Tamko la Tanganyika Law Society (TLS) juu ya uamuzi wa kamati ya mawakili kumuondoa Bi. Fatma Amani Karume katika rejista ya mawakili Tanzania bara

Tanganyika Law Society

Verified Member
Oct 15, 2018
14
75
TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA TANGANYIKA LAW SOCIETY (TLS) JUU YA UAMUZI WA KAMATI YA MAWAKILI KUMUONDOA BI. FATMA AMANI KARUME KATIKA REJISTA YA MAWAKILI TANZANIA BARA NA UAMUZI WA WAKILI FATMA AMANI KARUME KUKATA RUFANI

Mnamo tarehe 2 Oktoba 2020 Baraza la Uongozi la Tanganyika Law Society (TLS) baada ya kuupokea na kusoma kwa makini Uamuzi wa Kamati ya Mawakili katika Maombi Namba 19 ya Mwaka 2019 baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Fatma Amani Karume, lilikaa na kuujadili. Baraza la Uongozi liliziona sababu zilizoifanya Kamati ya Mawakili kumkuta Wakili Fatma Amani Karume na hatia ya ukiukwaji mkubwa wa maadili ya taaluma ya sheria na kuamuru kuondolewa kwake katika Rejista ya Mawakili nchini.

Licha ya mambo mengi yanajitokeza mtu anapousoma uamuzi huo, Baraza la Uongozi liliguswa sana na mambo yafuatayo:

a. Namna ambavyo Mwanasheria Mkuu aliwasilisha upya malalamiko yake kwa Kamati ya Mawakili kinyume na amri na maelekezo ya Jaji Kiongozi Dr. Eliezer Mbuki Feleshi aliyoyatoa katika uamuzi wake katika kesi Ado Shaibu v. John Joseph Pombe Magufuli (The President of the United Republic of Tanzania) & wengine wawili (Misc. Civil Cause No 29 of 2018) ya kumuagiza Msajili wa Mahakama Kuu “ kuwasilisha madai ya kukiuka maadili ya kitaaluma yaliyomo katika mawasilisho ya mleta maombi na majibu ya mwisho ya mlalamikiwa pamoja na uamuzi huu kwenye Kamati ya Nidhamu ya Mawakili ili yaamuriwe.”

b. Muundo wa Kamati hiyo ya Mawakili kusikiliza lalamiko lililowasilishwa kwake na Mwanasheria Mkuu dhidi ya Bi. Fatma Amani Karume na uwezekano mkubwa wa kuwepo upendeleo au muonekano wa upendeleo;

c. Kupokelewa kwa ushahidi wa kieletroniki wakati shauri linaendelea ambao haukuambatanishwa kwenye lalamiko au katika Orodha ya Nyaraka zitakazotumiwa (kama ilikuwepo);

d. Ukubwa na ukali wa adhabu; na

e. Taathira ya uamuzi huo kwa uwakili/utetezi na uhuru wa mawakili Tanzania Bara.

Baraza la Uongozi, kupitia kwa Raisi wa TLS, liliwasiliana na Wakili Fatma Amani Karume ambaye alisema hakubaliani kabisa na uamuzi huo na yu tayari kukata rufani. Na hivyo basi, Baraza la Uongozi likizingatia wajibu wake mkubwa iliopewa na kifungu cha 4(1)(d) cha Sheria ya Chama cha Mawakili Tanganyika (Tanganyika Law Society Act Cap 307 R.E. 2002) unaoitaka TLS “kuwawakilisha, kuwalinda, na kuwasaidia wana taaluma wa sheria nchini Tanzania kuhusu hali ya utendaji kazi za sheria au vinginevyoliliazimia kwa kauli moja kutoa msaada wake kwa mwanachama wake, Fatma Amani Karume, kukata rufani dhidi ya uamuzi wote huo na Amri Andikwa ya Kamati ya Mawakili, na litampa msaada wote wa kisheria litakaloweza katika rufani yake kwa Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Limetolewa Jijini Dar es Salaam kwa Amri ya Baraza la Uongozi leo tarehe 6 Octoba 2020.

………………………………………

Dkt. Rugemeleza A.K. Nshala

Rais
 

Attachments

  • File size
    98.1 KB
    Views
    14

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,284
2,000
Asante sana Nshala, tyranic regime always surpasess rule of law.

Fatma kaonewa, ushahidi wa matamko yake kwenye tweeter haukuwa kwenye kesi ya Addo shaibu vs Jiwe.

Tuendelee kumtetea, i wish ningekuwa wakili ila huu upande wangu wa judiciary sina la kufanya.
 

bg_dg_dy

JF-Expert Member
Feb 27, 2009
541
500
Haujui kesi mahakamani zinaendeshwaje thats why u r being negative


Mahakama Kuu ya "USA" au ya Tanzania? Kama ya "USA" haki itapatikana, kama ya Tanzania, namtakia msaada na mkono wa Mungu baba Mwenyezi, mwenye wingi wa REHEMA!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,689
2,000
Bado Tundu Lisu baada ya Oktoba 28.

Tundu Lissu ni MWAMBA yule! Yaani ni zaidi ya JIWE!!! Huwezi kummaliza kirahisi rahisi tu.

Kama tu risasi zaidi ya 30 kutoka kwa kikosi cha watu wasiojulikana zilishindwa kumuondoa hapa duniani, baada ya hiyo Oktoba 28 nani atapata ujasiri wa kumbughudhi MWAMBA wa Tanzania! Na kipenzi pekee cha Watanzania wapenda Mabadiliko?
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,284
2,000
Kukata rufaa ni kutoa msaada au ni haki ya mtuhumiwa ?
vyote, huwezi kukata rufaa kwa shauri kama la Shangazi wa Taifa "Iron Lady" bila kuwa na Mawakili , tena wa kujitolea "

Ni haki kwakuwa ipo kisheria.
 

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,241
2,000
Sijaelewa. Aliondolewa na KAMATI hlf saiv anatetewa na BARAZA??

Hawa majaji wa3 wanawatoa nchi gani?
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,759
2,000
Kukata rufaa ni kutoa msaada au ni haki ya mtuhumiwa ?

Anakokata rufaa(kama haki yake ya mtuhumiwa) sio anakopata msaada wa kukata rufaa. Ni taasisi mbili tofauti

Kwahiyo TLS kama chama cha mawakili kinampa msaada mwanachama wao aliyefutiwa uwakili na Kamati ya maadili( Alitolea taarifa hili pia kwamba haiko chini yao). Baada ya kusambaa majina ya wale wajumbe wa Kamati ya maadili ya TLS wakina Said Mwema
 

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
1,435
2,000
Asante sana Nshala, tyranic regime always surpasess rule of law.

Fatma kaonewa, ushahidi wa matamko yake kwenye tweeter haukuwa kwenye kesi ya Addo shaibu vs Jiwe.

Tuendelee kumtetea, i wish ningekuwa wakili ila huu upande wangu wa judiciary sina la kufanya.

The door to active politics is wide open to anyone. A legal practitioner doesn’t have to politicize the profession. That’s simply unacceptable and a disgrace!

Ukiona mpaka washirika wako kwenye law firm wanakuambia shape up or ship out, ujue umetoka nje ya mstari.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,493
2,000
tUMALIZE UCHAGUZI KWANZA ASIJEISHIA SEGEREA HATA AJAPIGA KURA
 

Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,384
2,000
Aah..shangazi naye bwana...ilikuwa atulie kwanza..wangempa uwaziri Zanzibar!

Anakurupuka tu au ndio .. usanii mpya huo?

Tupo tunaangalia game!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom