Tamko la TAHLISO kuhusu udsm kufukuza wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la TAHLISO kuhusu udsm kufukuza wanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by WILSON J, Jan 11, 2012.

 1. WILSON J

  WILSON J Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTIONS STUDENTS' ORGANISATIONOFFICE OF THE CHAIRPERSON TAHLISO
  P.O BOX 474 MOB: +255754754417 +255717213600
  Email:makondapaul@gmail.com Email:tahliso@gmail.com
  TAARIFA YA TAHLISO KWA VYOMBO VYA HABARI11[SUP]st[/SUP] January, 2011Tumepokea kwa masikitiko na mshangao mkubwa juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na viongozi wa vyuo vikuu hapa nchini, kwani hatua hizi zinaendeleza kukandamiza haki ya msingi ya kila raia ya kupata elimu bila kubugudhiwa. Ndugu watanzania Hatua ambazo zimechukuliwa na uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Muhimbili na chuo cha CBE campus ya Dar es salaam ni unyanyasaji na ukandamizaji wa hali ya juu katika elimu yetu ya juu. Hakuna hata sehemu moja ambayo imeonyesha kujibu hoja za msingi ama madai ya msingi ya wana vyuo wenzetu katika vyuo nilivyoviainisha hapo juu na hii inaonyesha dhahiri viongozi wetu wa vyuo vikuu hawataki kukaa na kutafuta chanzo na suluhu stahiki ya migomo na migogoro katika vyuo, bali wanahangaika na matokeo ya matatizo ambayo ni madai ya msingi katika vyuo vyetu. Ndugu watanzania, Madai ya msingi ya wanavyuo hususani katika chuo kikuu cha Mlimani hayajapatiwa ufumbuzi na badala yake tunaona wanafunzi wakiendelea kufukuzwa katika mwendelezo unaotishia amani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kama haki ya kila raia wa kitanzania kutoa maoni yake, uamuzi huu umechukuliwa kwa haraka sana bila kupewa fursa ya kusikilizwa. kimsingi serikali yoyote ile ya chuo chochote kile ipo katika kutetea na kulinda maslahi ya wanachuo. Kwa hiyo basi serikali ya DARUSO ina haki ya kuhoji juu ya sababu zipi zimetumika kuwafukuza wanafunzi 51, kwa kufanya hivyo sasa inatimiza wajibu wake wa kila siku wa kikatiba, hapa ndipo tunashikwa na butwaa, iweje watu wanaotimiza wajibu wao wa kikatiba wafukuzwe chuo?,ina maana chuo hakitambui katiba ya DARUSO ? haya ni maswali ambayo hatuna majibu nayo.Ndugu WatanzaniaNilidhani chuo kikuu cha Mlimani ni chuo kikongwe ambacho kinatakiwa kuwa mfano (role model) wa vyuo vyote nchini badala yake kimeamua kuua demokrasia kwa kuwafukuza viongozi mbalimbali wa DARUSO akiwemo raisi, mawaziri na wabunge ambao walikuwa wanafanya vikao halali vinavyotambulika kisheria juu ya hatua gani zichuliwe kuwarudisha wanachuo wenzao. Sisi tuliamini hii ilikuwa ni njia muafaka ya viongozi wa DARUSO na menejimenti ya chuo kukaa meza moja na kuona hatma ya wanafunzi 51 na wala si kufukuza tena viongozi kama ambavyo imefanyika hivi sasa.Ndugu WatanzaniaNyakati Fulani Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema, naomba kunukuu "Taifa lolote lile ambalo vijana wake wasomi wanapiga magoti mbele ya watawala, litakuwa ni Taifa lililoparanganyika, kwani wasomi wana haki ya kukosoa na kupongeza katika kila hatua inayochukuliwa juu ya mustakabari wa nchi yao" mimi siko tayari kuwaona wasomi wakipiga magoti kwa dhana ya nidhamu ya uoga kwa watawala bali katika kulinda misingi ya kikatiba kwa kuheshimu uhuru wao wa kueleza fikra na dhamira yao kwa mustakabali wa nchi yao na wala sio kwa nia mbaya bali kwa kujenga nchi imara yenye kuheshimu haki ya kila raia (human rights) Ndugu WatanzaniaNatoa wito kwa watanzania wote wa kutokukubaliana na hali ya kufinya uhuru wa mawazo na demokrasia ambayo serikali na watanzania, wanaijenga kwa mustakabari wa nchi, na kwa mantiki hiyo umma wa wasomi una haki ya kutoa mawazo huru bila kuogopa uongozi wowote ule kwani hiyo ni haki ya kikatiba.Natoa wito kwa serikali na management za vyuo kuiheshimu katiba ya jamuhuri ya muungano inayotoa fursa na haki ya kufanya maandamo ya amani kwa watanzania wote.Naiomba serikali iingilie kati na kuzuia mara moja management za vyuo zinazogeuza vyuo kuwa sehemu ya ugandamizaji na unyanyasaji wa wanavyuo wanapohoji haki zao.Nawaomba wanavyuo wote popote pale walipo nchini tuwe na umoja na mshikamano katika kipindi hiki cha mpito kwani umoja ni ushindi wa Taifa. Binafsi tumejipanga kuwa pamoja na serikali za wanafunzi vyuo vikuu vyote ili kuhakikisha maslahi ya vijana wa vyuo vikuu yanalindwa bila kuchezewa na mtu yeyote. Tumeanza kuchukua hatua mbalimbali za kukutana na viongozi mbalimbali ili kuhakikisha haki inapatikana kwa ndugu zetu ambao wamekumbwa na dhoruba hili, na hivi sasa maongezi yanaendelea na waziri wa elimuMwisho naviomba vyuo vyote nchini visimame katika eneo lake. kwenye kukosoa vikosoe na kwenye kupongeza vipongeze kwa mstakabali wa nchi yetu. asipatikane hata mtu mmoja wa kujivuna na hali inavyoendelea nchini kwani chuo kikuuu ni sehemu pekee ya tanuru la fikra katika Taifa na wala sio sehemu ya siasa.
  Mungu ibariki TAHLISO, Mungu ibariki Tanzania .
  Asanteni kwa kunisikiliza.
  Paul MakondaMwenyekiti TAHLISO
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Thank you guys. Nawatakia mafanikio katika mazungumzo yenu na hao wenye inji...
   
