Tamko la TCRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la TCRA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dingswayo, Oct 12, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii nimeiokota kutoka Michuzi:

  Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaowachafua baadhi ya wagombea wa Uraisi 2010
  Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, imekiri kupata taarifa za kuwepo kwa ujumbe unaosambazwa kupitia simu za kiganjani ambao umekuwa ukiwahamasisha wananchi kutokuwachagua baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

  Akihojiwa na TBC, Naibu Mkurugenzi wa TCRA, Richard Kayombo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha namba hizo huku akitoa rai kwa Wananchi kutokuzijibu au kusambaza ujumbe huo.

  "Tumepokea malalamiko mengi tu, na ujumbe unakuja kwenye namba ambazo 03588108226 na mwingine kwenye namba 03588976578. Kwa mwelekeo wa haraka haraka, hizi namba zinaonekana ni namba za nje ya nchi. Lakini kwenye teknolojia, chochote kinaweza kikatokea. Inawezekana ni kweli ni namba ya nje ya nchi, lakini laini inayotumika na mtu aliyeko kwenye nchi nyingine. Lakini vile vile, inawezekana ni ujanja wa simu kutoka kwenye mtandao" alisema Kayombo.

  Hata hivyo, Kayombo alisema TCRA itazuia matumizi ya namba hizo kwa sasa mpaka uchaguzi utakapokamilika hapo Oktoba 31, 2010.

  Aidha, wananchi wameaswa kutojibu wala kusambaza ujumbe wanaotumiwa katika simu zao ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na uchunguzi unaoendelea wa kubaini chanzo cha mtandao huo.

  Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya saa mbili ya TBC, tarehe 11 Oktoba 2010.

  credit source: Tamko la TCRA kuhusu ujumbe wa simu unaowachafua baadhi ya wagombea wa Uraisi 2010 -
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  My translation
   
 3. m

  magee Senior Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  :decision::decision:mmmmh.......uhuru wa maoni uko wapi????Sijaziona hizo sms ila kinachinipa shida kunaubaya kusema tusimchague fulani???
  Mmmh kumbe hatuko huru!!!!Nimeshangazw na hili!!!:A S 13::A S 13::A S 13:
   
 4. R

  Rayase Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwan hizo sms zinasemaje! Kuna mtu aliyepata atuambie jamani
   
 5. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi sijatumiwa, lakini jamaa zangu wametumiwa na jumbe hizo zimejaa uhuni kabisa. Majibu ya Kinana juu ya kuwadharau wapinzani na maudhui ya jumbe hizi kuhusu wapinzani zinafanana sana hata sijui kwa nini nisioanishe chama tawala dhidi ya upinzani. Sasa hivi damu kumwagika ndio maneno ya kila wakati ya viongozi wa ccm kiasi yanakera hata kuyasikia, maana mtu mzima anapodanganya waziwazi mbele ya watu wazima wenzake inatia kinyaa. Kweli mfa maji haachi kutapatapa, lakini ccm sasa wanatuburuza kutupeleka pabaya, hawajakubali demokrasia inayoruhusu kukubaliwa na kukataliwa. Wanaijua ya kukubaliwa tu.
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mimi nilipopata hiyo sms nilijibu na kuwakebehi kuwa, hawana lolote ni kutapatapa tu.
   
 7. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  My Translation
   
 8. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Msg inasema:Slaa ni mropokaji na mgonvi anatukana vyombo vya ulinzi na usalama.Anataka damu imwagike ili mradi aingie Ikulu.Tumkatalie kuigeuza nhi yetu Somalia,hii inatumwa kwa namba +3588108226
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nilipata hiyo sms inayomkashifu slaa kwamba ni mropokaji. pia nyingine inasema kuwa slaa anapambana na vyombo vya usalama hafai. nyingine inasema kuwa slaa anataka kuibadilisha tz iwe kama rwanda na burindi hivyo asipewe kura. ni crap na insults tupu.

  TCRA wanajua ni nani anayezituma ila wanapiga propaganda tu hapa
   
 10. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pia mimi nimepata kutoka namba hii +3588108226 ukisisitiza tusimchague Slaa,nasema enyi mlotumwa na Mafisadi nyumbani kwangu nikiwa na njaa na shida Sijawahi kuwaona hao Mafisadi kunisaidia.hata Ahadi zinazotolewa na Mgombea wa CCM NI HAKI YETU KUPATA HUDUMA HIZO,Barabara ,Madawa, Elimu iliyo bora ni wajibu wa Serikali kuwapatia wananchi wake si kutumia kuombea leo majukwani kuombea kura bali inawajibika kufanya hivyo.kama leo CCM inatuahidi Barabara kwanini hukujenga kabla Badala yake unaifanya ndio rugha ya kuombea. kampeni kama kisingizio.
   
 11. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naamini kama huo ujumbe ungekuwa unamchafua jk, huyo jamaa aliyetuma angekuwa lupango. Jana nilimsikia kaimu mkurugenzi tume ya mawasiliano, nikahizi kuna kitu anataka kuficha. Sehemu ya kwanza ya kumtafuta huyo mtu aliye tuma huo ujumbe ni nchi unakotoka through country code number na balozi wa nchi husika anapaswa kusaidia kuiarifu nchi yake kusaka mtu mwenye namaba hiyo nchini finland (+3). Lkn kaimu mkurugenzi alianza kubashiri kuwa ile namba inaweza kuwa ya kutengenezwa hapa nchini. Chadema wanawenza anzia kwa balozi wa finland awambie kwa nini ujumbe toka nchini kwake unaingilia siasa za tanzania.
   
 12. F

  Future Bishop Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ngadema nafikiri watu wa IT wanaweza kusaidia katika hili. Inawezakana aliyetuma yuko Tanzania na hayuko Finland with the current technology anything can happen. Ukiwa unatumia skype kwa mawasiliano yaani toka skype na kuongea na watu wenye simu (kwa kununua skype credit) unaweza pia kutuma message. Na ukituma message anayepokea ataona inatoka kwa mtu ambaye hajamsave kwenye simu yake. Simu inayopokea message kutoka skype itaonyesha skype name ya huyo mtu aliyetuma. Kwa hiyo kama skype name yangu ni future.bishop anayepokea message yangu kutoka skype itaonyesha imetoka kwa future.bishop na haitaonyesha namba yoyote. Kwa hiyo kama nikicreate skype name ya namba ya finland na nikatuma message kupitia skype utakachoona ni hiyo namba ambayo ndiyo itakuwa skype address yangu.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Siamini kama kuna watu wanazisupport izo msg
   
 14. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Mafisadi at work! Ufisadi wa 2005 kwa CCM wenyewe kw wenyewe sasa unaelekezwa Chadema. Hivi Kikwete hawezi kuingia kwenye ushindani bila mbinu chafu?
   
 15. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  TCRA na makampuni yote ya simu nchini hivi wanashindwaje kujua chanzo cha SMS hizo za kuwachafua wagombea? Hata zile zinazodaiwa kuwa na mionzi nazo wanashindwa kweli? wakati TCRA ndio wahusika wakuu wa mawasiliano nchini?

  Kwa uelewa wangu wa haraka haraka, kwa mfano mimi natumia laini ya Vodacom ambayo inatambulika na iliyosajiliwa pia natumia handset aina ya Nokia ambayo IMEI Number yake inatambulika na inajulikana na mtandao wakati simu iko hewani, pia inajulikana mahali popote. HIVI WANASHINDWAJE KUTAMBUA NAMBA HIZO?

  Hata mimi ni mmojawapo wa watu waliotumiwa ujumbe huo ambao ulikuwa kama ifuatavyo Nanukuu.

  "Slaa ni mropokaji na mgomvi anatukana vyombo vya ulinzi na usalama. Anataka damu imwagike ili mradiaingie Ikulu. Tumkatalie kuigeuza nchi yetu Somalia. <From +3588108226> 09.Oct.2010 23:41"

  Halafu ule utata wa simu zinazodaiwa kuwa na mionzi uchunguzi wake umefikia wapi?
   
 16. S

  Sheka Senior Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huku ndokuishiwa na ahadi za danganya toto, baada ya kubaini watanzania hawapo nao wanaanza kutumia kampeni chafu kama walivyofanya mwaka 1995 kwa kuonyesha video za mauaji ya Rwand tuwkataeni hao.
   
 17. M

  Msavila JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Swala hili la kumwagika damu sijui wanalipendea nini. Katika hostoria ya kumwagika damu iwe Rwanda , Ivory Coast na kwingineko ni serikali za vyama tawala ndo hutumia majeshi kuzuia mabadiliko. tuliokuwa na akili wakati serikali za kikomunisti zilipoanguka, majeshi hayakuingilila kati kwani lilikuwa swala la kisiasa na si mashambulizi toka nje. Majeshi yalipokataa kumwaga damu za wananchi ambao ndio sababu ya kuwapo kwao, wanasiasa walishangaa na serikali zikaanguka kama domino. Sasa kwetu hapa majeshi yana wasiwasi gani? kwani kitakachotokea ni mabadiliko ya kamanda mkuu wa majeshi na si katiba!!! Chonde chonde majeshi yaache siasa ifuate mkondo wake.
   
 18. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  What is the use of having TCRA kama bado hawajampata huyu mtu!!!

  Kama kweli wanasema ni ngumu kumfahamu basi TCRA si chombo kinachotufaa kuratifu mawasiliano TZ. Watu wasomi halafu bado wanaendekeza blah blah!!! Shittt!!!
   
 19. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hazikupita siku mbili Kikwete akiwa Songea akawaasa wananchi kuwa kuna wagombea wa vyama vya siasa wanahubiri umwagikaji wa damu na wanataka kutumia miili ya watanzania wasio na hatia kama ngazi za kupandia ikulu.
  Hiyo inaonesha kuwa tayari tumeshapata source ya hizo sms,kama sivyo basi jamaa amedandia treni kwa mbele,labda nae alipata hiyo sms halafu akakurupuka kusema.
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mimi nipatapo message za iana hiyo naweka kwenye ignore list yangu. Tena ninaiagiza simu yangu isipokee simu kama hizo tena. Kwa hoyo ukituma kwangu haiwi delivered.
   
Loading...