Uchaguzi 2020 Tamko la Ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi Mkuu Tanzania 2020

Ukiona watu wanawababaikia hao mabeberu ujue kuna asilimia fulani ni vibaraka wao.Beberu hawezi kukutetea bure, kama hatamani kitu kutoka kwako. Ndio maana magu anawatenda kwa akili kubwa.

Kinachompeleka mzungu sehemu ni maslahi yao tu. If they have nothing to gain, they won’t intervene hata mkichinjana kama walivyofanya Rwanda!
 
Nyinyi Marekani amueni moja tumechoka matamko ya kila siku

Halafu hawa wazungu walipaswa kuwa wanafanya effort ya kupata uelewa sahihi wa local environment.

There’s no such thing as peaceful protest kwenye hizi nchi masikini. Ndani ya hizo protests kuna watu ambao wanazitumia kama kichaka cha kuwawezesha kufanya uporaji bila kuwajibishwa. Looting is the ultimate goal of their involvement. They usually create chaos in order to rob people! So, at the end of the day, a lot of innocent people end up sustaining bodily and economic injuries!
 
Ambao wamekuwa wakitamka kuwa wazungu ni mabeberu, ukiangalia hata posts zao humu, utaona ni watu wenye upeo mdogo, akili ndogo na uelewa mdogo - ni low IQ minds.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mtazamo wa msomaji





China yataka uchaguzi wa Tanzania kutoingiliwa

habarileo.co.tz10/22/2020



SERIKALI ya China imesisitiza msimamo wa nchi hiyo na kuyataka mataifa mengine kutoingilia masuala ya ndani ya nchi mbalimbali duniani, ikisema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kusimamia uchaguzi wake mwenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhao Lijian wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari mjini Beijing nchini humo.

“Tunaamini kuwa Serikali ya Tanzania na watu wake wana busara na uwezo wa kuendesha uchaguzi. Tunawaombea uchaguzi uwe salama na wenye mafanikio. Kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine inapaswa kuwa kanuni ya kufuatwa na nchi nyingine duniani. China inazitaka nchi zote kuheshimu kanuni hii na pande zote zinapaswa kuunga mkono uhuru wa nchi za Afrika na kulinda uhuru na uimara wao,” alisema Zhao.

Msemaji huyo wa Serikali ya China aliulizwa kuhusu maoni yake baada ya kuripotiwa kuwa Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu wake Oktoba 28, mwaka huu, na kwamba Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania hivi karibuni ulitoa taarifa juu ya uchaguzi huo ikiitaka Serikali ya Tanzania idumishe mchakato wa demokrasia, ikibainisha kuwa haitasita kuchukua hatua kwa watakaobainika kusababisha vurugu au kuvuruga mchakato huo wa demokrasia.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Balozi wa China nchini, Wang Ke kutoa wito kwa mataifa mengine duniani kuheshimiana na kuacha kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio chochote kile na kueleza kuridhishwa kwake na namna mchakato wa Uchaguzi Mkuu unavyoendelea nchini.

Balozi Wang aliyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge. Alisema kuwa ni lazima mataifa yote yaendeleze uhusiano mwema miongoni mwao na kutoingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine.

Aidha, alisema kuwa China itaendelea kuheshimu masuala ya ndani ya mataifa yote, Tanzania ikiwamo. Alieleza kuridhika kwake na mchakato wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinavyoendelea nchini na kuwatakia Watanzania kila la heri katika uchaguzi huo.

Katibu Mkuu Balozi Brigedia Ibuge alisema ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China kisiasa, kiuchumi na kijamii ni madhubuti na imara. Alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea pia kuheshimu ushirikiano na mataifa mengine.

Aliishukuru China kwa ushirikiano wake wa kimkakati kwa Tanzania. Alisema uhusiano huo utaendelea kudumishwa kwa maslahi ya pande zote mbili.
 
Daaah kwa akili hizi n afadhali tuu mmekosa kila kitu, kwahy ulkuwa mnataka kushinda ili mpate misaada.?
-Wapi nimesema tunataka tushinde ili tupate misaada?
-Heshimuni democracy ili mpate misaada nchi hii ni masikini/ tegemezi
 
Hey hey leave TZ alone.
Kila nchi ijisort,ndio sababu tuna mahakama,anaejiskia kuibiwa ataenda mahakamani.
Hata wao wanajua vizuri Lissu hawezi kumshinda Magufuli,na wabunge wengi CCM kushinda ni kutokana na utendaji mzuri wa Magufuli.
Wao wakivote nchi gani huwaingilia.
 
Yani heri Sadam Hussein walimkamata kajificha kwenye shimo la panya ndevu kasahau nje. Huyu wa kwetu watamkuta kajianika juu ya mawe kama kenge!
Yaani kirahisi tu kwani halindwi?.Hata hivyo wakati anafanya hizi sarakasi naamini alikuwa anajua kwamba kuna USA n.k.Lakini jiulize licha ya hivyo kwa nini sarakasi zimefanyika tena kwa kujiamini kabisa!
 
Hao nao hawana msaada wowote kila siku maneno hayo hayo tu hapa naanza kukubali duniani hakuna mungu au kama yupo hashiguliki na maisha ya duniani jamani Chadema wenzangu tutafute njia nyingine na sisi hii ya masanduku imeshagoma
Kuna kundi au genge la watu wameishajimilikisha hii nchi. Sasa mwaka huu wameamua kukunjua makucha yao wazi wazi kabisa.
 
wananiboa mods hawa
nyuzi zangu kibao halafu za kawaida sana yaani hazipiti
Mimi nilipigwa ban wiki moja baada ya kutokubaliana na hoja ya mgombea urais CCM! Post zangu zakawaida zinazozimwa ni nyingi sana yaani wakiona jina tu, zinaishia Lumumba!
 
Kuna kundi au genge la watu wameishajimilikisha hii nchi. Sasa mwaka huu wameamua kukunjua makucha yao wazi wazi kabisa.
Ila kusema kweli inaumiza mtu akishinda kwa halali huwezi kuumia kwakuwa amekushinda lkn sio kwa utapeli huu waliofanya
Viongozi wa dini wote kimya maaskofu masheikh mapadri sasa najiuliza huko kanisani na misikitini wanamuomba nani
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom