Uchaguzi 2020 Tamko la Tume ya Haki za binadamu kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Watanzania wote waliotimiza vigezo kwa mujibu wa sheria, wanatarajia kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Hatua hii muhimu imefikiwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa miezi kadhaa uliohusisha hatua za uhuishaji wa madaftari ya kudumu ya wapiga kura, uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali na kampeni.

Tume, inapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Mosi, kwa kulipa uzito tukio hilo na kutoa fedha za kuligharamia ili wananchi waweze kutimiziwa haki yao ya kikatiba.

Pili, Tume inazipongeza Serikali zetu, kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa maandalizi mazuri na kwa mwendelezo wa utoaji elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu uchaguzi mkuu na kwa kusimamia vyema hatua zote za mchakato wa uchaguzi kwa weledi huku zikizingatia sheria na kanuni za nchi, haki, usawa, usalama na amani.

Pia Tume inalipongeza Jeshi la Polisi kwa kulinda usalama wa raia na mali zao katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi. Vilevile, Tume inavipongeza vyombo vya habari kwa kuzingatia haki ya kikatiba ya wananchi kwa kuwahabarisha kuhusu matukio na sera zilizokuwa zinanadiwa na wagombea na vyama vyao na elimu iliyokuwa ikitolewa na wadau mbalimbali katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi. Jambo hilo limetoa fursa kwa wananchi kuwasikiliza na kuwapima wagombea wa vyama mbalimbali na litawasaidia kuchagua viongozi sahihi siku ya upigaji kura.

Tume inawaasa wananchi wote raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuzingatia sheria na kanuni za nchi kwa kuhifadhi amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

Katika kipindi hiki cha siku zilizobakia kuhitimisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2020, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kutoa wito ufuatao kwa wadau mbalimbali:

1. Wananchi
Wajitokeze kwa wingi na kutumia vyema haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi watakaodumisha amani, umoja na mshikamano nchini na kuliletea maendeleo Taifa letu.

2. Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama
i) Wasimamie amani ili watanzania waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura katika hali ya utulivu na amani na kuchagua viongozi bora.

ii) Wanapotekeleza majukumu yao wazingatie maadili, waheshimu haki za binadamu na na mising i ya utawala bora na waepuke matumizi makubwa ya nguvu yasiyokuwa ya lazima.

3. Mamlaka zenye dhamana ya kusimamia uchaguzi
i) Zihakikishe uchaguzi mkuu unasimamiwa kwa haki na amani wakati wote.

ii) Wadumishe amani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa wazi, wenye amani na utulivu.

4. Viongozi wa dini
Waendelee kukemea maovu na kuliombea taifa katika kipindi hiki muhimu ili haki, amani, utulivu na upendo viendelee kudumishwa sasa na hata baada ya uchaguzi kumalizika.

5. Wagombea watakaoshindwa
Kwa kuwa katika kila ushindani ni lazima awepo mshindi na atakaeshindwa, wagombea watakaoshindwa wanaombwa wakubali matokeo ili kudumisha amani ya nchi yetu. Ambaye hataridhishwa na matokeo, ni vema akafuata mkondo wa sheria na kanuni zilizowekwa zinazoruhusu kudai haki badala ya kutafuta njia za mkato katika kudai haki ambazo matokeo yake yanaweza kuwa hasi.

Tume inawatakia Watanzania wote Uchaguzi mwema

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Imetolewa na:
Jaji (Mst) Mathew P. M. Mwaimu
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Oktoba 26, 2020
 
Mbona hawajawaasa wapigakura kurudi nyumbani kusubiria matokeo badala ya kubaki vituoni na kulinda kura,au hawajaona uzito wa jambo hilo
 
Nimeona neno HAKI kwenye andiko lao (niwape hongera), cha ajabu wengine wote pamoja na Magu kamusi zao hazina neno haki ni Amani tu.
 
Asanteni tume

Kesho Watanzania tunajambo letu, tunaenda kumfundisha msaliti wa Nchi kwenye boksi la kura
 
Watanzania wote waliotimiza vigezo kwa mujibu wa sheria, wanatarajia kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Hatua hii muhimu imefikiwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa miezi kadhaa uliohusisha hatua za uhuishaji wa madaftari ya kudumu ya wapiga kura, uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali na kampeni.

Tume, inapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Mosi, kwa kulipa uzito tukio hilo na kutoa fedha za kuligharamia ili wananchi waweze kutimiziwa haki yao ya kikatiba.

