Tamko la Shighela kwa wabunge wa CCM kuhusu sheria ya mifuko ya hifadhi za jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Shighela kwa wabunge wa CCM kuhusu sheria ya mifuko ya hifadhi za jamii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Aug 5, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Nimemwona Shighela wa UVCCM akiwaasa wabunge vijana wa CCM  kushikamana kuipinga sheria kandamizi iliyopitishwa na bunge mwezi april?

  Je, wabunge hao vijana wa CCM wakati inapitishwa hawakuwepo bungeni? Pia je kama walikuwepo, je hawakuisoma na kuielewa kuona kama ina tija kwa manufaa ya wachangiaji? Je shighela haoni kama anapambana na serikali yake ambayo ndo iliyoomba sheria hiyo ibadilishwe kwa usitawi wa mifuko hiyo?

  Na pia je alikuwa wapi muda ule kama mdau kupinga sheria hiyo aanze kulalama sasa? pia je hao wabunge wake wa CCM haoni aningia nao tifu huku wao walionana inaafikiwa wakasema ndiyo!

  CHANZO :ITV taarifa ya saa mbili usiku
   
 2. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  ndio kazi walioisahau huko nyuma,wao ndio speaker wa umma
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Wametao ushauri mzuri!
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hiyo mifuko ni WIZI mtupu hata Startv wametoa taarifa ya Wachimbaji wa Dhahabu wakilalamika mbele ya mbunge wa Kisarawe Mh. Jaffu na nina uhakika hata J. Mnyika Mbunge wa Ubungo naye ameshalitolea tamko hilo linalohusu eti YTALIPWA MAFAO YAKO BAADA YA KUFIKISHA MIAKA 55.

  Hizo hela kwanini wameenda jengea majengo km UKUMBI wa Bunge, UDOM nk Mm ni mwajiriwa wa Shirika ambalo liko ICU na saa yoyote linakufa kwa hiyo sitapewa mafao tena,

  Ila nikatafute kazi kwenye kampuni ingine na mafao yangu yataendelezwa hadi nikifika miaka 55, wapi na wapi km elimu yangu nindogo naomba hela zangu kwani huko hazizai wala kupata riba
   
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Namtetea mwanachama mwenzangu wa shighela kwa hoja yake hii. Ukitaka kumfunga simba kengele lazima uwe na vison, mission, plan A na B na kikubwa uzingatie TIME FACTOR! na kubwa kuliko uzingatie ANY RISK SHOULD BE REWARDER (CHEAP PUBLICITY).

  Shinghela anajua kabisa analolifanya na amezingatia hivo vigezo hapo juu, wakati mswada unapita bungeni angeweza kureact ila reaction yake ingemezwa na MAGAMBA, kwa kujua hilo aksubiri fo THE PERFECT TIMING ambayo nia sasa hakuna linalobamba kwenye media, sasa antwist media to ENJOY HIS MOMENT! hapo utakuwa umeelewa why now?

  TIME FACTOR NDO ILIYOMCOST KAFULILA NCCR. Vision yake ilikuwa superb, plan ilikuwa perfect, na power alikuwa nayo alipoteleza ni timing tu! Sasa kijana wetu yupo makini.

  Kuhusu kupambana na serikali hilo jambo dogo sababu siasa za bong hasa chama chetu EVERY BODY FOR HIMSELF GOD FOR US ALL. Kumbuka 2015 inakuja na hajapa publicity toka ameingia so its now or never kujihakikishia kajimbo.
   
 6. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Binafsi siipendi CCM na naichukia sana lakini sioni tatizo kwa mwana CCM kama Shigella kupinga maamuzi ya wabunge wa chama chake kumbuka Shighela si mbunge,pia kama inavyodaiwa kuwa kipengele cha fao la kujitoa kilichomekwa huenda hata baadhi ya wana CCM walizungukwa.
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kama serikali imeshindwa kulipa fedha za nssf/ppf basi ssra waitishe tenda ya kuuza majengo yote yaliyojengwa na mifuko then hela irudi kwenye hifadhi...

  Pili mtoa mada ebu mfatilie mnyika vizuri kuhusu upitishwaji ya hyo sheria,kumbuka mswada ulivyoletwa hawakuweka hiko kipengele,serikali imekiingiza kijanjajanja tu..
   
