Tamko la Vijana 'WASOMI' wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma Dhidi ya wabunge wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Vijana 'WASOMI' wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma Dhidi ya wabunge wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzanzibara, Nov 19, 2010.

 1. Mzanzibara

  Mzanzibara Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waraka huu umesomwa muda si mrefu mbele ya vyombo vya habari zaidi ya 15 huko Dodoma.

  TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
  NDUGU WANANCHI,.


  Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

  Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.


  Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.


  Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.


  Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.


  Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?


  Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.


  Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.


  Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .


  Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.


  Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.


  Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.


  Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.


  Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.


  Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.


  Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.


  Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.


  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.


  Aksanteni sana.


  IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD

  KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA
   
 2. K

  Kisu changariba Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watoto wanaponzwa na vibeer na chips kuku zitolewazo Dom Hotel. Cant you guys use yoyr heads?? Shule inawasidia nini kama hata tamko mnaandikiwa na vigogo??
   
 3. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nonsense!!!!!!
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Elimu haijawakomboa, My poor Tanzania kama hawa vijana ndo taifa la kesho wanakuwa na akili finyu kiasi hiki, kweli maisha magumu na umasikini ni urithi wetu!
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawa wasinasibu kuwa ni vijana wasomi bali ni vijana wanaokariri
  hiyo taarifa yao imejaa, mapungufu kibao sasa kama usomi umeishia kwenye mtazamo huo ni
  dhahili kuwa serkali imeingia hasara kubwa sana kuwa na taifa la wasomi wa aina hiyo
  siku za mbeleni
   
 6. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sasa nimeelewa kwanini rafiki yangu alinisihi sana nisimpeleke mwanangu chuo kikuu dodoma.

  He was RIGHT!
   
 7. s

  seniorita JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  pure nonsense; they didnt walk out of their resposibility, but out of their responsibility to the people they represent. Hivi hawa vijana wanawakilisha wenzao wote, au ni kundi tu lililonunuliwa na CCM mafia; for heavens' sake; vijana ndio wanaokuwa more affected by this unfair system, no employment, when they are employed they ar egiven meagre salaries, and when they complain, "I do not need your votes" etc. Mama zenu na baba zenu wanahangaika na ukata vijijini, halafu you bring this nonsense!!!! Someni mpate busara, na si kusoma kuendeleza ujinga, otherwise they is no need mtumie country's resources to harbor foilly; that you can get it even without going to school
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mamluki waliotumwa na baba zao wafisadi!kila tunapopiga hatua katika kutafuta haki na kuweka ustawi mzuri wa jamii wa siku zijazo,lazima watokee watu wa kuturudisha nyuma!Hakuna haja ya kurudi nyuma ,lazima tusonge mbele tuu,ujinga kwetu ni mwiko!!
   
 9. Mzanzibara

  Mzanzibara Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaliyosemwa yana mantiki au hayana???
   
 10. D

  Dina JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hawa nao, tukisitisha hiyo ada sijui watafanyaje!
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wababishaji tu hao na wezi wachanga wamali za umma, mbona kulingana na
  mwenendo mbaya wa kuhesabu na kutangaza matokeo ya kura
  hawakutoa masikitiko yao, wasomi gani hao wasiokuwa na upeo wa mambo
  mafidhuli wakubwa hawa, hawako fair kabisa
   
 12. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hao ni wasomi CCM na wanawakilisha CCM, ngoja tusubiri tamko la wasomi Chadema
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Is not the right person. Vyuo vyote TAnzania serikali zao ni CHADEMA. hUYU KIRAKA TU.
   
 14. Double X

  Double X Senior Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PAMBAFFFF, mi nilifikiri kuna la maana kumbe ni upupu mtupu!!!wote hamnazo hapo udom!
   
 15. O

  Oracles Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi?au wametumwa?njaa nyingine bana...hawana ada afu wanamsaidia mkwere...mmeishiwa ninyi..usomi wenu wa mashaka.
   
 16. Mzanzibara

  Mzanzibara Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lmao!!Watu wameanza kushtukia Chadema wahuni,wameamka!!
   
 17. Mzanzibara

  Mzanzibara Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yetu macho,mi ntapost tu!
   
 18. M

  Milindi JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,210
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nyie mnaojifanya wasomi wakati ni wavivu wa kufikiri acheni hizo,ni wapuuzi na ccm itawafanya kama kondomu.Baada ya kuwatumia na mikopo mtaendelee kupata kwa shida.Mlitaka wananchi waandamane ndipo mjue kuwa uchakachuaji ulifanyika.Ninawapongeza wabunge wa Chadema kwa kufanya hivyo na tunasubiri mchanganuo jinsi hawa walivyoiba mpaka dunia nzima ielewe huyu jamaa si rais halali ila katiba mbovu ndio inamuweka madarakani.Hongera sana Chadema na tunasubiri taarifa rasmi kuhusu jinsi mafisadi hawa walivyoiba kura.
   
 19. m

  matawi JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama kweli ni maoni ya wanafunzi Dodoma basi liko tatizo kubwa la wasomi/vijana wetu. Chadema iko vitani kuwapigania watanzania wote kwa dhuluma zinazofanywa na serikali iliyopo madarakani na hiyo move ni ujumbe kwa watanzania na dunia nzima kuhusu udidimizwaji wa demokrasia nchini. Kingine cha kuelewa hapa chadema hawakusema hawatahudhuria mikutano ya bunge wataendelea kama kawaida wao wana tatizo la kikiwete kufoji kura za kumuingiza ikulu huku akifahamu kuwa Rais akiapishwa hakuna chombo au mahakama yoyote inayoweza kutengua . Vijana fuatilieni mambo kiundani. Labda tusubiri TAHLISO kama wana maoni tofauti
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama kweli ni wanavyuo you are in the wrong place. Think with your head not with your stomach. Mnajidhalilisha kujishirikisha kwenye issue msiyo na uzoefu nayo. Nawatahadharisha you will be dumped by the same person using you now. Tanzania na Africa haihitaji vilaza
   
Loading...