Pili, Tume inazipongeza Serikali zetu, kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa maandalizi mazuri na kwa mwendelezo wa utoaji elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu uchaguzi mkuu na kwa kusimamia vyema hatua zote za mchakato wa uchaguzi kwa weledi huku zikizingatia sheria na kanuni za nchi, haki, usawa, usalama na amani.

Pia Tume inalipongeza Jeshi la Polisi kwa kulinda usalama wa raia na mali zao katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi. Vilevile, Tume inavipongeza vyombo vya habari kwa kuzingatia haki ya kikatiba ya wananchi kwa kuwahabarisha kuhusu matukio na sera zilizokuwa zinanadiwa na wagombea na vyama vyao na elimu iliyokuwa ikitolewa na wadau mbalimbali katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi. Jambo hilo limetoa fursa kwa wananchi kuwasikiliza na kuwapima wagombea wa vyama mbalimbali na litawasaidia kuchagua viongozi sahihi siku ya upigaji kura.

Tume inawaasa wananchi wote raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuzingatia sheria na kanuni za nchi kwa kuhifadhi amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

Katika kipindi hiki cha siku zilizobakia kuhitimisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2020, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kutoa wito ufuatao kwa wadau mbalimbali:

1. Wananchi
Wajitokeze kwa wingi na kutumia vyema haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi watakaodumisha amani, umoja na mshikamano nchini na kuliletea maendeleo Taifa letu.

2. Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama
i) Wasimamie amani ili watanzania waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura katika hali ya utulivu na amani na kuchagua viongozi bora.

ii) Wanapotekeleza majukumu yao wazingatie maadili, waheshimu haki za binadamu na na mising i ya utawala bora na waepuke matumizi makubwa ya nguvu yasiyokuwa ya lazima.

3. Mamlaka zenye dhamana ya kusimamia uchaguzi
i) Zihakikishe uchaguzi mkuu unasimamiwa kwa haki na amani wakati wote.

ii) Wadumishe amani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa wazi, wenye amani na utulivu.

4. Viongozi wa dini
Waendelee kukemea maovu na kuliombea taifa katika kipindi hiki muhimu ili haki, amani, utulivu na upendo viendelee kudumishwa sasa na hata baada ya uchaguzi kumalizika.

5. Wagombea watakaoshindwa
Kwa kuwa katika kila ushindani ni lazima awepo mshindi na atakaeshindwa, wagombea watakaoshindwa wanaombwa wakubali matokeo ili kudumisha amani ya nchi yetu. Ambaye hataridhishwa na matokeo, ni vema akafuata mkondo wa sheria na kanuni zilizowekwa zinazoruhusu kudai haki badala ya kutafuta njia za mkato katika kudai haki ambazo matokeo yake yanaweza kuwa hasi.

Tume inawatakia Watanzania wote Uchaguzi mwema

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Imetolewa na:
Jaji (Mst) Mathew P. M. Mwaimu
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Oktoba 26, 2020
Tume hii ni ya serikali hivyo inapopongeza mauaji Zanzibar haishangazi.
 
Haki
Haki
Haki
Haki

Bila Haki amani itatokea wapi?
Bila AMANI haki itatoka wapi!?
Leo hii Libya, somalia na kwingineko kutaja kwa ufupi hawana amani, tujiulize je kuna haki kwao!?

Usidanfanyike, bila AMANI, bunge, mahakama na serikali vyote haviwezi kutekeleza majukumu yao na uonevu wa wenye nguvu utatawala.
 
Ukinyimwa chakula utakuwa na amani?
Wakichukuwa nyumba yako utakuwa na amani
 
Wakiku
 
Haiwezekani tudumishe AMANI bila kwepo HAKI

Umetoa mfano wa Libya na Somalia, huko AMANI ilitoweka baada ya watawala wa nchi hizo, kutoona umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa HAKI

Vivyo hivyo na TZ ndiko inakotaka kuekekea, kwa watawala wetu kutotaka kutokekeleza majukumu yao kwa HAKI hivyo kupelekea AMANI iweze kutoweka nchini kwetu

Mithali 34:14
Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Bila AMANI haki itatoka wapi!?
Leo hii Libya, somalia na kwingineko kutaja kwa ufupi hawana amani, tujiulize je kuna haki kwao!?
Usidanfanyike, bila AMANI, bunge, mahakama na serikali vyote haviwezi kutekeleza majukumu yao na uonevu wa wenye nguvu utatawala.
Kwani waliosababisha machafuko Libya ni nan kama sio wapinzani
 
Back
Top Bottom