 3. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hayo mazungumzo yatachukuwa muda gani? ikishindikana tangazeni mgomo kwa vyuo vyote nchini kushinikiza hili
   
 4. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Makonda ni mshirika wa serikali iliyopo madarakani.Ana jipya hapa?
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145

  ccm=makonda

  rais= brainless
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  tatizo ni nini sasa hapo? Kama kijana katoa mawazo mazuri haijalishi yuko chama gani. Mimi nakupongeza sana makonda kwa hayo mazuri mliyoandika na tunasubiri sasa utekelezaji, kwani yanayoendelea ni ukandamizaji mkubwa sana wa haki za wanafunzi na watanzania. Hivi vyuo viache siasa na kujikita katika ufumbuzi wa matatizo kwa kutumia taaluma na si mabavu kama wanavyofanya hivi sasa.
  Bravo tahiliso na tunasubiri utekelezaji wenu.
   
 7. u

  utantambua JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sinaga imani ni tahliso sorry
   
 8. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Kuna haja ya kuwasaidia hawa vijana! Haya ni matokeo ya vyeo vya kulipana fadhila!
   
 9. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  too much words with nod actions!!!!
   
 10. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Makonda the end will justfy what you wrote here, continue being focused and enhance demanded comitments.
   
 11. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Naskia eti UDSM wanafanyiwa hvyo coz walimzomea baba yake Riz1, akamwambia rafiki yake mukandakandambili awashughulikie, kwa hiyo nae alipopata sababu ndo kashikia hapohapo
   
Loading...