 8. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Ndugu yangu mswaada tangu unatayrishwa mpaka kupitisha lazima utausoma tu.Ikumbukwe hata kama walizungukwa kwenye kamati, lakini kwenye kupitisha wabunge hawa wapashwa kwa umoja wao kuukataa, usingepita.

  Nina kumbukumbu kuwa wabunge wa upinzani waliupigia kelele na kuukataa. Lakini kwa sababu kuna syndicate (kamati ya CCM) walielekezwa kupitisha huku wakijua ni sheria kandamizi.

  Ni wakati ule kam kweli sheria zingekuwa zinapitishwa kwa maslahi ya umma usingepita, ila kwa sababu mambo mengi bungeni yanapita kwa wingi wa wabunge wengi wa CCM.Ni vyema kuzingatia maslahi ya umma kuliko kukumbatia chama.

  Kwa mtazamo wangu shighela kama raia wa tanzania ana haki ya kusema, lakini akumbuke CCM ndo iliyopitisha sheria hiyo.bac apingane na chama chake
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sometimes naona kama wabunge wa CCM wanataka ku'take advantage ya kujizolea umaarufu katika swala hili.
  Awali walitumia wingi wao kuwakomoa wananchi, leo wamegeuka.
   
 10. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Mnyika anaposema bunge dhaifu mnachukia, hata kama kilichomekewa, wakati wa kupitisha wangekikataa ilikuweka schedule of amendment, lakini hapa kilichotumika ni wingi wa wabunge wa CCM kupitisha bila kuchambua na kukataa.

  Tatizo wapinzani wakipinga wanaonekana wanachuki kumbe wanahoja.Udhaifu katika bunge lazima urekebishwe
   
 11. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Shigela yupo sahihi watupe chetu tusepe
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  Hivi nyinyi watanzania mnadhani mna bunge au mfano wa bunge!Lile ni kama kundi la walanchi kila kitu ndio.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Katika suala hili Wabunge wooooote; wa CCM na upinzani wameonyesha kuwa si wawakilishi wa wananchi. Tumewatuma watuwakilishe lakini wanaenda kupitisha sheria za kutukandamiza.

  Tunashtuka wanajifanya eti sheria irudishwe ifanyiwe marekebisho utadhani sheria hii ilipitishwa na Bunge la Uingereza. Huu ni ukora tu.

  Wao wanaangalia masilahi yao zaidi; wakati wa sheria ya mchakato wa katiba kwa kuwa iliwahusi basi wabunge wa CDM walionyesha machungu hadi kutoka nje ila kwa hili la wafanyakazi wanyonge jamaa hawakuona kama kuna shida.

  Wabunge wote walikaa kimya. Leo wengine wanaleta usanii tu mbona wakati wa kujadili hii sheria hawakuonyesha uchungu au walikuwa wamelala wote?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wangekataa tungewasikia wakipiga kelele. Kumbuka sheria ya kutunga katiba mpya jamaa walikataa na wakaonyesha kwa vitendo kwa kutoka nje na mwisho wake Rais akawasikikiza na sheria kurekebishwa. Lakini kwa hili hatukusikia wakisema kitu. Wabunge wote hapa wametuangusha.
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hii kitu sababu haikugusa maslahi yao , waliona poa tu raiua wa kawaida tufe tuu na njaa wao wakineemeka
   
 16. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dawa ni kuchagua wabunge wengi wa upinzaniu katika uchaguzi ujao ili sheria za Bunge zibadilike wawe wanapiga kura badala ya kuitikia Ndiooo
   
 17. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60

  hapo ulipo ndo umegonga kiusahihi, sheria hii ni mbovu kuliko, sasa kwa sababu imewakera watanzania walio wengi .sasa kwa sababu wanaona chama chao ndo kilihusika kuwakomoa,wanajikosha mbele ya jamii.tujifunze kutetea masilahi umma, badala ya kusubiri ukakasi mpevu kwenye jamii
   
 18. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mwenye picha ya Shigela atuwekee hapa. Tafadhali
   
 19. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Binafsi naona 2015 ni mbali sana,nataka nikachukue jimbo la kalenga fasta,mgimwa ni kama karatasi au digdig2[kisimba hela].
   
 20. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja kiukweli tunahitaji pesa zetu leo. Hatuna uhakika wa kuishi hiyo miaka 60. Time value of Money. Huyu JK vipi?
   
Loading...