Tamko la Vijana 'WASOMI' wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma Dhidi ya wabunge wa CHADEMA

watoto wajinga hawa jamani mpaka wanaudhi. hivi chips nyama choma na bia ndo zinaendesha taifa?
nani asiejua makapi mengi ndo yanamwagwa huko udom??? basi hamna jipya linalotegemewa toka pande hizo atleast not from me.
 
Kuwalaumu kwa kuwakejeri wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma ni kutowatendea haki. Wao wametoa hoja zao kwa ufasaha na kwa lugha ya kistaarabu. Hamna dhalau yoyote katika hoja zao. Ningetegemea kuona hoja zao zinapingwa kwa hoja badala ya kusema kwa ujumla kwamba hoja zao ni nonsense au kuhoji kiwango chao cha elimu. Wewe ukisema hoja zao ni nonsense na wao wanao uwezo wa kusema hivyo na mhariri akaandika. Hiyo haitakuwa na manufaa yoyote katika forum ya kisomi kama hii.

Baada ya kusema hayo mimi binafsi kwa upeo wangu wa ufahamu na uelewa naunga mkono hoja za vijana hawa wasomi. Nionavyo mimi, wanacho jaribu kufanya wabunge wachache wa Chadema ni kubadilisha uamuzi na chaguo la wengi kwa utashi wa watu watu wachache. Kwa mantiki ya kawaida, chama kilichoshindwa kupata hata asilimia ishirini ya kura zote za ubunge nchini hakiwezi kutarajia matokeo tofauti sana katika ngazi ya uraisi. Wangekuwa wanayakataa pia na matokeo ya ubunge na udiwani tungewaona wanahoja. Kama udiwani hawakuweza kupata hata asilimia kumi ya kura zote ni miujiza gani wangetumia kupata uraisi wa nchi?

Wanamkataa Raisi, sawa. Raisi kamteua Waziri Mkuu kwa madaraka yake yale yale ya uraisi wanaoukataa, mbona hawakutoka nje Waziri Mkuu alivyoingia bungeni? Je Baraza la Mawaziri litakaloteuliwa na mheshimiwa Raisi nalo watalipinga? Ina maana hawatahudhuria vikao vya bajiti vya wizara mbalimbali? Hiyo serikali kivuli bungeni itakuwa na maana gani? Wabunge wa Chadema hawatakuwemo katika kamati mbalimbali za Bunge zinazosaidia wizara na idara mbalimbali za serikali?

Waheshimiwa wanalalamikia Katiba na sheria za uchaguzi. Malalamiko yao hayawezi kuwa hayana msingi katika kona zote nne. Nakubali kuwa yapo mapungufu katika sheria za uchaguzi ambayo yanahitaji kutizamwa zaidi. Yalikuwepo mengine mengi lakin baadhi yake yameshatatuliwa. Hata hivyo, Chedema wakati wanaingia katika uchaguzi mkuu walikuwa wanayajua matatizo hayo. Mengine yalishajulikana wakati mfumo wa vyama vingi vinaanza. Kwa wabunge makini tulitarajia kwamba wangejipanga kutumia nafasi zao chache bungeni kuyatafutia matatizo hayo suluhu. Kwa kuanza na kumkataa Raisi ambaye chama chake kina zaidi ya asilimia sabini ya wabunge wowote ni dhahiri kwamba Chadema hakijaanza vizuri. Ni vigumu kuwashawishi wabunge wengi wa CCM kuunga mkono hoja zenu kama mnaanza ubunge kwa uhasama usiokuwa na dira. Uhasama mnaouonesha unajenga uimara na umoja kwa wabunge wa CHAMA cha Mapinduzi jambo ambalo ni hatari kwa uimara wa Chadema. Nani asiyeju namna mgawanyiko ndani ya Chama cha Mapinduzi Bungeni na kwingineko kulivyosaidia kuimarika kwa Chadema? Nikisema hivyo nitaitwa majina mengi kama "mwenye chuki na mageuzi", fisadi wa kisiasa na kadhalika. Lakini kwa mtu mtulivu wa fikira maneno kama haya hayawezi kutolewa na "mtu anayepinga mabadiliko".

Kwa maoni yangu kumsisa Raisui hakutakuwa na faida yoyote ndani ya Chadema mbali ya manufaa kwa wana CCM. Watanzani tujifunze kukubali kushindwa na kuheshimu maamuzi ya wengi. CHADEMA mlikuwa na msemo mzuri wa kifalsafa katika kampeni zenu:" People Power". Kwamba ukiwa na watu una nguvu. Kama ingekuwa kweli watu walimtaka SLAA na Tume ya Uchaguzi Iikachakachua kama CHADEMA wanavyodai, dalili ingeonekana. Kwa sasa malalamiko mengi yanatoka kwa viongozi wa CHADEMA sio wananchi. Hata wanachama wengi wa Chadema hawajaonesha malalamiko ya msingi wakati matokeo ya uchaguzi wa Raisi yanatangazwa. Sehemu chache zilizokuwa na matatizo katika matokeo ya Ubunge ambako wanachi waliwachagua Chadema, malalamiko ya kwanza yalitoka kwa wananchi na wala sio viongozi wa Chadema. Bahati nzuri uchaguzi wa mwaka huu ulishuhudiwa na mamia ya waangalizi wa kimataifa na wandani. Hatukuona ripoti yoyote inayozungumzia kuibiwa kwa kura za Uraisi.[/QUOTE

unasupport kitu usichokijua my friend. Tumia akili kidogo utakuja gundua hilo. Afterall sidhami kama hili ni tamko la wanafunzi wa vyuo Dom kulingana na timing yake.
 
Waraka huu umesomwa muda si mrefu mbele ya vyombo vya habari zaidi ya 15 huko Dodoma.

TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.


NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.

Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.

Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.

Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.

Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?

Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.

Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.

Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .

Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.

Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.

Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.

Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.

Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.

Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.

Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.

Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.

Aksanteni sana.

IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA

Ni Tamko la 'pupils' wa shule za msingi waliopo Dodoma katika shughuli za halaiki na chipukizi kwa maadalizi ya sherehe za mapinduzi ya Unguja na PembaJanuari, 1971
 
Binafsi nasikitishwa sana na tabia ya baadhi ya wachangiaji kutokuwa wavumilivu na wastaarabu na kuamua kutoa hoja za matusi na kejeri badala ya kujibu hoja. Msingi wa majadiliano, nijuavyo mimi, ni uvumilivu na kuheshimu hoja na mawazo ya wengine hata kama utayaona ni dhaifu kiasi gani. Kwa hali kama hii kuendelea licha ya wachangiaji kutoa tahadhari mimi nataka kuanza kutupia lawama kwa mhariri wa Forum au utaratibu unaoongoza forum yetu. Siyo haki hata kidogo kwa mchangiaji kuchangia anachokiona kuwa sahihi akaishia kutukanwa au kukejeriwa kwamba haja soma, kijana mjinga, amenunuliwa kwa fedha za chips na kadhalika. Sijui kama wachangiaji wenzangu hatujui kama wanafunzi wa vyuo vya juu ni watu wazima kama sisi na wengine zaidi yetu? Kwa nini ujione bora na mjuzi sana kiasi cha kuwadharau na kuwatukana wachangiaji wenzako eti kwa sababu wana mawazo na msimamo tofauti na wewe? Pia nashindwa kuelewa ni kwa nini mhariri akaruhusu michango haramu kama hiyo?
 
Back
Top Bottom