Tamko la SIKIKA kuhusu rushwa - Wizara ya Nishati na Madini

Hapa wakuu kuna maswali mengi.?
Hivi Rais wetu ajui au anajua bajeti ya Nishati na madini aliyowasilishwa na waziri husika.?
Je waziri mkuu naye ajuii kabisa kilichomo ndani ya bajeti husika.?
Je nani ni boss wa katibu mkuu Jairo?
Je kweli waziri wanishati na madini ajui tuhuma hizo.?
Nionavyo wajinga ndio waliwao.?au Je wanasubili nini?
Hivi Rais anavyosafiri nini kazi ya makamu wa Rais,? Waziri mkuu alisikika akisema mpaka Rais arudi ndo atowe ushauri?????

Mzee wa Rubisi,

The way this government works is that it had mastered the art of lies.
Ministers are almost ceremonial posts tu, hata maPS nao ni kama mapambo pale wizarani.
Ministers ni wanasiasa and often completely clueless.
The PSs are often a bit knowledgable, ndio watendaji.
The real decision makers are the technical advisors, these are often the directors of various idaras. Uchafu wote unaanzia hapa. Kwa hawa madirectors. Ngeleja and Jairo may not know a shit about the technical details but the directors do. The directors ndio wanawashauri. Wakidanganya then the entire ministry and country is screwed.
Mfano, kuna company A and company B bidding for power generation tender.
Plan A is a briefcase company, willing to cut a 10% facilitation fee to the directors and PS, inturn, company A wins the tender at very bad contract to the country, such as charging high tariffs but delivering substandard.
Company B is a proper established company, FCPA compliants and all, don't cut the 10% facilitation fees and their offer is actually beneficial to the country as a whole. Lower tariffs and superior standard delivery.
Well, these directors will make up stories to tarnish company B.
At the end, ndio tupo hapa tulipo na mikataba mingi.

To clean the system should start from these directors.

Saying all that, mwenye macho haambiwi tazama. President, ministers and PS should know better.
after all, as a leader, one is responsible for his or her subordinates mistakes. If they screw once, unawasamehe, twice, a warning, third, they get fired. If they steal, they should face jailtime. NOT TRANSFER THEM TO ANOTHER IDARA OR WIZARA.
 
Tuesday, 19 July 2011 21:26

Hoseah naye atangaza kuanza uchunguzi wa kina

Kizitto Noya na Ramadhan Semtawa

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya jana kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.Pinda alisema hayo, baada ya gazeti hili kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga Sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

"Suala hilo bado tunalifanyia kazi," alisema Pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na Rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. "Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."

Akizungumzia suala hilo la Jairo bungeni juzi, Pinda alisema: "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.

Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua."Tuhuma za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma."Tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DP kwa ajili ya utaratibu," alisema Shellukindo akiinukuu barua hiyo.

Kauli ya Dk Hoseah
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza uchunguzi wake juu ya madai hayo ya Wizara ya Nishati na Madini kuzichangisha taasisi zilizo chini yake fedha kwa ajili ya kufanikisha bajeti hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema jana kwamba tuhuma hizo ni nzito na tayari taasisi hiyo imeanza kuzichunguza.

Alisema taasisi yake inafanya uchunguzi kwa umakini na kwamba kila anayetuhumiwa atapewa nafasi ya kujitetea na kusisitiza kwamba ofisi yake inalichukulia suala la nishati ya nchi kwa uzito mkubwa."Tumeshaanza uchunguzi... jambo zito kama lile hadi Bunge linaahirishwa unafikiri tunaweza kuliacha hivihivi? Suala la nishati tunalichukulia ‘very serious’. Tutafanya uchunguzi wetu na tutaona matokeo baada ya kukamilika," alisema.

Lema alia na Ngeleja
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema jana aliomba mwongozo wa Spika akitaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja awajibishwe kwa tuhuma za rushwa zinazoikabili wizara yake.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo bungeni ikiwa ni siku moja baada ya wabunge kuikwamisha Bajeti ya Wizara hiyo.

"Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja asiwajibishwe kutokana na kitendo kilichofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye Waziri Mkuu alimwona kuwa na makosa katika kufanya ushawishi wa kuitetea bajeti ya wizara hiyo?" Alisema.

