Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.
Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.
Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.
Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.
Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya Bunge moja je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?
Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.
Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.
Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .
Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.
Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.
Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.
Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.
Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.
Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.
Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.
Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.
Aksanteni sana.
IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA
Msiwalaumu sana. Their problem is that they are NOT getting education, they are just getting information about education
nyinyi wana chadema jf branch mbona mnakosa ustaarabu wasomi si wametoa mtazamo wao!!!!
wapeni uhuru wa kuongea kama kuna wana chadema udom branch na wao si waseme ya kwao!
mnapenda kulazimisha kila kitu!!!
msomi akiwa chadema akiwa ccm si msomi...........! msomi aisifuye chadema aikosoaye si msomi.....! kama mchangia mada mmoja alivyosema... twasubiri wasomi wa chama cha migomo nao watoe tamko...!
Hao ni wasomi wa wapi kikundi fulani cha mafisadi, tutatoana roho wasiwatanie watanzania.
Msomi gani unaunga mkono sheria inavunjwa, Usomi si kuunga mkono ufisadi.
Hao ni wale watoto wa mafisadi kama kweli wanauchungu na nchi hii, embu waorodheshe majina yao tuwafahamu, maana isijekuwa wale Mkada wanaonunuliwa na CCM kwa 5000 na kupewa kadi halafu unasema usomi.
Mbona hawakutoa tamko wakati ule NEC imewazuia kupiga kura, hao ni kikundi cha wezi tu, wale ambao wanajiita UVCCM.
Hata mtoe tamko maana aliitoa Shimbo bado watu wakawa na msimamo ndio hiyo inayotoleawa na wapumbavu.
WaTZ na Wana Chadema tusonge mbele najua CCM na mafisadi wanakereka na mambo mnayofanya lakini sisi wananchi tunaiamini sana Chadema na viongozi wake.
PEOPLES POWER
(Kwani hawa watoto wao wametumwa na wapiga kura wa wabunge wa Chadema? Wametoka katika majimbo waliyotoka hawa wabunge hadi wazungumzie matarajio ya wapiga kura wao?)Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla (ghafla ) kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.
Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.
Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
(Kama hawa watoto wanafahamu/wanajiita wasomi walipaswa kuchambua hoja with data; wangefanya utafiti kuipitia katiba na kanuni za kudumu za bunge maana hizo ndiyo zinatoa muongozo!! Hoja bila vielelezo inaonyesha mapungufu makubwa ya hawa "wasomi")Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.
Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni 9Je ni kifungu kipi cha katiba au kanuni za kudumu za bunge kinazongumzia hili?
(kwa nini hawajauwasilisha kwa wanahabari?)Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao
(Hii kauli mbiuu si ya Chadema, ni ya CCM, hawa ni wabunge wa Chadema, mnapaswa kulitambua hilo)wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja' je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?
(Wasomi feki kumbukeni kwamba hoja ya Chadema ni kwamba kura zilizompa ushindi rais wenu ZILICHAKACHULIWA!! Hiyo ndiyo sababu kuu ya kutomkubali, ukweli ni kwamba hakuchaguliwa kwa kura nyingi kama mnavyodai/mlivyotumwa kueleza)Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune (wabunge?) hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.
(Bunge halina kazi moja tu ya kupitisha sheria, wabunge wa Chadema bado wana kazi nyingi bungeni na nje ya bunge! Mbunge si mtu wa kuhudhuria vikao Dodoma tu na kupitisha sheria kama mnavyodhani)Nne Kwa badhi (baadhi?) ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.
Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .
( Kususia hotuba ya Rais kuna uhusiano gain na machafuko? Je, wizi wa kura na KUCHAKACHUA MATOKEO mmeona hakuhusiani na machafuko? Mbonamlikaa kimya wakati CCM inachakachua matokeo? Au pale ilipotumia vyombo vya dola kuiba kura? Ina maana maoni ya wengi na malalamiko ya wananchi hamkuyasikia? Mbona hamkotoa tamko hapo?)Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.
(Hapa mmepotoka; ina maana mnaanza kuwashawishi wapiga kura wawakatae Chadema? Who are you to do this? Waacheni wananchi wenyewe waliowachagua wabunge hawa kwa kura nyingi watoe maoni yao; unajuajje kama ndiyo walikuwa wanatekeleza mojawapo ya maelekezo ya wapiga kura wao?)Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.
(Nyie ndiyo mmekosa nidhamu! Mtu anaweza kuendelea kuwa baba lakini endapo hatiumizi wajibu wake; au hatendei haki wanawe wote basi mtoto ana hali ya kumwambia baba ‘sikuridhika na hili"!! Hiki ndicho kinafanywa na Chadema)Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.
Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.
(Huo ndiyo mkakati wa CCM; kuleta agenda za nchi jirani kama kielelezo cha amani!! Angalia nini kimetokea Kenya, sasa wana Katiba mpya; agenda hizo zilikuwa zinaletwa na wapinzani, sasa kila kitu kiko OK!! Leo hii bado nyie manoojiita wasomi mnaona agenda za Chadema amabazo ndiyo zitatupeleka kwenye agenda ya Katiba mpya kuwa ni mwanzo wa machafuko!! What a shame? Mnanishangaza hadi leo hamjaweza kuelewa maana halisi ya mapinduzi ya kweli)Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani
(Acheni upuuzi, mbona mmedanganyika kwa CCM hadi kuitisha press conference?)Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache
(NYIE NDIYO MUWAOMBE WAO RADHI PAMOJA NA KUTUCHEFUA WANANCHI)Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.
(WTF?? Na kazi yenu nyie ni nini? Mmekuwa tawi la WACHAKACHUAJI?)Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.
(Vipi kuhusu ubaguzi unaofanywa na CCM miaka mingi tokea uhuru?)Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA
(who the hell are you?):angry:Aksanteni sana.
IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.
KNOWLEDGE *IS NOT* POWER..........IT IS REALLY:
Knowledge becomes power only when it is put into action for the attainment of a definite objective.