Lema alisema haiwezekani Katibu Mkuu kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwashawishi wabunge halafu waziri mwenye dhamana asijue kinachoendelea ndani ya wizara yake na hivyo akataka na yeye awajibishwe.Hata hivyo, akijibu mwongozo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema suala hilo limeshatolewa ufafanuzi na Waziri Mkuu na kwamba mjadala huo umeshafungwa.“Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 (1), Waziri Mkuu ameshaomba muda na kwamba suala hilo linakwenda kushughulikiwa... naomba tuwaache wafanye kazi inayostahili, hili jambo lipo administratively (kiutawala),” alisema Makinda.

Jairo anena
Licha ya kuendelea kumiminiwa tuhuma za kuchangisha fedha katika idara zilizo chini ya wizara yake, Jairo amekataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Niacheni.”Alisema hayo kwa simu jana akisema kwa sasa si wakati mwafaka kwake kusema chochote kuhusu tuhuma hizo:

"Kwa sasa sina majibu," alijibu kwa kifupi maoni yake kuhusu tuhuma hizo zilizoibuliwa bungeni juzi na Shellukindo.Alipoulizwa kama ana mpango wa kujiuzulu badala ya kusubiri uamuzi wa Rais alijibu: "Niache kwanza, naomba hili nalo nisijibu."
 
Wateule wa BWANA,karibuni mezani kwake..............Hawajibiki wala kuwajibishwa mtu hapo,wote waarabu wa PEMBA,wanajuana kwa vilemba
 
Jairo's cash demand must be investigated

Tuesday, 19 July 2011 21:59
THE CITIZEN

The scandal exposed in Parliament on Monday in which the permanent secretary for ministry of Minerals and Energy, Mr David Jairo, is said to have directed 20 agencies operating under the ministry, to contribute Sh50 million each, which would add to Sh1 billion), to facilitate approval of its 2011/12 Budget is distressing, to say the least.
The issue begs the question: Is this how our august House's affairs are conducted, in which case MPs (Names please!) have to be bribed using taxpayers' money, before they can endorse a government proposal?

While we agree lobbying is an old practice, common even in Western democracies, the idea of giving hefty bribes to lawmakers so that they can vote for or against a certain issue at hand would attract stiff penalty anywhere.

Why, that would not be facilitation but rather, a blatant violation and abuse of basic democratic processes.
As suggested in the PS's letter to the CEOs under his boss's docket, availing huge sums of money "has been a normal practice" whenever his ministry would be presenting its budget. Which is to say, the scam has always been there; as from when, only the culprits know!

And demanding issuance of money to, ostensibly, pay "officials who are usually present when the ministry's budget is being tabled", people who, as we all know, earn huge salaries, not to mention the hefty per diems, is most outrageous.

The funds the agencies deposited in the Dodoma NMB account, it is revealed, have all been withdrawn and it has not been made public into whose pockets they went to (We need all the names of these culprits including those who received bribes in previous years from the same Ministry) .If the PS's letter tabled in the House proves authentic, we expect the author(s) behind the demand to face the music.

Meanwhile, the government should throw a security ring around the whistle blower, Ms Beatrice Shelukindo, as she must have created powerful enemies already. This would encourage others to garner the courage to expose corruption that is increasingly eating into the very core of our body politic.

Hapa sioni lolote la maana zaidi aya hadithi tulizo zoea. Kwa kashfa kama hii kiongozi hahitaji kusubiri afukuzwe bali alipaswa ajiuzulu mara moja kwa hiari au shinikizo. Inaonekana Jairo ana kiburi kwasababu fulani.

Jairo alikuwa katibu wa Rais Kikwete na sijui uchunguzi gani utakaoweza kwenda ndani zaidi ya hapo kwa nchi zetu za Afrika. Huyu ana siri nyingi za mkuu na ndio maana kuna shida kumshinikiza aondoke, kinachofanywa ni kutaka kutupumbaza kwa kutumia PCCB.

Kazi ya PCCB ni kutafuta mianya ya rushwa na kuizuia kabla haijatendeka kwa uchache wa kusema. Inapotokea PCCB ikafanyia kazi taarifa za bunge, ni wazi hawakujua au walijua kinachoendelea lakini walikaa kimya. Taasisi ya namna hii haina public trust.

Ninashangaa Hosea anaposema suala la nishati wanalichukulia kwa uzito! uzito gani uliozidi ule wa Richmond ambayo yeye alishiriki kikamilifu kuficha uozo wake kwa taarifa za uongo. Hata alitakiwa kujiuzulu aligomea azimio la bunge. Leo tunawezaje kumwani mtu huyu kufanya uchunguzi wa Jairo? Yaani kesi ya nyani kula mahindi afanye uchunguzi tumbili!!

Zaidi ya hapo uchunguzi gani unahitajika wakati kuna barua, je DPP na DCI wanafanya kazi gani na wanasubiri nini. Utaona kuwa wote wanaogopa kutia mkono kwasababu wao ni wateule wa Rais kama alivyo Jairo.
Hukuna kitu tunasubiri changa la macho.
 
At first I thought CCM MP's were sheep being shepherded by the government to say "ndiyoooo" and "kwa asilimia mia" to every government and ruling party proposal. Now it is likely that most of these MP's over the years have traded their dignity and self respect for hand outs from government ministries. Mh is it possible that CCM MP's have been acting dumb all these years in exchange for cash?
 
Je kuna mtu ana mashaka kwa nini Tanzania imefika hapa ilipofika ; kwenye kiza totoro miaka 50 baada ya Uhuru, wakati takribani miaka 25 hivi iliyopita tulikuwa na umeme wa ziada? Jibu ni watawala wanafiki, wezi na mafisadi waliorithi utawala toka kwa Hayati Baba wa Taifa ambao kwa bahati mbaya walifaulu kumsadikisha kuwa walikuwa wafuasi wake watiifu hadi aliwaamini kuwaachia nchi. Viongozi hao ndiyo tulio nao hadi sasa na ndiyo waliosheheni ndani ya chama lao bovu, chakavu, lililosheheni walevi wa ufisadi nalenye kansa ya wizi wa umma, ufisadi na ubabaishaji uliorithishwa mpaka kwa vizazi vyao.
Sintashangaa kama nisivyoshangaa kumwona Ngeleja akibakia adamant bila ya kujiuzulu yeye wala katibu wake mkuu, bila shaka walikuwa wakitekeleza kazi waliyoelekezwa na mkuu wao ambaye naye ni mshiriki katikakashfa karibu zote zinazohusu nishati tangu 1994 hadi leo kwa nafasi mbalimbali! Jee Unamtarajia kiongozi wa namna hii kuchukua hatua yoyote?
Ufumbuzi wa gonjwa hili ni kudai ukombozi mpya utakaohakikisha CCM inatupwa chooni na kufukiwa kabisa. tanzania bila CCM si tu inawezekana bali itakuwa bora mara elfyu kuliko ilivyo sasa haswa ikizingatiwa kwamba hakuna kiongozi atakayetokana na CCM atakayekuwa na ubavu wa kupambana na Rushwa. Hawa kina Nape, Sitta, Mukama ni wasanii na wachumia tumbo tu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
yaani hawa jamaa ni wakufukuza kazi sio kujiudhulu tena,halafu wale wote waliotoa rushwa watajwe na waliopokea pia.
Urafiki katika siasa ni mwiko jamani,tumechoshwa na tume za uchunguzi yaani hadi mambo yaliyowazi tunaunda tume basi zifutwe taasisi za kudhibiti rushwa.
vyombo vya habari viwemstari wa mbele kutaka majina ya waliohusika hadharani maana wanaopewa hizo ripoti wanafungia chapati.
Fukuza wote kuanza upya sio ujinga.............
 
Je kuna mtu ana mashaka kwa nini Tanzania imefika hapa ilipofika ; kwenye kiza totoro miaka 50 baada ya Uhuru, wakati takribani miaka 25 hivi iliyopita tulikuwa na umeme wa ziada? Jibu ni watawala wanafiki, wezi na mafisadi waliorithi utawala toka kwa Hayati Baba wa Taifa ambao kwa bahati mbaya walifaulu kumsadikisha kuwa walikuwa wafuasi wake watiifu hadi aliwaamini kuwaachia nchi. Viongozi hao ndiyo tulio nao hadi sasa na ndiyo waliosheheni ndani ya chama lao bovu, chakavu, lililosheheni walevi wa ufisadi nalenye kansa ya wizi wa umma, ufisadi na ubabaishaji uliorithishwa mpaka kwa vizazi vyao.
Sintashangaa kama nisivyoshangaa kumwona Ngeleja akibakia adamant bila ya kujiuzulu yeye wala katibu wake mkuu, bila shaka walikuwa wakitekeleza kazi waliyoelekezwa na mkuu wao ambaye naye ni mshiriki katikakashfa karibu zote zinazohusu nishati tangu 1994 hadi leo kwa nafasi mbalimbali! Jee Unamtarajia kiongozi wa namna hii kuchukua hatua yoyote?
Ufumbuzi wa gonjwa hili ni kudai ukombozi mpya utakaohakikisha CCM inatupwa chooni na kufukiwa kabisa. tanzania bila CCM si tu inawezekana bali itakuwa bora mara elfyu kuliko ilivyo sasa haswa ikizingatiwa kwamba hakuna kiongozi atakayetokana na CCM atakayekuwa na ubavu wa kupambana na Rushwa. Hawa kina Nape, Sitta, Mukama ni wasanii na wachumia tumbo tu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Hakuna wakati tulikuwa na umeme wa ziada, umeme ulikuwako kwenye baadhi ya miji na vijiji tu. Naomba weka sawa historia yako, ikiwa hii leo chini 15% ya watanzania ndio wenye umeme, itakuwaje miaka 25% nyuma tuwe na zaidi ya 100%. Naona hapa kidoogo umechemsha.
 
At first I thought CCM MP's were sheep being shepherded by the government to say "ndiyoooo" and "kwa asilimia mia" to every government and ruling party proposal. Now it is likely that most of these MP's over the years have traded their dignity and self respect for hand outs from government ministries. Mh is it possible that CCM MP's have been acting dumb all these years in exchange for cash?

If that is the case, I have a feeling its more than just CCM MP's who are the culprits here. I wouldn't be surprised to see even the opposition was / is involved.
 
Wanasema bajeti ya Serikali ya Tanzania inadhaminiwa kwa kadiri ya asilimia 40 na Wahisani kutoka nje, huku asilimia 60 ni pesa za Serikali, lakini sitoshangaa kwamba hizo takwimu za bajeti wanazotoa Bungeni kila mwaka ni uwongo mtupu na ukweli ni kwamba asilimia 90 au zaidi ya bajeti ni pesa za misaada, wakati Serikali haichangii kile kiasi wanachotakiwa au wanachodai. Ndiyo maana hawana uchungu na rushwa za kiuwendawazimu kama hizi. Suluhisho hapa ni Wahisani kusimamisha kabisa misaada yote ya kusaidia bajeti ya Serikali kila mwaka.
 
If that is the case, I have a feeling its more than just CCM MP's who are the culprits here. I wouldn't be surprised to see even the opposition was / is involved.

Let's wait and see who were involved in this scandal.
 
If that is the case, I have a feeling its more than just CCM MP's who are the culprits here. I wouldn't be surprised to see even the opposition was / is involved.

It's possible but highly unlikely. CCM are the majority so if you have courted the majority of CCM you have no use for opposition votes. Unless you can point out a situation where opposition votes were needed to make a difference then your statement is highly unlikely. The votes of the opposition in parliament are usually more of a statement rather than any real power.

But umeeleweka.....
 
Tatizo la umeme linawahusu CCM tu; ndio walioliitengeneza, wakalidumisha na sasa tunavuna matunda yake. Huwezi kutenganisha tatizo la nishati na utawala/uongozi wa CCM.
 
Maneno mengi haya ya kuelimishana ni kwamba sisi wote hatuna akili ya kutosha kuelewa hata hili la wazi ambalo linaachilia maovu mengi yametendeka hivi hivi. Hizo taasisi, Tanesco iwamo, ndizo hazina hela ya mafuta tuko gizani, halafu wahonge 50m/=!

Tuna kazi moja tu kumfukuza na kuwafukuza wote wahusika leo na jana. Wa leo hakuna kusubiri ni kufukuza na rumande. Wa jana tuchunguze kwa ku-extract more information kutoka hawa wa leo wakati wakiwa rumande. Hakuna visingizio vya alikuwa anatimiza maelekezo ya nani maana kama yeye aliona haifai angejiuzuru na kama yeye hana akili kiasi hicho sisi hatuwezi kujua hayo maana sifa za jumla anazo kutetea nafasi aliyopewa ni wote ndani waende kualumiana huko rumande (kwenda mahakama ni njia moja ya kuwafikiria haki zao, kama zipo). Cheo ni dhamana hatuwezi kuendelea kuona wapo wakati kuna watendaji wazzuri wengi na inawezekana uzuri wao ndio unaowanyima nafasi hizi. Kwa hili ni kazi moja tu.
 
At first I thought CCM MP's were sheep being shepherded by the government to say "ndiyoooo" and "kwa asilimia mia" to every government and ruling party proposal. Now it is likely that most of these MP's over the years have traded their dignity and self respect for hand outs from government ministries. Mh is it possible that CCM MP's have been acting dumb all these years in exchange for cash?
I doubt if they have changed, what has changed so far is the country's political landscape. They had no options, people are suffering you cant just stand up and say "naunga mkono hii hoja" when there is nothing concrete in it to alleviate some of these problems. Remember it was the same CCM MP's who were cheering when Sitta called opp Mp's "hypocrites" for wanting to reduce unnecessary spending, and when Pinda said "hata wao wanamezea mate". Yet they cheered again when he said they will do their best, even reducing "Posho" spending to tackle power rationing. I dont think they have changed, they had no options. They have to appease their voters and their weak party at the same time. It's a difficult task.
 
CCM is a BIG mistake. Jamani our country is very rich than you can ever immagine. Jk timua wote kuanza upya sio ujinga!
 
Tatizo la umeme linawahusu CCM tu; ndio walioliitengeneza, wakalidumisha na sasa tunavuna matunda yake. Huwezi kutenganisha tatizo la nishati na utawala/uongozi wa CCM.
Huwezi kutofautisha tatizo la umeme na SAP,ambayo muasisi wa CDM aliipigia debe mpaka tukaifuata.
 
Mzee wa Rubisi,

The way this government works is that it had mastered the art of lies.
Ministers are almost ceremonial posts tu, hata maPS nao ni kama mapambo pale wizarani.
Ministers ni wanasiasa and often completely clueless.
The PSs are often a bit knowledgable, ndio watendaji.
The real decision makers are the technical advisors, these are often the directors of various idaras. Uchafu wote unaanzia hapa. Kwa hawa madirectors. Ngeleja and Jairo may not know a shit about the technical details but the directors do. The directors ndio wanawashauri. Wakidanganya then the entire ministry and country is screwed.
Mfano, kuna company A and company B bidding for power generation tender.
Plan A is a briefcase company, willing to cut a 10% facilitation fee to the directors and PS, inturn, company A wins the tender at very bad contract to the country, such as charging high tariffs but delivering substandard.
Company B is a proper established company, FCPA compliants and all, don't cut the 10% facilitation fees and their offer is actually beneficial to the country as a whole. Lower tariffs and superior standard delivery.
Well, these directors will make up stories to tarnish company B.
At the end, ndio tupo hapa tulipo na mikataba mingi.

To clean the system should start from these directors.

Saying all that, mwenye macho haambiwi tazama. President, ministers and PS should know better.
after all, as a leader, one is responsible for his or her subordinates mistakes. If they screw once, unawasamehe, twice, a warning, third, they get fired. If they steal, they should face jailtime. NOT TRANSFER THEM TO ANOTHER IDARA OR WIZARA.

Mkuu umesema ambayo kila siku yananikera na that is what TZ is all about! as i said back in a day that i am sometimes so embarrassed to introduce myself infront of brainiacs as Tanzanian!!. A leader suppose to be loyal to their country kinyume na TZ leaders who are lacking patriotism!, guys this country is going down!! Goshhhh!
 
Back
Top Bottom